MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Kuapishwa kwa Rais Magufuli kuwa Rais wa Tanzania kumehitimisha mnyukano wa zaidi ya miezi miwili wa kutafuta madaraka ya nchi kati ya vyama vya siasa. Mapambano ya kisiasa kwa sasa yamehamia tena ndani ya vyama vya siasa.
Wakati kwa sasa NLD ikitafuta Mwenyekiti wake wa Taifa, CHADEMA ikitafuta Katibu wake Mkuu , CUF ikitafuta Mwenyekiti wake Mkuu, huku Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi wakizidi kulaumiana kuhusu athari na matokeo ya kuingia kwenye UKAWA. Mnyukano rasmi ndani ya CCM kwa sasa ni kutafuta watendaji wa kuunda serikali ya CCM.
Kuanzia sasa tutaanza kuzisikia na kuzisoma habari za kuchafuana/kupakana matope ndani ya CCM ambazo msingi wake ni mnyukano wa nafasi za kisiasa katika serikali ya Rais Magufuli. Kuna wengine wameanza kujipitisha pitisha mbele ya Rais Magufuli ili asizisahau sura zao wakati wa kupanga safu ya uongozi!
Mnyukano utakuwa ni mkali zaidi kwenye nafasi ambazo mpaka sasa haijulikani kwa wananchi nakwa wanasiasa ndani ya CCM ni nani atateuliwa na Rais Magufuli.
Hatutashangaa kukutana na habari zenye mlengo wa mnyukano kati ya wanaCCM kwenye magazeti na mitandao mbali mbali kama ilivyokuwa wakati wa kutafuta mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.
Historia inadokeza chanzo cha kuanza kuyumba kwa serikali ya Rais Kikwete ni mnyukano wa wanaMtandao waliomwingiza Rais Kikwete Ikulu. Mnyukano wa nafasi za Uwaziri na hasa nafasi ya Uwaziri Mkuu kati ya Lowassa na Mzee Sitta ulikuwa ni kichocheo cha kuzorota kwa utendaji wa CCM na Serikali yake. Inasemekana wakati wa kampeni ndani na nje ya CCM, Rais mstaafu, Kikwete alikuwa anawaahidi watu mbali mbali nafasi za uongozi kama watamuunga mkono na akachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania. The rest is history!
Mnyukano kwa sasa ndani ya CCM utakuwa ni nafasi ya Uwaziri Mkuu hasa ikichukuliwa Waziri Mkuu ndiyo mbegu mojawapo inayozaa Baraza la Mawaziri. Waziri Mkuu ndiyo nguzo ya uelekeo wa Serikali katika utendaji wake kama Katiba yetu katika Ibara ya 55(1-2) inavyosema,
Tunaambiwa Rais Magufuli hakuwa na makundi au wapambe katika safari yake ya kuingia Ikulu. Kama ni kweli, ninatumaini itapunguza sana kama siyo kuondoa chanzo cha serikali yake kudhoofika kiutendaji kutokana na makundi ndani ya CCM na Serikali yake. Nilimsikia akisema ndani ya CCM kuna wanafiki.
Mwenyekiti mtarajiwa wa CCM-Taifa, Rais Magufuli ana nafasi kubwa ya kujifunza kutokana na makosa ya Marais wastaafu. Natumaini anafahamu makosa ya Marais waliopita!
Macho na masikio ya wananchi kwa sasa ni kufahamu nani atakuwa Waziri Mkuu ndani ya siku 14 kama Katiba inayotaka. Waziri Mkuu ndiyo gia ya Rais katika utendaji.

55.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(2) Pamoja na Mawaziri waliotanjwa katika ibara ndogo ya (1), Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua Naibu Mawaziri.