Vitalis Msungwite
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,318
- 7,985
Katika pitapita zangu mitandaoni hasa hapa JF, nimeona utapeli wa namna mbalimbali. Baadhi ni online marketing kupitia makampuni hewa, kuunganisha chanel kwenye ving'amuzi, kubadili line kuwa za chuo, forex, wale wanaouza saa kwa mill 5+(jina nimesahau) n.k.
Kuna group moja la whatsapp niliona promo ya mobistock na nikajiunga nayo. Niliweka 10,000 kama kianzio na nikakatwa 1000 kama ada ya kujiunga. Kwa kuuza vocha za 9000 nikapata 360 kOama kamisheni.nikaongeza 5000 kuweka nikakatwa 200.
Wizi uko hivi, ghalama ya kujiunga 1000 iliyokatwa ilihitaji vocha za 25000 ili kujifidia kwa kamisheni ya 4% kwa vocha au 100,000 kwa kuunganisha vifurushi vya ving'amuzi na luku kwa 1% kwa kila muamala.
Sasa kwa kukatwa 200 kwenye 5000 niliyoongeza inamaana kuwa hapo unafanya biashara hewa, kwasababu hiyo 200 ndio kamisheni kwa kuuza vocha za kiwango hicho. Maana yake hata hela yako haitarudi kwasababu utauza 4800 na kupata jumla hasi.
Kama kutakuwa na maelezo au ufafanuzi zaidi nipotayari kufuta kauli yangu ila kwasasa nasema "mobistock ni wizi mwingine kwa njia ya mtandao"
Nawasilisha