Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amekichambua kizazi cha vijana (Gen-Z) kama silaha kuu na yenye nguvu zaidi katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania, akitaja sifa tatu za kipekee zinazowafanya kuwa mstari wa mbele.
Akizungumza leo Januari 17, 2026 na Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 33 ya chama hicho, Mnyika amezitaja nguvu hizo tatu kuwa ni nguvu ya kimwili na nishati, nguvu ya wingi na nguvu ya ubunifu na udhubutu.
Akifafanua nguvu hizo, Mnyika ameeleza kuwa vijana wana uwezo mkubwa wa kuhimili mapambano ya nyanjani ukilinganisha na makundi mengine ya rika. Akirejea takwimu za demografia, amebainisha kuwa vijana ni asilimia 65 ya nguvukazi na ndilo kundi kubwa zaidi la wapiga kura nchini na barani Afrika.
Amekielezea kizazi cha sasa (Gen-Z) kama kundi lenye uwezo wa kipekee wa kukumbatia teknolojia na mitandao ya kijamii, ambayo imekuwa mtaji mkubwa wa kisiasa wakati vyombo vya habari vya kawaida vikikabiliwa na udhibiti.