MOF/BOT na Elimu ya Uchumi kwa Umma

mutanim

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
203
77
Kwa muda mrefu tumeona taasisi mbalimbali za kiserikali zikitoa elimu au kujiweka wazi kwa umma kwa kuelezea madhumuni ya huduma zao kwa wananchi; kwa uchache hingera zao TRA, TANESCO, NHIF, NSSF, PPF,DSE na NHC kwa kujiweka sawasawa katika eneo hilo la elimu kwa umma.

Haijapata kusikika taasisi zinazoshughulikia uchumi, wizara ya fedha na benki kuu kutoa habari zinazohusu mwelekeo wa uchumi wetu baada ya uchunguzi na upembuzi mwingi na adilifu wanaofanya siku nenda siku rudi.

Kwa ujumla kuna faida nyingi sana kwetu sisi wananchi iwapo taarifa hizi zinawezakupatikana kupitia vipindi vya vyombo rahisi vya habari, mfano TV na Redio ( taarifa zaweza kuwepo kwenye tuvuti ambapo upatikanaji unaweza kuwa na changamoto nyingi), tukizingatia kwamba vipo vyombo vya kitaifa vinavyoweza kupata kipato kwa kutengeneza na kurusha vipindi hivi.

Mambo ambayo yanaweza kuwekwa wazi kwa watu kupata taarifa za haraka ni kama kiwango cha kubadilisha fedha, riba za ukopaji kwa mabenki, mauzo ya miamala ya serikali, utabili (economic forecast) wa hali ya uchumi walau kwa mwezi mmoja ujao na kuongeza wigo pale uzoefu utakapoongezika n.k.

Ukiangalia nchi zinazoendelea mfano Kenya, Nigeria na Afrika Kusini, wanatoa sana taarifa na pia elimu ya namna hii, kwa mfano kupitia TV stations kama SABC n.k.

Faida kubwa inaweza kuonekanma kwa uchumi wetu kuwa unaotabirika, (predictable), kupima viashiria vya ukuaji au udondokaji kwa haraka na kuchukua hatua stahiki; kupanga kwa uhalisia bei za bidhaa na huduma (mfano mafuta na nauli za mabasi, mabasi ya kwenda kwa kasi) bila kupata upinzani kwani taarifa zitakuwapo.

Ni matumaini yangu kwamba mawazo ya namna hii si mapya na inawezekana wahusika wanayo malengo ya kufanya haya, basi kama ninaweza kuwashauri basi ingependeza waharakishe utekelezaji wake, wanaweza kujipanga kupata hata dakika tano tu za snap reporting ambazo watalipia kidogo sana na kutufikishia ujumbe wananchi ili tuwe na taarifa sahihi na kufanya maamuzi mapema.
 
Mawazo mujarabu haya,lakini kwa sababu wengi wenye mamlaka na mambo haya hawana exposure ya kutosha,wataona hakuna umuhimu wa jambo hili.
 
Ni hoja kubwa na muhimu kwa ustawi wa nchi yetu. Hili tatizo ni kubwa mno Tanzania. Siyo taasisi hizo tu. Tukijifananisha na Kenya tunaudhaifu mkubwa katika utoaji taarifa wa Huduma au bidhaa zetu. Itapendeza waliotajwa na sisi wengine popote tulipo tusambaze kazi zetu na namna ya kutupata.
 
Hili ni wazo muhimu sana hasa swala la FOREX maana uelewa upo ila sio wa kutosheleza hata DSE pia ni ya kusaidia maana kama hatuna tu stock market kwasasa
 
As long as Magufuli hatafanya mabadiliko ya maana pale BOT lazima tutegemee business as usual!!
 
Back
Top Bottom