MO awashangaza walimu singida awapiga na 50,000 kila mmoja, ukumbi walipuka kwa vigelegele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MO awashangaza walimu singida awapiga na 50,000 kila mmoja, ukumbi walipuka kwa vigelegele

Discussion in 'Jamii Photos' started by nngu007, Jun 13, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nape Nnauye not all business people who joined the politics are gready; there are some good business people whom because of Azimio la Arusha and Tanzanian Style of Socialism, they are more dedicated to our people more than heavy ranking CCM leaders whom love to drive around and abuse the population...
  “ The ultimate success in the work of building socialism in Tanzania-aselsewhere-depends upon the people of this nation. For any society is onlywhat the people make of it. The benefits to the people of a socialist societywill depend upon their contributions to it-their work, their co-operation forthe common good, and their acceptance of each other as equals andbrothers.”
  Julius K. Nyerere, 1968

  [​IMG]
  Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akizungumza na walimu 808 wa shule 43 za Msingi Manispaa katika hafla fupi iliyoandaliwa na ofisi yake kwa ajili ya kukutana na walimu hao ili kubaini changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

  Na Hillary Shoo, Singida.
  Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji (MO) amewashangaza walimu wa shule za Msingi Manispaa ya Singida pale alipowapa posho ya shilingi 50,000 kila mmoja wakati wa hafla fupi ya kuzungumzia changamoto zinazowakabili walimu hao.

  “Ndugu zangu walimu kwa kuwa leo hii nimefurahi kukutana nanyi hapa na kuzungumzia changamoto zinazowakabili katika kutekeleza kazi zenu za kila siku posho ya leo kila mwalimu atapata shilingi 50,000 .” alisema MO na kusababisha ukumbi mzima kulipuka kwa nderemo na vifijo.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki na walimu hao kwenye ukumbi wa chuo kipya cha ualimu Misuna Dewji aliwashukuru walimu kwa kukichagua chama cha CCM na kukipa ridhaa ya kuongoza nchi.
  Aidha alisema heshima waliyompa pamoja na wananchi wa jimbo hilo anaienzi na kuithamini kwa moyo wake wote kwani anatambua umuhimu wao katika jimbo hilo “Nani kama mwalimu, walimu waliitikia hakuna.”

  Mapema Kaimu Ofisa Elimu wa Manispaa ya Singida Ramadhan Labito alimweleza Mbunge kuwa walimu wanakabiliwa na changamoto nyingi ikwemo ukosefu wa madawati na uchakavu wa vyumba vya madarasa katika shule nyingi za msingi.

  Labito alitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa nyumba za walimu maeneo ya vijijini, kukopeshwa vyombo vya usafiri, kupatiwa viwanje vyenye hati, kupatiwa mikopo mbalimbali yenye masharti nafuu, kuimarishwa kwa vituo vya kulelea watoto yatima kititimo na Kompyuta mashuleni.
  Zingine kwa mujibu wa Kaimu Ofisa elimu Labito ni kuchimbiwa visima vidogo mashuleni ili upatikanaji wa maji kwa ajili ya kutunza mazingira ya shule yawe mazuri, kuuziwa vifaa vya ujenzi kwa bei poa pamoja na umeme wa jua kwa maeneo ya vijijini.

  Akijibu changamoto hizo MO alisema amezipokea na zile ambazo ana uwezo nazo atazitekeleza mwenyewe haraka iwezekanavyo lakini nyingine ambazo ziko nje ya uwezo ataziwasilisha serikalini kwa ajili ya utekelezaji.


  [​IMG]

  Walimu wa shule za msingi Manispaa ya Singida wakimsikiliza kwa makini Mh. Dewji kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Misuna.


  [​IMG]

  Walimu wakilipuka kwa nderemo na vifijo mara baada ya MO kuwatangazia posho ya 50,000 kila mmoja walimu hao.


  [​IMG]

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya
  Singida Salum Mahami akizungumza katika hafla hiyo.


  [​IMG]

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Yona Maki akizungumza kwenye hafla hiyo.

  [​IMG]

  Katibu Mwenezi wa CCM Singida Mjini Hassan Mazala alikuwa MC kwenye hafla hiyo.


  [​IMG]

  MO akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Mtamaa, walioketi mbele kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Yona Maki, Katibu wa CCM Mjini Mary Maziku na Kaimu Ofisa Elimu Manispaa ya Singida Ramadhan Labito.


  [​IMG]

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Salum Mahami akisalimiana na MO.

   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  pongezi kwa MO kutoa hiyo milioni 40
  lakini tatizo ni je hii ndio njia ya kutatua matatizo ya au ndio kawanyamazisha hao
  walimu kwa hiyo milioni 40?
  this is just power of money apigane walipwe vizuri sio kuweka gundi mdomo anapokuja kwa walala hoi anawanunua kwa pesa wanayompa kupitia posha na msharaha mnono hali matatizo yanaendelea
  mimi naichukulia hii kama uwekezaji kwa MO kuliko kwa walimu
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Bora hizo Nguvu za Pesa kuliko Midomo mitupu inawafukuza wananchi kwenye Ardhi zao hawapati chochote... ile pesa zinaenda kwenye Matumbo ya hao Mafisadi ndani ya CCM
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ni heri mwandishi angesema Waalimu wa CCM ingeeleweka kwani huu unaonekana kama mkutano wa CCM na kama kawaida yake mgao haukosi. Mgao wenyewe unaweza kuwa peremende, kanga au pesa lakini lisiloeleweka hasa ni kwa nini Waalimu wavae sare za CCM ?
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mo amedhalilisha waalimu na kuwapa Rushwa adharani hii nchni ya ajabu sana!

  CCM wanapenda kuanzisha mambo amabayo nina uhakika kama yakifanywa na wapinzani hawata kubali hata siku moja na utasikia watumishi wa serikali hawapaswi kushiriki katika mambo ya kisiasa; Katibu mwenezi wa CCM, waalimu wa shule za msingi, na Mkurugenzi wa Manispaa huu ni mchanganyiko wa watu gani? kama katibu mwenezi wa CCM hasinge kuwepo ningesema labda ni Mkurugenzi amekutana na waalimu wake na Mgeni rasmi alikuwa Mbunge!? lakini ilivyotolewa taarifa hata haijakaa vizuri hata kidogo.

  Huyu Mkurugenzi amejihaibisha kabisa, hakupaswa kushiki kuitia aibu serikali huku akijua yanayofanyika ni kinyume na utaratibu kabisa ni bora angewaachia waalimu na MO wenyewe ili likizuka na kuzuka yeye apate mlango wa kutokea, hawa ndio wakurugenzi wa kuokota mitaani.

  hakiak "Njaa mwana malevya, shibe mwana malegeza!"
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hakuna jipya, huyu katoa rushwa. Inapaswa akamatwe apelekwe sello. Viongoz wa aina hii ni kazi kuleta maendeleo. Singida kamwe haita endelea kwa mwendo huu. Polen walimu japo kujidharilisha wakutaka wenyewe!
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Ni imani yangu kuwa hii posho za kikao haikustahili kulipwa kwa walimu na mtumishi mwingine yeyote wa Serikali kwani kuhudhuria kikao haikuwa ni sehemu ya kazi zao. Nimekuwa nikipendekeza posho za vikao hivyo ifutwe. Mpaka hapo mfumo wa kulipana posho za vikao utakapofutwa, ninaelekeza kwamba posho hizi zote walizopewa hawa walimu zielekezwe katika mfuko wangu wa EMT.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Well Kama anatoa na serikali haitoi hiyo pesa it motivates the teacher's -- The Prime Minister of Italy does the same thing, hsi politicians don't like him but people of Italy loved him because he take from his pocket to better his people...
  In the US the same thing the call it PORK Projects...

  As long as you benefit the Mass and not keep to your belly; More Power as you know we will never ever have a leader like Julias Nyerere anymore ...
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Pesa yoyote anayopewa mtu kama mtu kwa kum-motivate kama unavyosema ni rushwa kama kazi ya hiyo fedha haipo na haijulikani ni malipo ya nini? basi huo ni ushawishi, Mbunge ange wawezesha waalimu kujua kuvua samaki siyo kuwapa samaki, sidhani kama tunachagua wabunge iliwatugawie fedha potelea mbali hizo fedha kama ni safi au chafu, Mbunge ana nafasi pana ya kutetea na kudai haki za wananchni ndani ya Bunge na katika vikao vya Halmashauri na hiyo ndiyo kazi ambayo mbunge anapashwa kuifanya kama MO hafanya hayo yote na hata kama yeye ni msamalia mwema basi aache Ubunge aendelee na usamalia mwema bila Ubunge! yah inawezekana na nadhani afanye hivyo, kila Ijumaa watu wakajipange kwake kupokea chochote aachie wanaoweza kuishika serikali wafanye kazi ya Ubunge.

  Hawa ni wafanyabiashara wachafu ambao wanafaidi kutokana na kulala kwa serikali hivyo mara zote watu kama hao utumika kuuwa nguvu za Umma na Bunge dhidi ya serikali, kitu amabacho hakikubaliki na hakifai hata kidogo, ebu niambie iwapo tukiwa na takribani nusu ya wabunge kama MO, tutakuwa na serikali ya aina gani? na kutakuwa na faida gani kuwa na Bunge!? waalimu hawa shida ya Tsh.50,000.00 mbona hatukumsikia wakati wa malalamiko ya kudai malipo ya waalimu ambayo yalitaka kuperekea mgomo mkubwa wa waalimu Tanzania kwa kudai malimbikizo yao!
  Shida ni uwajibikaji kwa maslahi ya Umma, rushwa ni rushwa tu hata kama inatolewa Italy au Marekani bado ni rushwa.
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Well If you look deeply right now after the failure of Communism there is no political system in this world right now which is fair and you will never ever find another one fair ... we have to change to please our donors and after AZIMIO LA ZANZIBAR we have washed our hands from supporting and protecting our nations; now we gave everything to whoever has Money; well most of our people will end up even not been proud of our nation we loved and cherish during JK Nyerere
   
 11. i411

  i411 JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  sasa wakati umefika zile milioni 12 wabunge wanazolipwa wazifanyie kazi kwa wananchi wao, sio kutudanganya posho yangu ipelekwe kushoto wakati unajua jibu haliwezekani. Kwa miezi sita hizo mishahara ya wabunge ni 72,000,000 tsh, hujaweka posho hapo. Kama wabunge wanamachungu na watu wao nazani zilefeza zinazojilumbikiza katika mabenki yao wanaweza wakazitoa kwa wananchi chapuchapu sio kufuata malumbano na maviongozi wa bunge mpaka kitu kipitishwe ni mwakani kama tunabahati. Angalau maramoja kwa mwaka wafanye kitu cha maana majimboni mwao sio kuilaumu serikali, wabunge wenyewe ndo serikali au wabunge wengine hawalijui hilo.
   
 12. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Waswahili husema mfundishe maskini kuvua samaki lakini sio kumpa samaki wa mlo mmoja sasa mo anapaswa kuwapa ujuzi wa kutengeneza pesa zaidi na sio kuwapa posho za mara moja kwa mwaka/miaka
   
 13. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkumbuke kuwa MO si mwanasiasa by nature, ....................bali mfanyabiashar aliyegeukia na siasana sasa an-play both games, ....................so money must speak louder than himself!!................
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  kisha kwepa ushuru sana wa kuingiza sukari ngoja atoe walau hiyo ahsante!
   
 15. F

  Fresh Air Member

  #15
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It pains . . . Kama walimu hawa wameshindwa kuiona rushwa hii iliyo dhahiri wanachowafundisha watoto ni nini? Kwa nini huyo Mo asitoe hiyo fedha kwa kitu fulani kitakachosaidia the whole of Singida, say kujenga dispensary ama another school? Ama hata ku-supply computers ktk mashule? How cheap are we going to get sisi waTz, hata tunashangililia kwa virushwa vya 50,000?
   
 16. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Hatuhitaji wabunge watakaowagawia wananchi fedha kutoka mifukoni mwao, hiyo ni dhihaka kwa wanaomchagua mbunge ili awape fedha. Tunataka wabunge watakaosimamia vizuri mapato ya taifa ili kila mwananchi apate huduma nzuri anazostahili kwa gharama ya serikali na siyo mbunge binafsi.
  Ni muhimu ieleweke kwamba maendeleo ya wananchi kwa ujumla hayatapatikana kwa kuchagua wabunge matajiri ili wawagawie pesa.
  Tukiacha hali hii iendelee tutarudisha sehemu kubwa ya jamii kwenye utumwa!
   
 17. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wengi wenu muna donge na wivu kwa kuwa hamkupata nyie inawauma sana hongera muheshimiwa Dewji kwa moyo wako wa kizalendo hio si rushwa na umeoneshga ubinadamu zaidi maana naamini hakuna aliewapa nauli ya kuja kwenye huo mkutano,hakuna,wewe ni zaidi ya binaadamu wengi waliokoment humu wana chuki kwa kuwa wawapendao hawana uwezo wa huo na moyo huo hongera sana Muheshimiwa Dewj mungu akuzidishie ulipopunguza akupe zaidi na zaidi inshaallah
   
 18. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Muheshimiwa mooo yaani leo umenifurahisha sana naamini hio ni SADAKA nzuri zaidi na wengi ya walimu naamini watakuombea dua mungu akulinde kwa kila Husda na Fitna unazopigwa maana wanakuchukia kwa vile una moyo wa kibinadamu zaidi safi sana muheshimiwa am proud of you
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani nina uhakika gesti zilijaa siku hiyo ....aaaah walimuuuuuuuuuu msitufanyie hivi bana
   
 20. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Singida ni mojawapo ya mikoa ambayo ipo nyuma sana kimaendeleo!!sasa nashawishika uwepo wao nyuma kumbe ni kwa sababu ya uvivu wa fikra namna hii??milioni arobaini hizo zilitosha kuchimba kisima fasta sasa nyie mmetia mfukoni halafu mnataka nani awachimbie??au watu wa marekani??shame on you wanyaturu na wengineo wa huko!!nyie ndo mnabakigi kulalama eti sijui wachaga wanapendelewa sijui rais ni ****** kumbe hamna akili.takukuru nayo iko wapi lakini??yani hili linchi linaboa kila kukicha.
   
Loading...