Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Rais Kikwete ni mojawapo ya marais bora kutokea katika jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Nasema hivyo nikiwa na reflect hali ilivyokua kutoka kipindi cha Mwinyi, Mkapa na mpaka sasa anamalizia Kikwete.

Ni suala lililo wazi na linaloonekana kua katika kipindi hiki tumeshuhudia maendeleo makubwa tu ambayo yanamgusa mtanzania wa kawaida moja kwa moja. Miundombinu imeboreshwa kwa kiasi kikubwa hasa barabara, viwanja vya ndege na hata reli japo kwa kiasi kidogo. Tumeshuhudia barabara mbali mbali zikijengwa kwa ubora wa hali ya juu including ile ya Dodoma Arusha, Ruaha mbuyuni Iringa, Dar mwanza na nyingine nyingi tu ambazo wewe msomaji unazijua.

Kumekua na comparisons nyingi tu za watu Kumkejeli kwa kushindwa kuwashughulikia vigogo wala rushwa, na kasi ya ukuaji uchumi. Itakumbukwa kua katika kipindi cha Mkapa kulikua na kasi nzuri ya ukuaji wa uchumi lakini uchumi huo ukawa ni wa baadhi ya watu. Mwananchi wa kawaida wa kule mbinga vijijini na Lupa tinga tinga haukumsaidia kwa lolote.

Anayebeza haya abeze tu lakini kimoyomoyo anashuhudia kua

1. Wafanyakazi wa ndani wamekua adimu sana na mishahara yao imepanda kisa ni shule za kata(japo zilipondwa sana
mwanzoni)

2. Wachangiaji wengi na waropokaji humu wamesoma katika shule na vyuo ambavyo vimepatikana ndani ya uongozi wa Kikwete

3. Bodi ya mikopo kwa wanafunzi, sekretarieti ya ajira pamoja na ukuaji mkubwa wa viwanda hapa Dar ni chini ya uongozi wake..

Kuna mambo mengi sana ambayo kwa kweli jamaa amejitahidi ukizingatia kua amekua katika kipindi ambacho serikali inafuatiliwa kwa umakini na watu wake.

Kuna mapungufu ambayo rais kikwete anayo ambayo ni kushindwa kukemea baadhi ya matatizo kama ufisadi na rushwa. Haya ni mapungufu ambayo tunategemea raisi ajaye kwanza atutoe hapa tulipo lakini atufikishe juu zaidi ya hapa.

Mi najua kua kama binadamu wa kawaida anayo mapungufu yake na haya ndio mapungufu makubwa ya rais wetu huyu, simlaumu kwa sababu kila binadamu ana mapungufu na hata wewe msomaji unayo yako kwa mfano inawezekana kuna demu mmoja unamhonga sana na anakufanyia vitimbi lakini bado uko naye na kumuacha unashindwa japo hupendi vitendo vyake. Matatizo mengine ni ya kimfumo zaidi na nadhani katiba ndio ilibidi iwe suluhu japo uongozi wake imeichakachua.

Suala ni kuhakikisha kua raisi ajaye awe na positive side sifa zoote za rais kikwete na negative side sifa ziwe chache...!Any way mi naishia hapa ila Big up Kikwete you stood for what you do bilieve na umeachive so Hongera...

Waropokaji na wasiokupenda watabwabwaja tu ila hata wao wakikalia hiko kiti chako hapo cha kwanza watataka wajaze matumbo yao.Is human nature hakuna malaika humu.
:A S crown-1::A S crown-1::A S crown-1::A S crown-1:

Sasa asingefanya haya ilitarajiwa afanye nn na ndiyo aliyoahidi kuyafanya, kumbuka kila awamu ya uongozi vyanzo mapato vinatofautina na hata idadi ya watu inaongezeka inayopelekea ongezeko la mapato kwa kulipa kodi, tukiwa wakweli maendeleo tuliyonayo hayaendani na rasilimali tulizonazo.
 
Tatizo lake yeye JK ni kwamba huwa haongei sana au hajui kutetea jitihada zake kwa sababu anajua kuwa kila mtu anaona jitihada zake, kumbe baadhi yetu tunawza tukawa hatuoni Universities pia zimefurika, no one qualified missses a placement in one o the universities we have today. Usikute kuna baadhi yake hadi zinaweza kuwa zinakosa wanafunzi wa kudahili!

Kweli kabisaaa mkuu...naunga mkono uloyasema
 
Kwa vile kila mtu na mtizamo wake na wewe uko sawa.
Nionavyo mimi ni kweli kabisa kila binadamu ana mapungufu yani ukamilifu kwa binadamu haiwezekani kwa vile si malaika.
Mtu huagaliwa Stregth zake na pua weakness zake thn anafanyiwa comparison na kuangalia ni upande upi una athari. Mimi sikubariani na wewe tu kwa sababu nionavyo mimi Ben Mkapa alifanya kazi kubwa mno na ni ya ziada,alipewa nchi ikiwa mfilisi kabisa. Ni yeye alieinyanyua nchi hii kutoka kutokopesheka hadi kukopesheka. Ben ndo alikuta madeni hayalipiki toka utawala wa mzee Ali,alilipa madeni,akajenga barabara na kuacha pesa ya kutosha hazina!
Miradi ya barabara ilianzishwa na Ben na JK kaja kukamilisha tu hiyo miradi.
Labda unisaidie mradi mkubwa na wa maendeleo kwa watanzania umeanzishwa na serikali ya JK na sio ule tu wa kukamilisha.
Na nikuambie tu rais ajaye atakuwa na wakati mugumu sana sawa na mzee Ben. Hazina itaachwa shida!
Weakness kwa JK ni kubwa zaidi ya strength,hana msimamo hawezi kuwa na maamuzi yeye kwake yote sawa tu ilimradi asionekane kamkosea mtu! Characteristics hizi ni hatari kwa taasisi kubwa km RAIS!
Ni maoni yangu km ulivyotoa yako!

AChA kujitoa ufaham wapi alilipa deni wakati alibadilishana na wazungu resilimali zetu
 
Kwa uelewa wako uko right. But he deserves an for sure you can't compare him with JK!!!!
JK kajitahidi na kaweka rekodi nzuri sana ya safari.....period!
 
kaua kilimo cha pamba , mahindi .Unapokuwa kiongozi kwa nafasi ya uraisi unatakiwa kuangalia na kushughurikia sector ambayo wananchi wako wengi wanajishughurisha nayo ili kuinua kipato cha unao waongoza. Huwezi kuuwa sector ya kilimo halafu ukashughurika na utarii , madini na mabarabara ukadhani unaboresha maisha ya wananchi. Hivi unafikiri kama mahindi kilo ingekuwa tsh. 1000 maisha ya watu yangekuwaje
 
Ngoja tumpe nchi Slaa, tuone itakavyokuwa na ongezeko la wanywagongo!
 
Back
Top Bottom