Mnyika ambana AG jioni ya leo huko bungeni

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,411
733
Wakuu nimeshangazwa na kitendo cha AG kutetea adhabu ya matumizi ya fedha haramu kubakia kama ilivyopendekezwa na seriklai ambayo ni kifungo kisichozidi miaka mitatu au faini isiyopungua sh mil 100 na kisichozidi Mil 500.

Mnyika alimbana AG vilivyo akipendekeza adhabu iende sambamba na kiwango cha pesa ulichopatikana nazo au mali au majengo ili kumfanya mtu au taasisi iliyotenda kosa hilo i feel kama adhabu kweli.

Binafsi nimejifunza kitu ya kwamba adhabu hizi zimependekezwa kuwa fare na serikali kwa ajili ya kuwalinda mafisadi wa nchi hii,maana baada ya kubanwa vilivyo na Mnyika nikaona Mh Chenge mzee wa vijisenti alinyanyuka na kwenda kwa AG Werema na nikaona anamuelekeza kitu kiasi cha kupoteza concetration ya kumsikiliza Mnyika aliekuwa akiendelea kutetea mapendekezo yake.

baada ya Mnyika kumaliza ndio nikaona kasimama na kupiga porojo tu huyu AG,nikagundua kwamba kama huyu asingekuwa fisadi llazima angejenga hoja kuhakikisha adhabu inaongezeka.

wakuu nawasilisha
 
Wabunge waachwe wafanye kazi waliyotumwa na wapiga kura wao. Mwanasheria wa serikali anafanya nini bungeni? kazi inatakiwa iishie kwenye baraza la mawaziri sio bungeni.
 
kwani huo muswada si nasikia jana ulikwama? pamoja na mswaada mwingine? nielemishe hasa walichokuwakuwa wanajadili ni mswada wa sheria gani huo?
 
cha kushangaza anasaidiwa kujibu point na chenge mimi nimejiuliza chenge yupo serikalini mpaka amsaidie AG hii nchi tunakwenda wapi yeye ni mbunge iweje awe kama mtu wa serikali. pili anatetea hiyo sheria kwa sababu anaogopa isije ikamkumba

je sheria ikoje kama kamati ilipitisha mabadiliko ya kifungu na bunge likawa limepitisha?
 
kwani huo muswada si nasikia jana ulikwama? pamoja na mswaada mwingine? nielemishe hasa walichokuwakuwa wanajadili ni mswada wa sheria gani huo?
Marekebisho ya sheria ya kudhibiti fedha haramu.
 
Hapo ndo utapata picha kuwa serikali hii ya kirafiki.Lakini mwisho wao uko karibu.
 
cha kushangaza anasaidiwa kujibu point na chenge mimi nimejiuliza chenge yupo serikalini mpaka amsaidie AG hii nchi tunakwenda wapi yeye ni mbunge iweje awe kama mtu wa serikali. pili anatetea hiyo sheria kwa sababu anaogopa isije ikamkumba

je sheria ikoje kama kamati ilipitisha mabadiliko ya kifungu na bunge likawa limepitisha?

Mkuu nimesikitika kuona mbunge ambaye anatakiwa kuisimamia serikali na kuhakikisha anatunga sheria yenye lengo la kukomesha uhali ndio kwanza anakwenda kuitetea serikali,nadhani ni mkakati wa kukusanya fedha chafu kwa ajili ya 2015.shame on Chenge na Werema
 
alichokuwa anajaribu kufanya vijisenti ni kumuonesha yule kilaza werema nini zaidi aongeze kukataa hoja ya mnyika iliyokuwa imelenga kuwabana wabadhirifu ambao naye ni mwanachama wao na labda atarithisha wanaye ila kwenye katiba mpya tunataka adhabu ya wabadhirifu iwe KUNYONGWA
 
Hureéeeee ag. Pole hao ndo vijana tunaowataka sio nyie vikongwe na hao kina wasira wameamka t u wakaunga hoja nakuaidi subirini kidogo....wapi ms. Tehetehteh back home after ban.
 
tatizo ni mfumo mbaya wa sheria uliopo kwani kuna sheria ya rushwa ambayo inataja adhabu kubwa ni miaka saba na sheria hii ya Anti money laundry ACT ilikuwepo na hata ukiisoma haitekelezeki kwani haitoi tafsiri inayoeleweka ya fedha chafu ni zipi kwani imetoka katika nchi zilizoendelea ambayo mfano wake ni tofauti na wa kwetu.
 
mbunge anatoka kwenye nafas yake huyooo, mpk viti vya mawazir, then anamtonya mwanasheria mkuu jinsi ya kujibu. Dah! Nimepata kutambua ni kias gan AG. Ni kilaza. Hana point kaz yake kusema acha iwe hivyo hvyo, wabunge wa ccm kaz yao ni kusema ndiooo, na si kupima hoja.
 
Jana kuna mwanajamii mmoja hapa forum alidiriki kusema kwamba John Mnyika anatumika na ccm, kwa kwel ilikuwa vgumu sana kumuelewa mantiki yake hasa alilenga kumaanisha nn.

Bt kiukwel leo Mnyika ameonesha makucha yake jinsi anavyoweza kuchambua vifungu vya katiba pamoja na kanuni za bunge, like him.

Pia sitoweza kumusahau pia mheshimiwa Zuberi Kabwe Zitto kwa jinsi anavyochambua mambo ya uchumi kitaifa na kimataif.

Mungu azidi kwa tia nguvu na mapenzi mema kwa watanzania kwa ujumla bila kujali itikadi za vyama.
 
Nilisha wahi kusema kuwa sipendi kuamini kama huko CCM hakuna wasomi waliobobea,kiasi cha kushindwa kuleta hoja,siku zote hoja hupingwa kwa hoja laiti kama ingewezekana ni bora tungepiga marufuku kura ya sauti,ya ndiyooooooooo na siyooooooooooooo
 
Hureéeeee ag. Pole hao ndo vijana tunaowataka sio nyie vikongwe na hao kina wasira wameamka t u wakaunga hoja nakuaidi subirini kidogo....wapi ms. Tehetehteh back home after ban.

Wasira sio kikongwe wewe!
he is 63 now.
tembelea wovuti ya bunge umjue vizuri.
Punguza kuchotwa na ushabiki wa hapa JF!..
 
Wakuu nimeshangazwa na kitendo cha AG kutetea adhabu ya matumizi ya fedha haramu kubakia kama ilivyopendekezwa na seriklai ambayo ni kifungo kisichozidi miaka mitatu au faini isiyopungua sh mil 100 na kisichozidi Mil 500.

Mnyika alimbana AG vilivyo akipendekeza adhabu iende sambamba na kiwango cha pesa ulichopatikana nazo au mali au majengo ili kumfanya mtu au taasisi iliyotenda kosa hilo i feel kama adhabu kweli.

Binafsi nimejifunza kitu ya kwamba adhabu hizi zimependekezwa kuwa fare na serikali kwa ajili ya kuwalinda mafisadi wa nchi hii,maana baada ya kubanwa vilivyo na Mnyika nikaona Mh Chenge mzee wa vijisenti alinyanyuka na kwenda kwa AG Werema na nikaona anamuelekeza kitu kiasi cha kupoteza concetration ya kumsikiliza Mnyika aliekuwa akiendelea kutetea mapendekezo yake.

baada ya Mnyika kumaliza ndio nikaona kasimama na kupiga porojo tu huyu AG,nikagundua kwamba kama huyu asingekuwa fisadi llazima angejenga hoja kuhakikisha adhabu inaongezeka.

wakuu nawasilisha
Labda aache kukaa nyuma ya mgongo wa CDM (kwa kuwa keshaeleweaka yupo upande gani na sasa aanze kujikuza njee ya JF) siasa sio jukwaa hili pekee, ajipe the right publicity pengine he is better than Zitto.
 
Back
Top Bottom