Confidencer
Member
- Aug 20, 2013
- 29
- 9
Rais Kikwete ni mojawapo ya marais bora kutokea katika jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Nasema hivyo nikiwa na reflect hali ilivyokua kutoka kipindi cha Mwinyi, Mkapa na mpaka sasa anamalizia Kikwete.
Ni suala lililo wazi na linaloonekana kua katika kipindi hiki tumeshuhudia maendeleo makubwa tu ambayo yanamgusa mtanzania wa kawaida moja kwa moja. Miundombinu imeboreshwa kwa kiasi kikubwa hasa barabara, viwanja vya ndege na hata reli japo kwa kiasi kidogo. Tumeshuhudia barabara mbali mbali zikijengwa kwa ubora wa hali ya juu including ile ya Dodoma Arusha, Ruaha mbuyuni Iringa, Dar mwanza na nyingine nyingi tu ambazo wewe msomaji unazijua.
Kumekua na comparisons nyingi tu za watu Kumkejeli kwa kushindwa kuwashughulikia vigogo wala rushwa, na kasi ya ukuaji uchumi. Itakumbukwa kua katika kipindi cha Mkapa kulikua na kasi nzuri ya ukuaji wa uchumi lakini uchumi huo ukawa ni wa baadhi ya watu. Mwananchi wa kawaida wa kule mbinga vijijini na Lupa tinga tinga haukumsaidia kwa lolote.
Anayebeza haya abeze tu lakini kimoyomoyo anashuhudia kua
1. Wafanyakazi wa ndani wamekua adimu sana na mishahara yao imepanda kisa ni shule za kata(japo zilipondwa sana
mwanzoni)
2. Wachangiaji wengi na waropokaji humu wamesoma katika shule na vyuo ambavyo vimepatikana ndani ya uongozi wa Kikwete
3. Bodi ya mikopo kwa wanafunzi, sekretarieti ya ajira pamoja na ukuaji mkubwa wa viwanda hapa Dar ni chini ya uongozi wake..
Kuna mambo mengi sana ambayo kwa kweli jamaa amejitahidi ukizingatia kua amekua katika kipindi ambacho serikali inafuatiliwa kwa umakini na watu wake.
Kuna mapungufu ambayo rais kikwete anayo ambayo ni kushindwa kukemea baadhi ya matatizo kama ufisadi na rushwa. Haya ni mapungufu ambayo tunategemea raisi ajaye kwanza atutoe hapa tulipo lakini atufikishe juu zaidi ya hapa.
Mi najua kua kama binadamu wa kawaida anayo mapungufu yake na haya ndio mapungufu makubwa ya rais wetu huyu, simlaumu kwa sababu kila binadamu ana mapungufu na hata wewe msomaji unayo yako kwa mfano inawezekana kuna demu mmoja unamhonga sana na anakufanyia vitimbi lakini bado uko naye na kumuacha unashindwa japo hupendi vitendo vyake. Matatizo mengine ni ya kimfumo zaidi na nadhani katiba ndio ilibidi iwe suluhu japo uongozi wake imeichakachua.
Suala ni kuhakikisha kua raisi ajaye awe na positive side sifa zoote za rais kikwete na negative side sifa ziwe chache...!Any way mi naishia hapa ila Big up Kikwete you stood for what you do bilieve na umeachive so Hongera...
Waropokaji na wasiokupenda watabwabwaja tu ila hata wao wakikalia hiko kiti chako hapo cha kwanza watataka wajaze matumbo yao.Is human nature hakuna malaika humu.
:A S crown-1::A S crown-1::A S crown-1::A S crown-1: