Moise Katumbi ana nguvu kuliko Serikali ya Kongo?

Moise Katumbi ana nguvu kuliko Serikali ya Kongo?

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,793
Reaction score
5,053
Inabidi Wakongo tukumbushwe kuwa Moise Katumbi sio Rais wa nchi.

Mambo ya kulalamika kuwa Moise Katumbi ndiyo sababu ya maisha kuwa magumu nchini eti anaongea na nchi jirani wasilete chakula Kongo ili kuchafua utawala wa Felix hayo ni uongo

Mambo ya kulalamika kuwa yeye ndo ana filisi maendeleo ya nchi ni uongo.

Sijui yeye ndo sababu za pesa zetu kushuka thamani.

Sijui kwanini hataki kusaidia rais kupigana na M23.

Mambo ya usalama watu wanakufa maiti zinaokotwa kwenye mifereji lawama zote kwake.

Huyu sio rais ni raia wa kawaida tua, lawama tupeleke kwa Felix sio kwa Katumbi.

Kama kweli anafanya haya yote si anaonyesha ana nguvu kuliko serekali yetu? Kwanini tusimpe nchi kama mtu ana uwezo wa kumiliki serekali yote mikononi mwake?

Je, nchi itamshinda?
 
Wakongo wanashangazaga sana. Badala ya kulaumu serikali yao wanalaumu wengine. Jeshi la kongo kazi kukimbia adui na kula rushwa na kunyanyasa raia.

Halafu wanataka majeshi ya nchi zingine kuja kupambana na m23. Halafu unakuta wakongo kusifu tu tshisekedi. Tangu wageni wameshutumu fardc ndio wameanza kupiga adui na sasa huenda wakatimua adui.

Wakongo waache kuchanganywa akili na adui yao rwanda kirahisi. Wageni hawawezi kupigana mstari wa mbele hii ni kazi ya fardc.
 
Kinacho niuma moise amekuwa kama yeye ndo rais wa nchi watu wanaandama
Kila kukicha lawama zote wanapeleka kwa kitumbo sijui kama Moise ndo amegeuka kuwa rais au
 
Congo inapaswa kupatikane kichwa mmoja mwenye vision ,uzalendo na asiye na ulafi aitawale ile kwa mkono wa chuma , ainyooshe ,kuna wapumbavu wengi ile nchi , nchi haiwezi kuendelea kwa kuwa na watu wapumbavu kama wale
 
Back
Top Bottom