MO awashangaza walimu singida awapiga na 50,000 kila mmoja, ukumbi walipuka kwa vigelegele

Basi kwa Taarifa yenu Tundu Lissu atatoa Tsh 100,000 kwa kila Mwalimu kwa Walimu 808! Subirini
 
Nina mashaka na ubora na uadilifu wa hawa waalimu. Tutegemee nini kutoka kwa wanafunzi watakaopitia kwenye mikono yao? Hata mtu akisema wanalipwa mishahara kidogo, hiyo elfu 50 itamaliza matatizo yao? Wameshanunuliwa na hawataweza kumuwajibisha mbunge wao kamwe!
 
wengi wenu muna donge na wivu kwa kuwa hamkupata nyie inawauma sana hongera muheshimiwa Dewji kwa moyo wako wa kizalendo hio si rushwa na umeoneshga ubinadamu zaidi maana naamini hakuna aliewapa nauli ya kuja kwenye huo mkutano,hakuna,wewe ni zaidi ya binaadamu wengi waliokoment humu wana chuki kwa kuwa wawapendao hawana uwezo wa huo na moyo huo hongera sana Muheshimiwa Dewj mungu akuzidishie ulipopunguza akupe zaidi na zaidi inshaallah
Napinga Waalimu kupewa hiyo hela kwasababu zifuatazo:

1)Huu mpango sio endelevu. Atawapa hizo fedha mara ngapi? Pia kuna makundi mengine kama askari na manesi, wao atawapa lini? Badala yake angepambana ndani ya CCM na bunge ili maisha ya waalimu yaboreshwe. Mfano mdogo, mwalimu mwenye shahada moja (ya miaka 4) anata mshahara nusu ya anaopata nesi mwenye cheti ktk serikali moja ya Tz. Haya ndio mambo ya kupigania. Hii elfu 50 itaponya njaa ya siku 1 tu, lakni ukiboresha maisha ya mwalimu, hata familia yake itafaidika.
2)Waalimu karibu wote wamevalisha T-shirt zenye picha ya MO. Hii gharama ya kumtangaza MO inazidi hata elfu 50 walizopewa. Tukiangalia juu juu, tanaweza kufikiri waalimu wamepata T-shirt na elfu 50, kumbe wamepewa kazi ya kumtangaza MO kwa miaka kadhaa kwa sh.elfu 50. Hii inawadhalilisha waalimu.
Mwisho, inasikitisha kwamba hii tabia ya viongozi kugawa vijizawadi kwa wananchi imemea kila mahali siku hizi. Hii tabia inapaswa kupingwa maana inaua dhana ya viongozi kuwakilisha wananchi. Nani atampiga MO kwa kutowapigania wananchi wake kisera na mipango endelevu kama ameshawapa watu elfu 50? Mwananchi gani atamwajibisha Mo kwa kutowawakilisha wananchi wake vizuri. Mwananchi atakuwa amekosea kufikiria Mbunge ni mgodi unaotema fedha?
Siwaonei gere waalimu na zawadi waliyopata, nawatetea maana naelewa madhira wanayopata. Alichofanya Mo ni kupata "cheap popularity"!
 
Basi kwa Taarifa yenu Tundu Lissu atatoa Tsh 100,000 kwa kila Mwalimu kwa Walimu 808! Subirini
Akifanya hivyo nae atastahili kuzomewa. Kutoa fedha once in a while hakuwezi kumletea anaepewa hizo fedha mabadiliko ya kweli!
 
ninachoona mimi apo ni jezi za ccm,,nikadhani niza cwt~~~~~~~hivi ni mkutano wa walimu ama wa ccm,,,,,,,,,,,alafua hao hao ndio wanaopewa kipaumbele katika kusimamia uchaguzi~~~~~hivi .....utakuwa wa haki kweli,,,,,,,,,,,,au ni mtumikie kafiri upate ujira wako ,,,,,,,cpati picha kama ningekuwa mmoja wao alafu nipepiga full chadema combat,,,
 
Hivi nani angekataa hizo pesa kati yenu nyie mnaotoa maneno mengi kabla ya kuanza kuuzungumzia uhalali wake? Halafu Mh Zitto yeye anataka kupeleka pesa yake ya posho jimboni, ile sio rushwa? Inawezekana na yeye MO ni pesa yake ya posho ila yeye kaamua kugawa kwa walimu, kuna shida hapo? Jamani hivi siku hizi hata ukitaka kumsaidia mtu ni rushwa? Hawa waalimu hebu angalieni walivyochanganyikiwa na hiyo Tsh 50,000, hivi wakipewa angalau wakaendeleze miradi yao ya kilimo ni tatizo?
 
Pesa yake ya Posho (40million)! we kweli umelala

Zito pia amekwambia anataka kupereka kugawia watu kama karanga!? au amekwambia anataka kuwekeza katika maendeleo ya Jimbo lake! Ukumbuke kuwa hatulaum bila kufiri kama unavyodhania na kufanya wewe, kama MO angewekeza hizo fedha katika maslahi mapana ya maendeleo ya Waalimu kwa maana ya halisi ya waalimu hakuna jinsi hayo maendeleo yange kuwa na sura na Rushwa lakini kuita watu na kuwagawia fedha ni Rushwa dhahiri labda kama unahoji kuwa nani anaujasiri wa kukataa Rushwa hiyo ipo wazi angalia hizo picha, idadi na aina ya washiriki utagunguwa kuwa si wote walienda kujidhalilisha katika hilo tukio (Sura zinazoonekana hapo ni za Wazee siamini kuwa hakuna waalimu vijana huko singida, wapo na tunawajuwa) ambao hawakufika hapo hii ina maana walikuwa na ujasiri wa kukataa hiyo rushwa ya Tsh.50,000.00 maana huo si mwisho wa matatizo bali ni mwanzo wa kujifunga mnyororo wa utumwa kwa MO.

Hapa ndipo kwenye tatizo ambalo tunataka liondoke hapa Tanzania, kuwafanya watu maskini kwa makusudi hili kuwatayarisha kukubali lolote pale wanaposikia harufu ya noti! Umaskini ni mbaya tunataka uondoke haraka sana na hawa wakina MO hawataki umaskini uishe kwasababu watakosa watumwa, umaskini ndio chanzo cha matatizo yote, MO ana anapashwa kuhojiwa na TAKUKURU katika hili jambo.
 
Kwako hiyo hela ndogo ila kwa mwalimu itamsaidia.wakiiba hela mnawasema,wakitoa hela mnawasema.au kwasababu ya chama chake?ingekuwa mwanasiasa wa chama kingine am sure watu wengi wangemsifia
 
pongezi kwa MO kutoa hiyo milioni 40
lakini tatizo ni je hii ndio njia ya kutatua matatizo ya au ndio kawanyamazisha hao
walimu kwa hiyo milioni 40?
this is just power of money apigane walipwe vizuri sio kuweka gundi mdomo anapokuja kwa walala hoi anawanunua kwa pesa wanayompa kupitia posha na msharaha mnono hali matatizo yanaendelea
mimi naichukulia hii kama uwekezaji kwa MO kuliko kwa walimu
...anajaribu kupinga kauli ya "bosi wake" wa zamani (Mzee Mkapa) kwa kuonyesha kwamba yeye kama mbunge atawaendeleza walimu na sio hiyo mishahara yao. Sasa hicho ndicho kilimpeleka bungeni kweli???? (kugawa pesa au kutetea pesa zinazotolewa na serikari kuelekea huko ziwafikie salama?). ...lakini nimeona kwenye thread moja hapa Mh. MO anatuhumiwa na 'mambo fulani fulani', amshajibu!?
 
thanks jf guys mna mawazo mapana cna am hap,coz huyu anajipa uhakika wa kuchaguliwa next time,elfu hamsin ki2 gan bwanaa,ka mlivyosema bora apambane hata waongezewe twenty kwenye salar kuliko hyo 50 ya 1 day
 
Pesa yake ya Posho (40million)! we kweli umelala

Zito pia amekwambia anataka kupereka kugawia watu kama karanga!? au amekwambia anataka kuwekeza katika maendeleo ya Jimbo lake! Ukumbuke kuwa hatulaum bila kufiri kama unavyodhania na kufanya wewe, kama MO angewekeza hizo fedha katika maslahi mapana ya maendeleo ya Waalimu kwa maana ya halisi ya waalimu hakuna jinsi hayo maendeleo yange kuwa na sura na Rushwa lakini kuita watu na kuwagawia fedha ni Rushwa dhahiri labda kama unahoji kuwa nani anaujasiri wa kukataa Rushwa hiyo ipo wazi angalia hizo picha, idadi na aina ya washiriki utagunguwa kuwa si wote walienda kujidhalilisha katika hilo tukio (Sura zinazoonekana hapo ni za Wazee siamini kuwa hakuna waalimu vijana huko singida, wapo na tunawajuwa) ambao hawakufika hapo hii ina maana walikuwa na ujasiri wa kukataa hiyo rushwa ya Tsh.50,000.00 maana huo si mwisho wa matatizo bali ni mwanzo wa kujifunga mnyororo wa utumwa kwa MO.

Hapa ndipo kwenye tatizo ambalo tunataka liondoke hapa Tanzania, kuwafanya watu maskini kwa makusudi hili kuwatayarisha kukubali lolote pale wanaposikia harufu ya noti! Umaskini ni mbaya tunataka uondoke haraka sana na hawa wakina MO hawataki umaskini uishe kwasababu watakosa watumwa, umaskini ndio chanzo cha matatizo yote, MO ana anapashwa kuhojiwa na TAKUKURU katika hili jambo.
Naona umeandika kwa hasira saana. Well double standard bado ipo tu hata ukigeuza kiswahili. Mmoja ametoa kwenye group na mwingine kwa individuals, na wote wametoa pesa. Sasa kipimo cha maendeleo, ni objective. Na kwa kuzingatia hali ya walimu wengi huenda mwingine hapo anakwenda kumlipia ada mwanae au hata matibabu. Hivi hayo sio maendeleo? Sasa tafsiri ya rushwa nayo ni pana, hivi ametoa in exchange of what? Kwahiyo siku hizi marufuku kusaidia?
Kwenye hizo picha huoni vijana? Unatumia miwani au unaona kawaida? MO amechangia miradi mingi saana huko Singida kwahilo ninamtetea labda tuongeze chumvi ya propaganda ya vyama.
 
Ona.... unavyowakilisha uvivu na uzembe, kazi kupenda bwereree tu. Mtu atoe 50,000 kwa watu karibu ya elfu moja wewe unafikiri ana lengo zuri huyu? Yeye ni mbunge, fedha za serikali zinachotwa mamilioni kwa mamilioni na sijawahi kumsikia hata siku moja akihoji. Rasilimali za taifa zilitoroshwa yeye kimya... halafu leo eti anajifanya kuwahurumia. Hawa ndio wale masadukao amabayo Yesu alitutahadharisha tujiepushe nao kwani hupenda kutoa sadaka mbele za madhabahu kwa uwazi ili kila mtu awaone...
 
Waalimu wa UPE yaani UPEPO wanaishi kwa shida halafu wanadanganyika kirahisi.
 
...anajaribu kupinga kauli ya "bosi wake" wa zamani (Mzee Mkapa) kwa kuonyesha kwamba yeye kama mbunge atawaendeleza walimu na sio hiyo mishahara yao. Sasa hicho ndicho kilimpeleka bungeni kweli???? (kugawa pesa au kutetea pesa zinazotolewa na serikari kuelekea huko ziwafikie salama?). ...lakini nimeona kwenye thread moja hapa Mh. MO anatuhumiwa na 'mambo fulani fulani', amshajibu!?
yepi madawa ya kulevya mbona unatutega
au ndio ile niangushega dhambi zako mwenyewe
kama ni hiyo tuhuma awezi kuwa na wasi wasi nayo leo
kuna miaka minne mpaka 2015 maana mtoto wa mkuu mzima
naye ni mtuhumiwa in short RiZ ONE
 
hiyo ni rushwa, msimung’unye maneno, akome la sivyo tutamuanza kibaraka wake mazala tumalizie na yeye.
 
Back
Top Bottom