Mnyika amtwanga barua waziri wa elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika amtwanga barua waziri wa elimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lua, Dec 14, 2011.

 1. L

  Lua JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuhusu migogoro ya UDSM, UDOM na MUHAS

  Kwa mujibu wa ibara ya 63 (2) na (3) mamlaka ya bunge ni kutunga sheria na kusimamia serikali. Kutokana na mamlaka hayo kazi za mbunge ni kuwakilisha wananchi, kushiriki katika kutunga sheria pamoja na kuisimamia serikali na viongozi wake.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Kawambwa aliahidi bungeni kwenye mkutano wa nne kwamba serikali imepata mkakati wa kumaliza migogoro na matatizo katika vyuo vikuu nchini na kwamba hatua za haraka zingechukuliwa kama sehemu ya utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2012/12.

  Hata hivyo, badala ya migomo na migogoro kumalizika inaelekea kuongezeka. Katika siku za karibuni pamekuwepo na maandamano ya mara kwa mara katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS). Aidha, hali ya mambo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) haijatulia mpaka sasa, huku wanafunzi 567 wakiwa bado wamesimamishwa. Katika kipindi cha mwezi mmoja imekuwa ikijirudia rudia hali ya mvutano baina ya wanafunzi na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

  Hali katika vyuo vikuu hivi na vingine haiendani na ahadi ambayo Waziri Kawambwa alizitoa bungeni na kwa umma miezi kadhaa iliyopita. Leo nimeingia ofisini jimboni na kukatizwa kazi za kufuatilia masuala mengine ya wananchi na habari za mgomo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam Mlimani.

  Pamoja na kuwa bado sijapokea taarifa rasmi ya toka kwa Utawala wa Chuo au kwa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO); wakati nikifuatilia taarifa zaidi nimeona nichukue hatua za kiutendaji za kuwasiliana na wizara yenye dhamana ili waweze kuingilia kati kama sehemu ya kutimiza ahadi iliyotolewa bungeni.

  Katika kukabiliana migomo na migogoro katika elimu ya juu serikali imekuwa ikichukua hatua dhidi ya matokeo badala ya kushughulikia vyanzo vya matatizo hivyo natarajia wakati huu Waziri husika atajielekeza katika madai ya msingi ya wanafunzi na wahadhiri.

  Serikali izingatie kwamba chimbuko la mgogoro wa MUHAS ni tofauti katika utekelezaji wa agizo la serikali la tarehe 12 Juni 2009 (GN. 178) ambayo limefanya mabadiliko ya makubwa kwenye uendeshaji wa serikali za wanafunzi katika vyuo vikuu na hivyo kuanzisha mivutano baina ya wanafunzi na utawala katika chuo hicho na vyuo vingine nchini.

  Serikali irejee kwamba chanzo cha migomo UDOM ni madai ya wanafunzi kuhusu mafunzo kwa vitendo na malalamiko mengine kutoka kwa wahadhiri. Toka wanafunzi wasimamishwe mwezi Juni 2011 mpaka sasa ikiwa imepita karibu miezi sita wanafunzi 567 bado wamesimamishwa masomo huku zoezi la kumhoji mmoja mmoja likisuasua na kutarajiwa likiwa limepangwa kumalizika mwishoni mwa Mwezi Machi mwaka 2011. Serikali inaweza kabisa kwa kushirikiana na chuo kuharakisha taratibu za kinidhamu wakati huo huo kushughulikia madai ya msingi ya wanafunzi ili kuepusha mazingira ya mivutano kudumu kwa muda mrefu.

  Serikali itambue kwamba chanzo cha migomo ya hivi karibuni UDSM ni kugeuzwa kwa taratibu za utoaji mikopo na hatimaye kuchelewa kwa malipo ya wanafunzi na wengine kupata pungufu au kukosa kabisa. Katika mazingira hayo ni muhimu kwa Waziri Kawambwa kuweka wazi kwa umma ripoti ya Tume ya Rais iliyoundwa tarehe 14 Februari 2011 na kukabidhi taarifa yake tarehe 29 Aprili yenye mapendekezo ya jinsi ya kuboresha utaratibu wa sasa wa ugharamiaji, utoaji na urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu.
  Kuwekwa wazi kwa taarifa hii kutawezesha wawakilishi wa wananchi, wanafunzi, wazazi, vyuo vikuu na wadau wengine wote kuunganisha nguvu katika kushughulikia matatizo yanayoendelea kujitokeza katika elimu ya juu hivi sasa.

  Ikumbukwe kwamba Rais Jakaya Kikwete aliahidi mwaka 2007 kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wanafunzi wa elimu juu nchini ili kupunguza migomo na migogoro. Katika Mkutano wake na wanafunzi wa vyuo vikuu mwezi Februari 2007 alikwenda mbali zaidi kwa kuwaeleza kwamba hakuna mtoto wa maskini atayeshindwa kuendelea na masomo kutokana na masharti ya mikopo.

  Miaka mitano imepita toka ahadi hizo zitolewe migomo katika vyuo vikuu inaendelea na pia wapo watoto wa walalahoi ambao wamefaulu kidato cha sita lakini wemeshindwa kuendelea na masomo kutokana na kukosa mikopo; hivyo Waziri asipochukua hatua za haraka itadhihirika kwamba ahadi za serikali zimekuwa za ‘kiini macho'
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Yaani kwa wale wa UDOM nimesikia hakuna dalili ya kurudi...na kama wakirudi wanakuwa wamekaa nyumbani karibu mwaka mmoja...kwanini ujinga wa uongozi wa vyuo kama UDOM uumize watoto wa wakulima? Nina ndugu yangu karudi nyumbani shinyanga na sasa anafanya kazi ya kuendesha pikipiki kama bodaboda baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu.....tatizo la kuwa na madaraka makubwa ya raisi ndio yanazaa haya....VC na Ma-DV ni wateule wake,tena anawachagua kulingana na anavyopenda yeye,kwanini wasilinde maslahi yake? vijana wanaambiwa wakiwa wanaadress mambo yao ya msingi wanaambiwa ni CHADEMA..huu ndio mtindo wa pale UDOM...na nadhani hata vyuo vingine vya umma.
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,043
  Likes Received: 3,072
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa feb 3,2007 pale diamond Jubilee nami nikiwa ndani ya nyumba
   
 4. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ujumbe umefika.Swali Je waziri usika ataisoma hiyo barua.?
   
 5. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nadhani wabunge wengi wangekuwa na mtazamo kama wa Mh. Mnyika basi matatizo ya vyuo vikuu nchini yasingalikuwepo tatizo wengi wao wamelala na wanadhani hayawahusu. Hongera Mh. Mnyika wa uwajibikaji wako.
   
 6. L

  Lua JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yeye kama mbunge ametimiza wajibu wake wa kuishauri serikali. kama hatoijibu itakuwa ni kiburi tu.
   
 7. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Thax sn bro John, kwa kuliona hlo, bt not only that 2claim kwa hyo wizara! Issue n kwamba hata wale 2lomalza na 2naotegemea kuajiriwa na hyo wizara bado 2po mtaani, it ths reality is contrary opposing km walvo sema bungen kua sept post zngekua zshatoka, wakaongeza tena kua 15 Nov zngekua out bt til now ni hadith hadth njoo uongo mtupu utawale.....! Cku s nyng x unver dents 2taandamana! Sjui sku ile ya kiama watajiteteaje af mi ntakua kiranja yan, watakoma! I ril hate tanzanian politics. Wameunguza 64 bilions kwa upuuzi! Broo Jay naomba na hili upoteze muda uwambie kua sku s nyng 2taingia kuchimba dawa il 2pate ya kula!
   
 8. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  siasa hapa kule
   
 9. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Good kaka endelea na ukomavu dhidi ya uonevu
   
Loading...