Mnyukano wa uchaguzi UVCCM waanza; wasema si dhambi kuutamani urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyukano wa uchaguzi UVCCM waanza; wasema si dhambi kuutamani urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 8, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATANO, AGOSTI 08, 2012 05:50 BAKARI KIMWANGA NA JERRY TEMU, DAR ES SALAAM

  *Wenyewe wasema si dhambi kuutamani urais
  *Shigella atangaza kiama wadanganyifu

  UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema si dhambi kwa wanachama wa CCM kuutamani urais mwaka 2015 na kusisitiza jambo hilo lifanyike wakati ukifika.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martini Shigella, alisema kuanzia sasa umoja huo, utakuwa makini kwa kufanya uchunguzi dhidi ya wanachama wake waliochukua fomu kuwania nafasi mbalimbali ili kubaini makundi ya watu wanaotaka kuvuruga umoja huo, kwa ajili ya mbio za urais.

  Alisema UVCCM, utakuwa makini kupitia fomu za watu walioomba kuteuliwa kuwania nafasi mbalimbali na iwapo itabainika kama kuna watu waliofoji vyeti watachukuliwa hatua kali na kukosa sifa za kuteuliwa.
  “Kuutamani urais hivi sasa, si dhambi kwa mwana CCM, ila tunachoangalia ni wakati gani… ikibainika kuna kundi la watu ambao wanasukumwa na kugombea urais wanataka kutumia uchaguzi huu, tutapambana nao na kuwaengua kwenye kinyang’anyiro,

  “UVCCM, haitakuwa tayari kuona wanaingiza vijana ambao wataingia kwenye jumuiya hii kwa lengo la kutengeneza makundi ya mtandao wa urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  “Baada ya hatua ya kurudisha fomu, tutapitia majina ya watakaoteuliwa baada ya kupitiwa fomu zao na kuna mambo mengi ambayo yatachunguzwa …kwa kila aliyerudisha fomu katika ngazi mbalimbali. Napenda kutamka kuwa ni marufuku wagombea kuanza kampeni hata kwa kujipitisha katika ngazi za wilaya na mikoa kwa lengo la kujitambulisha.

  “UVCCM, hatutapenda kuona waliochukua fomu wanaanza kuchafuana maana hatutaki kuona wagombea wanapakana matope.

  “Na kwa kutumia idara mbalimbali za UVCCM na chama kwa ujumla tutafuatilia mienendo na taratibu za waliomba fomu hizo ili kubaini nani ni nani na lengo lake, ni nini ndani ya umoja wetu. Hatutakuwa tayari kuruhusu watu ambao ni mamluki na wenye lengo la kuivuruga UVCCM tutawabaini mapema,” alisema Shigella.

  Alisema mchakato wa uchaguzi wa ndani ya umoja huo, utazingatia sifa na uwezo wa nafasi mgombea anayewania na si kumbeba mtoto wa kigogo yeyote.

  Akizungumzia idadi ya wana UVCCM waliorejesha fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa , alisema kwa upande wa Tanzania Bara hadi juzi jioni, jumla ya wagombea 60 wamerudisha fomu ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo na kwamba fomu za mikoani hazijaingizwa, wakati kwa upande wa Zanzibar, waliorudisha fomu ni zaidi 51.

  Hata hivyo uchaguzi wa mwaka huu umekuwa wa aina yake huku nafasi ya Uenyekiti wa Taifa, waliomba kuteuliwa ni pamoja na mtoto wa mwana mapinduzi wa Zanzibar, Thabit Jecha Kombo, Sadifa Juma Khamis, Rashid Msaraka, Nadra Khamis, Mwanaamina Haji Faruk, Jamal k. Ali, Mabrouk Mrakib, Asila Ali Suleiman na Lulu Mcham Abdallah.  [h=4][/h]
   
Loading...