Marekebisho ya sheria ya kudhibiti fedha haramu.kwani huo muswada si nasikia jana ulikwama? pamoja na mswaada mwingine? nielemishe hasa walichokuwakuwa wanajadili ni mswada wa sheria gani huo?
cha kushangaza anasaidiwa kujibu point na chenge mimi nimejiuliza chenge yupo serikalini mpaka amsaidie AG hii nchi tunakwenda wapi yeye ni mbunge iweje awe kama mtu wa serikali. pili anatetea hiyo sheria kwa sababu anaogopa isije ikamkumba
je sheria ikoje kama kamati ilipitisha mabadiliko ya kifungu na bunge likawa limepitisha?
.....laiti kama ingewezekana ni bora tungepiga marufuku kura ya sauti,ya ndiyooooooooo na siyooooooooooooo
Hureéeeee ag. Pole hao ndo vijana tunaowataka sio nyie vikongwe na hao kina wasira wameamka t u wakaunga hoja nakuaidi subirini kidogo....wapi ms. Tehetehteh back home after ban.
Labda aache kukaa nyuma ya mgongo wa CDM (kwa kuwa keshaeleweaka yupo upande gani na sasa aanze kujikuza njee ya JF) siasa sio jukwaa hili pekee, ajipe the right publicity pengine he is better than Zitto.Wakuu nimeshangazwa na kitendo cha AG kutetea adhabu ya matumizi ya fedha haramu kubakia kama ilivyopendekezwa na seriklai ambayo ni kifungo kisichozidi miaka mitatu au faini isiyopungua sh mil 100 na kisichozidi Mil 500.
Mnyika alimbana AG vilivyo akipendekeza adhabu iende sambamba na kiwango cha pesa ulichopatikana nazo au mali au majengo ili kumfanya mtu au taasisi iliyotenda kosa hilo i feel kama adhabu kweli.
Binafsi nimejifunza kitu ya kwamba adhabu hizi zimependekezwa kuwa fare na serikali kwa ajili ya kuwalinda mafisadi wa nchi hii,maana baada ya kubanwa vilivyo na Mnyika nikaona Mh Chenge mzee wa vijisenti alinyanyuka na kwenda kwa AG Werema na nikaona anamuelekeza kitu kiasi cha kupoteza concetration ya kumsikiliza Mnyika aliekuwa akiendelea kutetea mapendekezo yake.
baada ya Mnyika kumaliza ndio nikaona kasimama na kupiga porojo tu huyu AG,nikagundua kwamba kama huyu asingekuwa fisadi llazima angejenga hoja kuhakikisha adhabu inaongezeka.
wakuu nawasilisha