MO Dewji kutoa 200m kumbakisha Mkude, Ajibu, Kotei na Banda

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,043
114,496
Wachezaji muhimu wanataka kusepa Simba baada ya mikataba yao Kuisha Simba walimshirikisha tajiri Mohamed Dewji Kwa Ajili ya kuwasaidia kuwabakiza wachezaji hao mhimu.

Kutokana na ripoti ya kocha wa Simba ameshauri waongezwe wachezaji sita wa kazi golikipa mmoja, beki watatu, Winga mmoja, na Mshambuliaji mmoja, Katika ripoti hiyo inatabainisha kuwa wachezaji ambao hawajaisaidia timu hata kwa asilimia 20 waachwe hata kwa kupelekwa Kwa mkopo. Pia ripoti ikasisitizia wachezaji mhimu wasiondoke kwenye timu kama mikataba imeisha waongezewe.

Baada ya ripoti hiyo kukabidhiwa kamati ya utendaji ya kupelekwa Kwa kamati ya usajili chini ya Zacharia Hanspope ikajadiliwa na ikaonekana Mapendekezo ya Omog yatafuatwa Kwa asilimia zote tatizo likaja Kwa wachezaji mhimu ambao wanamaliza mikataba ikawa changamoto kubwa. Ndio kamati ikapeleka barua ya ombi Kwa tajiri kijana MO aweze kuwasaidia.

Baada ya Mo kupokea barua hiyo aliwakubalia Simba Kwa Sharti moja tu fedha ambayo ataitoa iwekwe kwenye mchakato wa mabadiliko ya Simba. Mjumbe mmoja kutoka kamati ya usajili ambaye ni rafiki wa Mo ameagizwa kuzungumza na wachezaji wanne (Mkude, Ajibu, Kotei na Banda) ili kuona namna ambavyo wanaweza kubaki katika tetesi za usajili Mkude anataka milion 70 na kuendelea, Ajibu anataka Milioni 50, Banda na Kotei wote wanataka milioni 40 kila mmoja mambo yakienda Sawa MO atatoa milioni 200 kuwabakiza Nyota hao.

Mpaka sasa Simba imetumia zaidi ya Milioni 200 kuwasajili Nyota watano watatu kutoka azam (Manula, Kapombe, Bocco) Jamali Mwambeleko kutoka Mbao na Yusuph Mlipili kutoka Toto . Ikiwa Manula Milioni 70, Kapombe milioni 50, Bocco milioni 47, Mwambeleko milioni 30, na Mlipili milioni 10 .
 
Najua mashabiki maandazi hawatanielewa. Ningekuwa mimi ndio Hanspope/Kaburu ningewabakiza Kotei, Banda na Ajib. Huyo Mkude asepe zake. Hajui hata maana ya kapteni. Kila siku migogoro yeye, mara asusie timu, mara aondoke kambini wakati ligi inaendelea, mara naenda yanga mpaka anachosha. Aende tu, hiyo namba yake walishacheza wakina Nikodemus Njohole, Leny, chuji atakuwa yeye asepe zake tu tumeshamchoka.
 
Najua mashabiki maandazi hawatanielewa. Ningekuwa mimi ndio Hanspope/Kaburu ningewabakiza Kotei, Banda na Ajib. Huyo Mkude asepe zake. Hajui hata maana ya kapteni. Kila siku migogoro yeye, mara asusie timu, mara aondoke kambini wakati ligi inaendelea, mara naenda yanga mpaka anachosha. Aende tu, hiyo namba yake walishacheza wakina Nikodemus Njohole, Leny, chuji atakuwa yeye asepe zake tu tumeshamchoka.
Nakuunga mkono mkuu
 
Ni jambo zuri lakini kama wanataka kusepa pia anaweza kuwaacha wakasepa kwani hata wakibaki wanaweza kuwa kama wameshinikizwa hivyo wanaweza wasitimize wajukumu yai vizuri
 
Back
Top Bottom