Baada ya kutumikia
Simba SC kwa takribani miaka 11, nahodha wa klabu hiyo
Mohamed Hussein ameagana rasmi na Wekundu wa Msimbazi kufuatia
mkataba wake kumalizika na
kutoongezwa tena.
View attachment 3411217
Mohamed Hussein, maarufu kama "Zimbwe Jr", ameacha alama kubwa ndani ya kikosi hicho akichangia mafanikio lukuki ikiwemo ubingwa wa
Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mataji ya
Kombe la FA na safari mbalimbali za kimataifa kwenye michuano ya CAF.
View attachment 3411216
Tetesi zinaeleza kuwa Mohamed Hussein huenda akatua Yanga SC baada ya kuondoka Simba, huku akihusishwa na ofa ya kuvutia iliyowekwa mezani na mabingwa hao wa kihistoria.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Yanga SC inadaiwa kumpa
Mkataba wa Miaka Miwili wenye masharti yafuatayo:
- Pesa ya usajili: Shilingi milioni 300
- Mshahara: TSh. Milioni 25 kwa Mwezi
- Gari: Harrier Anaconda mpya
- Tiketi za ndege: Vacation ya kifahari Dubai