Mo xtra kinywaji kipya

Hizi energy drinks naishiaga kuzisikia na kuziona ila hata ladha yake siijui
 
Naomba kuuliza nini athari ya hizi energy kiafya?
Madhara yake hayana tofauti sana na Watumiaji wa Viagra ambapo huonekana wakiwa hodari sana kwa nguvu nyingi wakati husika wa kujamiiana lkn hurudi ktk hali ile ile pale tu waachapo kutumia.

Mwili ulio na afya bora hauhitaji kemikali zozote za ziada kuliko;

*Kumcha Mungu ili uwe na amani "AYUBU 22:21"
*Mapumziko utapochoka
*Chakula bora na cha asili
*mazoezi ya kiasi mara kwa mara, kumbuka "too much is harmful/chochote kikizidi kiasi huleta madhara"
*Maji mengi si ya baridi
*Matunda
*Kutoendekeza msongo wa mawazo tokana na hali yoyote ile/Free stressed acceptance
*Kutoendekeza starehe

NB:
Ushauri wangu siyo sheria so una uhuru wa kuufata au kuupuza.
 
Zinanguvu Kweli Kweli! Nguvu Zote Unazozojua Wewe Ikiwa Ni Pamoja Na Nguvu Za Kiume. Ukitaka Kupiga Show Ya Ukweli, Tupia Mbili Hivi, Halafu Kama Hutoona Matokeo Njoo Niambie.

Kuna Vijana Nilikuwa Nafanya Nao KAZI Ngumu Kupakia Mizigo, Wanatupia Hizo Energy Drinks, KAZI Inaenda Chapchap...
 
Hakuna ulazima wowote wa kutumia ikiwa baadaye ni kupata madhara chungunzima ktk afya yako zaidi ya ulimbukeni tu wa kuiga iga Watu jinsi wanavyohangaika na kila waonacho mbele yao hawapitwi nacho hata kama kina athari ktk maisha yao kiafya.

Kwanini unywe kinywaji chenye masharti tele?
Hujiulizi kwanini uwekewe masharti mengi ikiwa hicho kinywaji kina faida nzuri kwa afya yako?
Utapungukiwa nini hasa ikiwa hutatumia hicho kinywaji?

Mfano:
Naamini na sitaacha kuamini kamwe kuwa kunywa maji mengi yaliyochemshwa na yasiyo ya baridi ni muhimu sana kwa afya zetu Binadamu, Je nani aliyewahi kukatazwa asinywe maji mengi kwa kigezo cha kuathiri afya yake mwilini?

Azam energy drink ina masharti mengi sana tena si ya kitoto.

MFANO.
*Usinywe zaidi ya kiasi cha chupa 1 kwa siku 1(24hrs)
*Usinywe nusu saa kabla haujaenda kulala
*Mwanamke mjamzito hapaswi kabisa kuinywa
*.....
Sasa hayo mateso yote ya nini? Si bora tu uwe huru kutumia vitu ambavyo uliruhusiwa na Mungu vitokanavyo na matunda, mbegu mbegu, mimea, mizizi na viumbe vilivyomo baharini 7bu ndivyo vinavyoendana na afya zetu Binadamu.

KUMBUKA:
Binadamu tumeumbwa na udongo ndiyomaana penye mimea tofauti ktk ardhi hupatikana na rutuba nzuri kwa kilimo, halikadhalika nasi Binadamu yatupasa tuzingatie vyakula vitokanavyo na visababishi vya rutuba ya ardhi.
Akasema hii ina nguvu kuliko ile. Hivi vinywaji huwa vina nguvu gani inayozungumziwa? Kwa wale watumiaji wa hivi vinywaji tafadhali vina nguvu gani?
 
Bahati mbaya hivi vinywaji vyote kuanzia soda na hivi vipya vipya vyote nina mwaka wa 11 situmii mkuu. Wala sina mpango hata wa kuonja
Kaka tuko pa1, tangu 2010 niliachana na soda, vyakula na vinywaji vya kemikali, nyama nyekundu zaidi ya kula samaki tu.

Kufa nitakufa tu wala sitaishi milele lakini siyo 7bu kunifanya nisitumie akili alizoniumba nazo Mungu kuwa na tahadhari ktk kuboresha afya yangu.
 
Marehemu Mzee Mengi angekua kwenye battle na Mo & Bakhresa basi angekuja na I-ENERGY.. IPP, ITV, I-touch, I-Energy.
r.i.p mzee wetu.
 
Mi nina mzigo wa Mo energy wazaman..ngoja nisiuuze kwanza nisubiri, ikitokea mabadiliko tu, bei napandisha maradufu
 
Wakazi wa Dasalama mnafaidi sana,Yaani Mo Energy Mikoa mingine bado hata haijafika tayari wameshabadili kuwa Mo Extra.Juzi kati pasaka hii nilitembelea Mujini kiukweli MO ENERGY NI BORA ZAIDI YA ENERGY zingine nilizozionja.
 
Marehemu Mzee Mengi angekua kwenye battle na Mo & Bakhresa basi angekuja na I-ENERGY.. IPP, ITV, I-touch, I-Energy.
r.i.p mzee wetu.
Kuna energy ya Coca-Cola sijajua kama inazalishwa hapa Coca-Cola kwanza au kule bonite moshi
 
Sijawai kunywa ila mwezi uliopita nilikosa redbull dukani nikanunua mo energy yaani nimekuwa addicted vibaya mno nishazinywa kama 6 hivi tangu mwezi uliopita
 
Asante mkuu kwa kuwajuza kiufasaha mkuu. Hasa hivyo vinywaji wanaviripukia hawa vijana under 30/28 years. Wengi hawana mpango wa kufuatilia kipi kina madhara watumie na kipi hakina madhara. Kizazi cha digital. Hivyo vinywaji naviona tu kwa mbali,naona tu vijana wanavyovilipukia. Nashangaa utasikia hiki kina nguvu sana. Kinywaji kiwe na nyongeza kweli na masharti? Unajua ukitamani kinywaji ujue una kiu. Ukinywa maji kila kitu kinakuwa sawa
 
Asante pia kwa kanielewa vzr, karibu tena.
 
Aisee unazijua vizuri....ktk zote hizo Mo energy ndio tamu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…