Mnyika kukata rufaa hukumu ya Spika

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
237


BAADA ya kubainika kwamba tuhuma zilizotolewa na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini dhidi ya baadhi ya wabunge kuwa walipokea rushwa hazikuthibiti na viongozi hao kukemewa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika amesema hajaridhika na uamuzi wa Spika Anne Makinda kuhusu uongozi wa wizara hiyo.

Kutokana na kutoridhika huko, sasa ameamua kukata rufaa ili anachokiona kinafaa kuchukuliwa dhidi ya viongozi hao kichukuliwe.

Mnyika jana alilazimika kutoa taarifa yake nje ya Bunge baada ya mkutano wa Bunge kuahirishwa juzi na yeye kukosa fursa ya kusema jambo hilo bungeni.

Mbunge huyo alisema katika taarifa yake kwamba anakusudia kukata rufaa, dhidi ya uamuzi wa Spika kwa madai kuwa maudhui yake hayazingatii Katiba ya nchi, sheria za nchi, kanuni za kudunmu za Bunge, uamuzi wa awali wa maspika wa Bunge na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu kama wa Bunge la Tanzania.

"Hata hivyo, kwa kuzingatia kuwa rufaa huchukua muda kusikilizwa, nilitaka niombe mwongozo wake kabla ya Mkutano wa Bunge kuahirishwa, kwa kuwa katika uamuzi wake hakueleza hatma ya Kamati ya Nishati na Madini ilivyovunjwa. "Hivyo Spika anapaswa bado kueleza kwa umma iwapo Kamati hiyo inarejeshwa au inaundwa nyingine au kuelekeza kamati nyingine ya kudumu ya Bunge inayopaswa kuisimamia Serikali wakati huu ambao nchi inakabiliwa na matatizo mengi kwenye sekta za nishati na madini yenye athari kwa maisha ya wananchi," alisema Mnyika.

Alisema katika uamuzi wake, Spika alieleza kwamba Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliackim Maswi walitoa maelezo yasiyokuwa na ukweli hivyo uwepo wa Kamati ya Bunge kwa ajili ya kuisimamia Wizara hiyo kwa niaba ya Bunge ni suala linalohitaji uamuzi wa haraka.

Alisistiza kusudio lake la rufaa ili taarifa kamili ya Kamati Ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iwasilishwe kwa ukamilifu kwenye kamati husika ya kudumu ya Bunge na hatimaye taarifa kamili kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni ili ‘mbivu na mbovu' zijulikane na masuala yanayohitaji kufanyiwa uchunguzi wa ziada na vyombo vingine vya nje ya Bunge yaendelee kwa hatua zaidi.

Aidha, alisema atakata rufaa kwa kuwa kiwango cha ‘adhabu' kilichotolewa kwenye uamuzi wa Spika hakilingani na ‘makosa' ambayo yameelezwa kuwa na uzito wenye kuathiri "kwa kiasi kikubwa hadhi ya Bunge kama taasisi na heshima ya wabunge waliohusishwa".

"Spika amefanya uamuzi wake chini ya Kanuni ya 5(1) na 72 (1) lakini hakuzingatia kuwa kanuni ya 72 (3) inaeleza kuwa iwapo mbunge ameshindwa kuthibitisha ukweli Spika amepewa fursa ya kumsimamisha mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vitano," alisema.

Aliongeza kuwa atakata rufaa, kwa kuwa waliodaiwa kutoa tuhuma bila ushahidi, walipaswa kujieleza kuhusu tuhuma hizo kabla ya kuhukumiwa kwa misingi ya kanuni za haki ya asili zilizopo pia katika Katiba ya Nchi na kwa kuzingatia matakwa ya kanuni za kudumu za Bunge.

Pia alisema atakata rufaa kwa kile alichokieleza kuwa ni adhabu aliyopewa Maswi kutolingana na ukubwa wa makosa anayodaiwa kufanya.

"Iikiwa ni kweli amevunja haki za Bunge kwa kuzusha tuhuma za uongo dhidi ya wabunge kwa ajili ya kujihami dhidi ya baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliokuwa wanahoji kuhusu utendaji wa wizara yake. "Kwa kosa hilo ikiwa maelezo ya Spika kuhusu matokeo ya uchunguzi wa Kamati ni sahihi anapaswa kufunguliwa mashtaka kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge na kupewa adhabu ya zaidi ya onyo ikiwamo hata faini au kifungo au walau kutakiwa kuwajibika," alisema Mnyika.

Waziri Muhongo na Katibu Mkuu Maswi walishasema hawana lolote la kuzungumza juu ya suala hilo na kuomba waachiwe wananchi waamue wenyewe na wao wanasonga mbele kutumikia wananchi kuondokana na kero zinazowakabili.


SOURCE: Habari leo
 
binafsi huwa najiuliza maswali mingi, hivi ONYO KALI ni adhabu ya aina gani, ie hivi hii ni adhabu pia au maana sielewi adhabu walopewa
 
Je Mhe. Mnyika hiyo rufaa yako itatumalizia wana Ubungo tatizo la Maji Au la. Ohhh usitulaumu 2015 wewe kalia ya kujitafutia umaarufu wakati sisi wapiga kura wako tuna kero kibao na huzishughulikii. Rufaa hizo 2015 zitakupigia kura.
 
Je Mhe. Mnyika hiyo rufaa yako itatumalizia wana Ubungo tatizo la Maji Au la. Ohhh usitulaumu 2015 wewe kalia ya kujitafutia umaarufu wakati sisi wapiga kura wako tuna kero kibao na huzishughulikii. Rufaa hizo 2015 zitakupigia kura.


Ndugu yangu, mbona unatutafutia Ban wenzio! Kwa nini huoni kuwa mbunge awapo bungeni anawajibika kuwa na mtazamo wa kitaifa zaidi ikiwa ni pamoja na jimbo lake kuliko kufikiria na kufanya kazi katika kipimo cha kibiriti?
 
Je Mhe. Mnyika hiyo rufaa yako itatumalizia wana Ubungo tatizo la Maji Au la. Ohhh usitulaumu 2015 wewe kalia ya kujitafutia umaarufu wakati sisi wapiga kura wako tuna kero kibao na huzishughulikii. Rufaa hizo 2015 zitakupigia kura.

Mkuu hebu kuwa mpole kidogo!
Wewe hapo unalipa kodi kibao. Je,kodi hizo unamlipa Mnyika? Wewe unayekamuliwa kodi kila upande umefanya juhudi gani kumbana yule unayemlipa kodi awajibike kukupatia huduma hiyo muhimu ya maji? Mbunge hana fedha za kukuletea huduma hiyo na anachoweza kufanya ni kumbana huyo mtoza kodi awajibike! Na ili Mbunge afanikiwe ktk hilo anahitaji support ya hasira ya wanachi wake waliokosa huduma muhimu! Mwonyeshe JK + Serikali yake kuwa una hasira kubwa kutokana na kero ya maji usipoona inapatiwa ufumbuzi mapema! Wananchi mkibaki kumng'ang'ania mbunge na Serikali nayo inazidi kubana ili CCM iwe na Turufu 2015 kwamba Mbunge CDM kashindwa!! Tafakari!!!
 
Ndugu yangu, mbona unatutafutia Ban wenzio! Kwa nini huoni kuwa mbunge awapo bungeni anawajibika kuwa na mtazamo wa kitaifa zaidi ikiwa ni pamoja na jimbo lake kuliko kufikiria na kufanya kazi katika kipimo cha kibiriti?

Yaani Jimbo lake ndo kibiriti sisi wapiga kura wake ndo njiti. Haya 2015 utampigia wewe
 
Kweli kashindwa kaona ajikite Kwenye kujitafutia umaarufu tu. sawa.
 

Mimi naona wewe unaweza kufanya vizuri kuliko unayemtetea. 2015 jitokeze basi.
 
Yaani Jimbo lake ndo kibiriti sisi wapiga kura wake ndo njiti. Haya 2015 utampigia wewe
nafikiri mpigie utakayemtaka,hata chama cha dovutwa kipigie,lakini ujue wajibu wa mbunge si kwa jimbo lake tu, hata kwa taifa pia! Nenda kwenye katiba!
 
Mnyika kana kwanza ule ushahidi wako uliotoa kwenye hiyo kamati ya Ngwilizi then twende sawa!!!!otherwise ni walewale.yaani mlivyokuwa mnaongea kwa mbwembwe vile alafu........yaani hadi inakera.kiongozi makini haongozi kwa udaku....
 
Hupajui dawasko wewe au unataka aje akuletee maji na lori jishughulishe acha izmišlja ovyo....idiot
Je Mhe. Mnyika hiyo rufaa yako itatumalizia wana Ubungo tatizo la Maji Au la. Ohhh usitulaumu 2015 wewe kalia ya kujitafutia umaarufu wakati sisi wapiga kura wako tuna kero kibao na huzishughulikii. Rufaa hizo 2015 zitakupigia kura.
 
Yaani Jimbo lake ndo kibiriti sisi wapiga kura wake ndo njiti. Haya 2015 utampigia wewe

Kwa Ujinga wenu wa kutokuangalia mbali mtabaki hivyo hivyo, jimbo la Ubungo limejaa wasomi, waelewa wa mambo, watu wastaarabu, vi kura vyenu vichache vya wajinga wajinga wala havina mshiko kaeni navyo
 

:crazy:ikiwa upeo wetu wananchi utaishia kuona matatizo ya majimbo yetu bila kuzingatia utaratibu wa kuyatatua,ni ukweli usiopingika kuwa CCM itatumia mwanya huo kuonesha kuwa tumeshindwa.
 
“Taarifa kamili iwasilishwe na kujadiliwa bungeni ili ‘mbivu na mbichi’ zijulikane na masuala yanayohitaji kufanyiwa uchunguzi wa ziada na vyombo vingine vya nje ya Bunge yaendelee kwa hatua zaidi badala ya uamuzi huu wa funika kombe,WAZIRI Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika amesema anakusudia kukata rufaa akitaka taarifa kamili juu ya tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge, iwasilishwe bungeni kwa sababu Spika Anne Makinda amekiuka taratibu katika uamuzi wake.

Mbali na hilo, atakata rufaa kupinga kiwango cha adhabu kilichotolewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi kwa maelezo ni kidogo na inalishushia heshima Bunge.

Hatua hiyo inatokana na Spika Makinda kutoa uamuzi wa ripoti ya Ngwilizi bungeni juzi huku akiwasafisha wabunge waliotuhumiwa kwa rushwa na wakati huo akiwakaanga Profesa Muhongo na Katibu wake, Maswi.

Spika Makinda alisema tuhuma zilizotolewa dhidi ya wabunge hao zimethibitika kuwa ni za uongo.

Alisema kamati ndogo ya Bunge ya Haki, Kinga , Madaraka ya Bunge ambayo iliongozwa na Mbunge wa Malalo, (CCM), Hassan Ngwilizi ilifanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma hizo na kugundua kuwa tuhuma hizo zilikuwa hazina uthibitisho.

Taarifa kwa umma aliyoitoa Mnyika jana ilisema Spika amefikia uamuzi wa moja kwa moja wa kutoa adhabu ya ‘onyo kali’ kinyume na masharti ya kanuni ya 5 (1).

“Taarifa kamili iwasilishwe na kujadiliwa bungeni ili ‘mbivu na mbichi’ zijulikane na masuala yanayohitaji kufanyiwa uchunguzi wa ziada na vyombo vingine vya nje ya Bunge yaendelee kwa hatua zaidi badala ya uamuzi huu wa funika kombe,” alisema Mnyika.

“Kuna masuala ya ziada ambayo binafsi niliyaeleza mbele ya kamati ndogo chini ya kiapo ambayo sitakiwi kuyaeleza nje ya Bunge kwa mujibu wa kanuni na sheria… Hata hivyo taarifa kamili ikiingia bungeni kutakuwa na uhuru wa majadiliano kwa mujibu wa Ibara ya 100 ya Katiba ya Nchi,” alisema.

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo alisema Spika alifanya uamuzi chini ya Kanuni ya 5(1) na 72 (1) lakini hakuzingatia kanuni ya 72 (3) ambayo inaeleza iwapo mbunge ameshindwa kuthibitisha ukweli Spika ana mamlaka ya kumsimamisha mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vitano.

“Kwa kuzingatia rufaa huchukua muda kusikilizwa nilitaka niombe mwongozo wa Spika kabla ya Mkutano wa Bunge kuahirishwa kwa kuwa katika uamuzi wake hakueleza hatima ya Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa,” alisema Mnyika.

Aliongeza: “Spika anapaswa bado kuueleza umma iwapo kamati hiyo inarejeshwa au inaundwa kamati nyingine."

Alisema ikiwa maelezo ya Spika kuhusu matokeo ya uchunguzi wa kamati ni sahihi Maswi anapaswa kufunguliwa mashtaka mahakamani.” alisema Mnyika.
 
Go Mnyika.Unawajibika kitaifa na kijimbo.Kiapo cha katiba kinakufunga katika mipaka ya katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…