Mnyika Bunge linakwisha, njoo uone ya jimboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika Bunge linakwisha, njoo uone ya jimboni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiswigo, Aug 10, 2012.

 1. K

  Kiswigo Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  John John Mnyika umeonyesha umahiri mkubwa katika kuchangia mijadala na kutoa hoja binafsi bungeni, na hasa katika kikao hiki kinachokaribia kwisha. Sikushangaa kwamba michango hiyo na hoja hizo hazikuwalenga watu wako wa Ubungo maana katika kipindi chote cha kuelekea katika mkutano huu, hukuwahi kuzunguka jimboni na kufanya mikutano na wapiga kura wako ili kubaini kero na matatizo yao na kuona namna bora ya kuyawasilisha. Muda mwingi ulikuwa na operesheni sangara, ukikosoa hali mbaya ya uongozi na uduni wa maisha ya watanzania wa majimbo mengine.

  Kwa vile sasa unarudi Dar es Salaam (nikiamini hupitilizi kwenda Kinondoni - CDM Makao Makuu), njoo uone yale yale uliyoyatumia kukufikisha hapo ulipo yakiwa hayajaguswa. Kero zenyewe naweza kukumbusha kwamba:

  Ukosefu wa maji japo wizara ya maji na bomba kubwa linapita ubungo;
  Makorongo kwenye barabara zetu zinazoingia ndani kutoka barabara kuu ya Morogoro;
  Ukosefu wa vituo vya kutosha vya afya, polisi;
  Uhaba wa vyumba vya madarasa katika mashule yetu;
  Ukosefu wa umeme katika maeneo ya pembezoni kama vile mbezi msumi, makabe na mbopo n.k.

  Usidanganywe na watu watakaokutaka uende kwenye ziara M4C ukajikuta unang'olewa, 2015 ni keshokutwa tu!

  Tafakari, chukua hatua.
   
 2. b

  banyimwa Senior Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huku Bonyokwa tuna hasira naye sana. Hata daladala zimeamua kuongeza nauli zikidai barabara ni mbovu na ukweli ni kwamba huku kuna makorongo na toka achaguliwe hajawahi kuonekana wala kufanya lolote. Hata diwani wake hajulikani alipo.
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndo mkome kuchagua watu kwa uwezo wa kuupepeta mdomo majukwaani. Jamaa kumbe ni hopeless hivyo?
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Waambie wana Bonyokwa wasihofu katiba mpya na muongozo wa spika utaleta barabara huko.
   
 5. T

  Tiote Senior Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika 2015 tutashuhudia anguko la wabunge wengi waliochaguliwa kwa mtindo huu na mabo leo wanajifanya vinara wa kupigania haki za nchi huku wakisahau kwamba nchi inaanzia majimboni mwao.
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Join Date : 9th August 2012
  Posts : 9

  Rep Power : 302
  Likes Received: 0

  Likes Given: 0


  Naona umeingia na kuanza na kamanda Mnyika, nadhani jaribu kujifunza namna ya kuandika na kupost hoja hapa JF...
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Kumbeeeeeee!

   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Maji maji maji maji!!!!! Kimara hakuna!!!!!!!!!!

  Naomba mwongozo wa Mnyika!
   
 9. B

  Ba'mdgo JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona barabara nyingi za kuingia ndani zilibigwa rafu karibu maeneo mengi ya ubungo na hata barabara ya makabe pia kwani mara nyingi napita. mimi nibo ubungo makuburi wakati barabara zinajengwa baadhi ya watu nakumbuka walikuwa wanawatania wana CCM kuwa wameishi maeneo hayo zaidi ya miaka 20 wajawai kutengenezewa barabara namna hiyo. kuhusu maji alisimamia viosk vinavyouza maji bei iwe sh 20/= pamoja na kulalamikia dawasco mara kwa mara anasikika kwa hilo na kama mnakumbuka alishaandamana na wapiga kura wake mpaka dawasco ubungo kwa ajili ya maji:

  Kabla ya kulaumu kwanza lazima ujuwe majukumu ya mbunge na mbunge atoi pesa zake mfukoni iliajenge barabara au kutatua kero husika bali ni kuyajuwa matatizo na kuyaoji kwa serekali kuu au serikali za mitaa. madiwani wanalalamika halimashauri kutotoa hela wanazopitisha kwa ajili ya maendeleo
   
 10. w

  watenda Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huku ni kutishana na haikubaliki. Ulitaka awe amechangia thread ngapi ndo apate hadhi ya kumjadili Mnyika au wateule wachache ambao wewe unawaona wana sifa ya kitukufu? Hili ni jukwaa huru na watu wanachangia humu bila woga wala vitisho. Mkuu Kiswigo karibu na hongera kwa kuanza kwa kishindo na usitishwe vichwa uchwara ambavyo havijadili hoja bali watu na matukio. Kama mbwai mbwai tu bwana!
   
 11. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Walalamishi wengi mara nyingi ni wale ambao hawa kumpigia kura.hata wafanyiwe nini hawataacha kulalamika.
   
 12. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, kabla ya Mnyika kuna wabunge wangapi wa Chama cha Magamba waliowahi kuongoza Ubungo? Na ni wangapi wa CDM? Na hao Magamba wameongoza Ubungo kwa miaka mingapi? Na Mnyika kaongoza muda gani? Je, matatizo hayo yameibuka wakati wa Mnyika tu? Kama yalikuwepo tangu huko nyuma (na ni ukweli ndio maana hayajatatuliwa hadi sasa) nani tapeli, wabunge wa Mabwepande au Mnyika? Hivi kwa ku-post thread hii, unatumia kiungo gani cha mwili wako ktk kufikiri? Ni hayo tu Mheshimiwa, sasa naomba unijibu. Ahsante sana!
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Acha kulea na kuupaka mafuta uzembe. Mbunge yeyote anpoingia madarakani anakuwa na platform yake ya uchaguzi na huyu bwana nilipokuwa nasikiliza na kusoma habari zake za kampeni, yale yaliyoorodheshwa na mwanzilishi wa thread hii ndo zilikuwa platform zake. Alipoahidi alipaswa kujua kwamba kuna financial or resource implications na alitakiwa kujua namna ya kuzipata. Katika hili hatutarajii afanye kama traffic anayemwambia mke wake abandike sufuria ya ugali yeye ankwenda barabarani kupiga bao ndo arudi na mboga.

  Wala suala hapa siyo kupigania vioski viuze maji 20/= bila kujua wenye vioski wameyatoa wapi na kwa gharama zipi. Wala zile juvenile tricks za kufanya maandamano kwenda Dawasco (ambazo ni mbinu za kiuanaharakati na siyo za kiongozi) haziwezi kutatua kero. Mbunge anapaswa kuwa na mikono miwili ya kuhemea. Mmoja bungeni na serikalini, na mwingine kwa connections zake na washirika wa maendeleo na tumeona hili kule Karatu ambako shida ya maji ilikuwa kubwa lakini Dr (Phd) alitaguta wafadhili wakafadhili mradi wa maji na mambo yakawa poa.

  Kuhusu barabara, mie ni shahidi. Last week nilikwenda kwa jamaa yangu maeneo ya Kimara Vyumba vinane. Nilitamani niache gari barabarani kusudi nichukue taxi kwa hofu ya kutoboa sample na hali hii ni kila mahali ndani ya maeneo ya pembezoni ya jimbo, ambako alichaguoiwa kwa kura nyingi kwa matumaini kwamba ahadi zake zingebadilisha mambo. Wanajuta.

  Kuhusu kumchagua au kutomchagua kwenye uchaguzi uliopita, hiyo ni hoja kengeza. Mbunge hatakiwi kubagua katika kuhudumia na wala kutompigia kura hakumnyimi mwananchi haki ya maendeleo. Kura ji mchakato wa kidemokrasia na inawezekana yule alimkataa alikuwa na mashaka na uwezo wake. Mnyika awe na busara na kupuuza hoja za kishabiki zinazompamba ili akidhi matumaini ya wananchi wake waliosubiri miaka mitano ili wampe kura, baada ya kushindwa 2005. Hizi siasa za kitaifa na kulia lia hata sisi kule jimbo la Kawe tunapata shida hiyo hiyo.
   
 14. K

  Kiswigo Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi mania ni mbaya sana. Wewe badala ya kutuambia Mnyika kafanya nini unarejea kwenye historia. Tuliikataa CCM baada ya kuridhika kwamba hawakufanya vizuri wakati wa uongozi wao na ni baada ya kushawishiwa na Mnyika kutoka na sera na ahadi zake. Na kwa vile ahadi za mgombea kwa mpiga kura ni kama makubaliano kati ya pande mbili, tunachotaka afanye ni kutekeleza upande wake wa ahadi kwani sisi tumetekeleza la kwetu kwa kumpatia madaraka. Kinachoskitisha ni kwamba hata kule kuonekana akahamasisha wananchi kujitolea na kuchangia maendeleo hakuna.

  Sasa kama una-resort kwenye matusi badala ya kujikita katika hoja, humsaidii kipenzi chako Mnyika maana atakapotuhitaji hatatuona na wewe hutamuokoa. Kilio hiki ni cha wana ubungo kwa sababu kero zilizopo hazichagui itikadi, in fact, wengi wa wanaolalamika ni wafuasi wake ambao walimnadi na sasa wanaona aibu kupita kwa watu waliokuwa wamewajengea matumaini makubwa. Kujibu swali lako, mimi nafikiri kwa kutumia kichwa na wewe mwenzangu unatumia moyo, ndo maana haya mapungufu ya Mnyika kwako wewe ni chuki na uzandiki. Bora Keenja alijenga madaraja na barabara za msumi, makabe na bonyokwa zilikuwa zinapitika.
   
 15. p

  pembe JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mleta hoja hajakosea katoa maoni/mawazo yake na sisi ndio tunayafanyia kazi. Wanachi wa jimbo la ubungo niwaambieni kwamba maendeleo yanaletwa na wanchi wenyewe ktk sehemu husika mbunge kama kiongozi anashauri, anafuatilia, an kuwajulisha mara kwa mara kinachoendelea.
  Sisi huku Mbezi Beach tuliona barabara zimeharibika na masika ndio yalikuwa yanakaribia. Tukahamasishana tukapata hela ya kutosha mafuta ya greda na operator wake. Mtendaji wa mtaa akaenda manispaa akalipa tukapata greda likasawazisha zile barax2 tulizoziainisha. Sasa ndio tunapambana na tatizo la majambazi! Inawezekana..play your part.
   
 16. m

  mudavadi Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenzenu akimaliza bunge anakwenda kuungana na Kamanda Lema kufanya shopping huko nje akidai anafungua matawi wakati hata katavi hajawahi kutembelea. Hivi unapoteza muda nje kwa diaspora ipi? Kwanza wengi ni wahamiaji haramu na ambao hawana voting power, achilia mbali kipato cha kuchangia chama. Ndugu zao waliowaacha huku nyuma hata mitumba wanashindwa kuwatumia.

  Mnyika ndugu yangu kumbuka ulikotoka.
   
 17. m

  makelemo JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pia kimara Baruti na Msewe hakuna maji na hakuna maelezo ya kutosha, tafadhali mheshimiwa, tunapima mtu kwa vitendo na si kwa maneno.
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwetu mbopo ni kitu cha ajabu sana nikikitamka hapa nakula ban....

  After all wewe hukumpigia kura huna haja ya kulalamika.
   
 19. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Watu bana...Miaka 49 hawajafanya lolote leo tunataka watu ambao hawana hata dola kufanya miujiza.
   
 20. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwani mlikubaliana naye kuwa muda wa kutekeleza ahadi zake mwisho lini? Mi nijuavyo ni 2015, sasa kwanini unadhani kashindwa ilhali hata nusu ya kipindi chake haijafika? Haraka ya nini? Kulalamika kwako si hoja, maana hata USA wapo maskini hadi leo na wakati taifa hilo ndilo tajiri zaidi duniani! Kuwa mvumilivu, na hasa ukijua kuwa mifumo mingi ya kisiasa kwa nchi kama yetu si ya kidemokrasia kihivyo. Jimbo la Mpinzani serikali inalipuuza utadhani inapingana na wananchi wake. Ila, kumbuka hata Rome haikujengwa siku moja.
   
Loading...