Mnyika kuendelea na hoja yake Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika kuendelea na hoja yake Bungeni

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,346
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Mnyika kuendelea na hoja yake Sunday, 09 January 2011 20:52

  Claud Mshana
  MBUNGE wa Ubungo kupitia Chadema, John Mnyika, amesema ataendelea na mpango wake wa kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu Katiba, licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko kuwa, ataunda tume itakayoshughulikia mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya.

  Kwa mujibu wa Mnyika, amefikia uamuzi huo baada ya kuwasiliana na baadhi ya wataalam wa masuala ya Katiba, viongozi wa asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini, viongozi wa chama chake na wapiga kura wake.

  Katika taarifa aliyotuma kwa vyombo vya habari jana, Mnyika anasema serikali ya Rais Kikwete imeshindwa kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu utakaotumika, hivyo anaamini kuwa hakutakuwa na mpango wa kuhusisha umma au bunge katika mchakato huo.

  Mbunge huyo alifafanua kuwa kauli ya Rais Kikwete aliyotoa mbele ya mabalozi mwishoni mwa wiki iliyopita, inadhihirisha kutokuwa na dhamira ya kuandika katiba mpya inayohusisha umma.
  Badala yake, kuendeleza hodhi ya serikali ambayo kwa mujibu wa Mnyika inaweza kusababisha mapitio yenye kasoro zile zile zinazolalamikiwa.

  “Baada ya kauli niliyotoa ya kutaka ufafanuzi na matamko yaliyotolewa na wadau mbalimbali ya kueleza kasoro za hatua ya Rais Kikwete ya kutaka moja kwa moja kuunda tume, nilitarajia kwamba kauli yake ya kwanza kabisa ya mwaka huu, angetumia fursa hiyo kufafanua suala husika ikiwamo kueleza kusudio la kupeleka mapendekezo ya mchakato bungeni,” inasema sehemu ya taarifa yake na kuongeza:

  “Hii inadhihirisha kwamba Rais Kikwete anataja katiba mpya kwa maneno tu, lakini haonyeshi kwa vitendo kuwezesha mchakato husika kwa kushirikisha umma kwa ukamilifu.”

  Kufuatia hali hiyo, Mnyika alisema anaendelea kukamilisha taratibu za kuwasilisha hoja binafsi kwenye bunge la Februari kuhusu mchakato wa katiba mpya.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,346
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Mnyika................you are a true servant of the people..........................of Tanzania...............
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi na kale kamama kasije ikataa isizungumziwe kisa, eti kiwete kashaanzisha mchakato!
   
 4. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  haina mpango tena JJ achana ha hiyo kitu
   
 5. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mhe Mnyika endelea, usirudi nyuma- ila kumbuka bila nguvu ya sheria kulinda mchakato nina wasiwasi na mbinu za mafisadi; walao iwepo nguvu ya sheria hata kama watachakachua kama sheria ya uchaguzi wa 2010; lakini kama ipo tutakuwa na pa kusimamia-bila hiyo sheria ya kuhalalisha na kulinda mchakato tutaishia kwenye vurugu kubwa za kisiasa-mafisasdi wamesema katiba mpya ni kupindua serikali iliyoko madarakani- tutegemee nini basi???????????(yaani kuwapindua); hizi ni moja ya sababu ya kudai pesa za Dowans!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...