Pesa yoyote anayopewa mtu kama mtu kwa kum-motivate kama unavyosema ni rushwa kama kazi ya hiyo fedha haipo na haijulikani ni malipo ya nini? basi huo ni ushawishi, Mbunge ange wawezesha waalimu kujua kuvua samaki siyo kuwapa samaki, sidhani kama tunachagua wabunge iliwatugawie fedha potelea mbali hizo fedha kama ni safi au chafu, Mbunge ana nafasi pana ya kutetea na kudai haki za wananchni ndani ya Bunge na katika vikao vya Halmashauri na hiyo ndiyo kazi ambayo mbunge anapashwa kuifanya kama MO hafanya hayo yote na hata kama yeye ni msamalia mwema basi aache Ubunge aendelee na usamalia mwema bila Ubunge! yah inawezekana na nadhani afanye hivyo, kila Ijumaa watu wakajipange kwake kupokea chochote aachie wanaoweza kuishika serikali wafanye kazi ya Ubunge.
Hawa ni wafanyabiashara wachafu ambao wanafaidi kutokana na kulala kwa serikali hivyo mara zote watu kama hao utumika kuuwa nguvu za Umma na Bunge dhidi ya serikali, kitu amabacho hakikubaliki na hakifai hata kidogo, ebu niambie iwapo tukiwa na takribani nusu ya wabunge kama MO, tutakuwa na serikali ya aina gani? na kutakuwa na faida gani kuwa na Bunge!? waalimu hawa shida ya Tsh.50,000.00 mbona hatukumsikia wakati wa malalamiko ya kudai malipo ya waalimu ambayo yalitaka kuperekea mgomo mkubwa wa waalimu Tanzania kwa kudai malimbikizo yao!
Shida ni uwajibikaji kwa maslahi ya Umma, rushwa ni rushwa tu hata kama inatolewa Italy au Marekani bado ni rushwa.