NyaniMzee
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 396
- 727
Mbunge wangu Mnyika. Kuna siku baada ya uchaguzi nilimsikia mpiga kura mmoja akisema tumempa Mnyika kura kwa vile hatuwataki CCM lakini hajatusaidia lolote. Mimi sikupenda Ile kauli kwa kuwa najua nimeteseka kiasi gani na hii CCM. Maji shida, usafiri shida, umeme shida, nk. Lakini baada ya uchaguzi nikatafakari Ile kauli ya mpiga kura wako nikagundua alikuwa sahihi. Mnyika jimbo la Kibamba likipata mtatuzi wa matatizo we utabaki historia kwa hoja binafsi bungeni wakati jimboni mateso tupu. Kila la kheri 2020 Mbunge wanguJ.J Mnyika. Endelea kuchekea miradi ya wauza maji wananunua dawasco lita 5000 kwa shs 1500/= wanatuuzia shs 15000/= . Tuko busy na hoja binafsi.