Mo Dewji kuzungumza na mashabiki wa Simba SC hivi karibuni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mohammed Dewji, mwekezaji mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, amesema klabu haijapotea na iko kwenye mchakato wa kujijenga upya. Katika ujumbe kwa mashabiki, Dewji amesema huu si wakati wa lawama bali mshikamano na hatua chanya.

Ameeleza kuwa Simba imejenga kikosi kipya, kuimarisha benchi la ufundi na kuweka msingi wa mwelekeo mpya. Ameahidi kuzungumza na mashabiki moja kwa moja hivi karibuni, huku akisisitiza kuwa mbele kuna mwanga na matumaini mapya.

IMG_5525.jpeg
 
Wapenzi wa Simba,

Najua mioyo yenu imebeba maswali mengi. Kama Rais wenu, msione nimekaa kimya wakati tumepitia kipindi hiki kigumu. Kupambania Simba ni wajibu wangu.

Huu siyo wakati wa lawama — ni wakati wa kusimama imara, kuwa kitu kimoja, na kuchukua hatua sahihi za kuleta mabadiliko chanya.

Katika siku chache zijazo, nitazungumza na nyie moja kwa moja. Kuna kazi kubwa inaendelea, na kuna matumaini ya kweli.

Simba haijapotea. Tumekuwa kwenye kipindi cha mpito — tumejenga kikosi kipya, tumeimarisha benchi la ufundi, na tumeweka msingi wa mwelekeo mpya. Msimu huu tumefika mbali zaidi ya matarajio, na msimu ujao tunarudi kwa nguvu mpya.

Naomba tuendelee kuwa wavumilivu. Tunahitaji kufanya marekebisho makubwa. Tuendelee kusimama pamoja kama familia moja.

Mbele yetu kuna mwanga. Na kwa pamoja, tutarudi tukiwa imara zaidi, wenye njaa zaidi, na wa kishujaa zaidi.
 
bhai kama yupo siriaz vile,ataokota okota wachezaji alafu huyo dubai msala anamuachia mzee wetu mangungu
 
Mohammed Dewji, mwekezaji mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, amesema klabu haijapotea na iko kwenye mchakato wa kujijenga upya. Katika ujumbe kwa mashabiki, Dewji amesema huu si wakati wa lawama bali mshikamano na hatua chanya.

Ameeleza kuwa Simba imejenga kikosi kipya, kuimarisha benchi la ufundi na kuweka msingi wa mwelekeo mpya. Ameahidi kuzungumza na mashabiki moja kwa moja hivi karibuni, huku akisisitiza kuwa mbele kuna mwanga na matumaini mapya.

View attachment 3402020
Kujenga timu kuna hitaji majadiliano, (maswali na majibu), Simba sc siyo ya mtu binafsi
 
Mohammed Dewji, mwekezaji mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, amesema klabu haijapotea na iko kwenye mchakato wa kujijenga upya. Katika ujumbe kwa mashabiki, Dewji amesema huu si wakati wa lawama bali mshikamano na hatua chanya.

Ameeleza kuwa Simba imejenga kikosi kipya, kuimarisha benchi la ufundi na kuweka msingi wa mwelekeo mpya. Ameahidi kuzungumza na mashabiki moja kwa moja hivi karibuni, huku akisisitiza kuwa mbele kuna mwanga na matumaini mapya.

View attachment 3402020
Kwenye uchaguzi alimleta Manzoki bila shaka kwenye mkutano huu atakuja na picha ya Achraf Hakimi! 😁😁😁
 
Mbele yetu kuna mwanga. Na kwa pamoja, tutarudi tukiwa imara zaidi, wenye njaa zaidi, na wa kishujaa zaidi.
Hii ni Yohana 3:27 nimemwelewa sana

27 Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lolote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.
 
Kuna haja gani mashabiki kulalamika wakati rais wenu anasema msimu huu mmefika mbali zaidi ya malengo yenu ya msimu
Msimu uliopita walikuwa nafasi ya 3 NBC premier league mwaka huu ni wa 2 na wameshiriki kombe la shirikisho Hadi fainali kama mshindi wa 2 wamepata bilioni 3

Yanga wamepata kombe la ubingwa wa NBC na makombe mengine eti wameambulia milioni mia nane namnukuu Aden Rage
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom