Modern Day Berlin Conference in Dar!


Inaweza kuwa propaganda mkuu maana Nkrumah si aliuwawa na CIA?
 
Wadugu,

My argument hapa ni kuwa Wakoloni walipotaka kujipatia mali na kujineemesha na wakakutana Berlin 1884, sisi hatukuwa na wa kututetea au kuwaambia hapana mnachofanya si sahihi wala haki.

Tukatawaliwa, tukaendendelea kuzalishia mataifa makubwa tulipochoka kutawaliwa (kisiasa) tukaamua kupigania Uhuru na kudai Uhuru. Tumepata Uhuru (kwa namna fulani hasa Kisiasa) lakini tumeendelea kuwa koloni la kiuchumi tukitawaliwa.

Sasa maudhui yangu si kuwalaani wakoloni au kutafuta kisingizi kuwa ni Wakoloni au Ubepari-Ubeberu. Bali ni kujihoji sisi kama tulilalamika kuhusu Berlin Conference na matokeo yake miaka 120 iliyopita, iweje leo hii kwa hiari tunaendelea kuburuzwa pamoja na sisi kuwa na kiti kwenye mkutano?

Ninahokasirikia si Mkoloni, yeye tunamjua. Najikasirikia nafsi yetu wenyewe na utashi wetu wenyewe kuwa sasa hivi, kwenye mfumo wa kisiasa na kiuchumi kidunia tuna uwakilishi na tuna uwezo (tukihiyari) kukataa kuburuzwa au kuambiwa cha kufanya na nchi Tajiri ambazo lengo lake ni kuendelea kutunyonya na si kutuona tukipata nguvu sawa kiuchumi na hata kisiasa kama wao.

Ndio maana nikasema najinukuu .

Lengo kuu ni kuhoji, kwa nini hatuundi mfumo wetu wenyewe bila kunyenyekea tunachoambiwa? Na ndiyo maana ya kusema tuna uwakilishi na hata tunaanda mikutano ambayo hatima yake si neema kwa Afrika bali kwa Wakoloni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…