Mnyika aibua tena ufisadi TANESCO

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,930
1,165
na Mwandishi wetu,

WAZIRI Kivuli wa Nishati na
Madini, John Mnyika, kwa
mara nyingine tena, ameibua
suala zima la mikataba tata
baina ya serikali na
makampuni ya umeme nchini, akimtaka pia Waziri mpya wa
Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo ataje
hadharani majina ya
watendaji wa Shirika la
Umeme nchini (TANESCO) wanaotuhumiwa kufanya
ubadhilifu mkubwa ndani ya
shirika hilo. Katika taarifa yake kwa umma
jana, Mnyika amemtaka waziri
huyo mbali na kuwaumbua
watendaji hao hadharani,
ahoji vyombo vya uchunguzi
vya kiserikali na mamlaka za nidhamu za watumishi hao ni
hatua zipi zilichukuliwa tangu
watendaji hao wahusishwe na
ubadhilifu. Mnyika alisema ufisadi hauko
TANESCO peke yake, bali
umejikita zaidi ndani ya
Wizara ya Nishati na Madini na
baadhi ya wataalamu kutoka
ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, ambao
wamesababisha nchi kuwa
katika hali mbaya. “Baadhi ya majina yao
yametajwa pia bungeni kwa
nyakati mbalimbali, hivyo
anachopaswa kufanya ni
kusimamia kwa vitendo
utekelezaji wa maazimio yaliyobaki ya Bunge ya
mwaka 2008 juu ya mkataba
baina ya TANESCO na kampuni
ya Richmond Development
Company LLC na ya mwaka
2011, kuhusu uhalali wa utaratibu wa wizara
kuchangisha fedha kwa ajili ya
kupitisha bajeti bungeni na
kuhusu uendeshaji wa sekta
ndogo ya gesi nchini,” alisema. Mnyika akizungumzia
mikataba hiyo, alisema ni
miaka minne toka maazimio
yapitishwe na Bunge, ambalo
liliagiza kwamba mkataba
kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC
(uliorithiwa na Dowans
Holdings S.A.) na ile kati ya
TANESCO na IPTL, SONGAS,
AGGREKO na Alstom Power
Rentals, ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo
mikataba ya madini
ilivyopitiwa upya na serikali. “Iwapo azimio hili
lingetekelezwa kwa ukamilifu
wake, gharama za uzalishaji
TANESCO na serikali kwa
ujumla zinazotokana na
matatizo katika mikataba zingepungua,” alisema na
kuongeza; “Pia, Azimio Na. 1 lilitaka
serikali izihusishe kamati za
kudumu za Bunge kwenye
hatua za awali za maandalizi
ya mikataba mikubwa ya
muda mrefu ya kibiashara ili kuondokana na utaratibu
uliopitwa na kwamba
mikataba ya kibiashara ni siri
hata kwa walipa kodi
wenyewe.” Alisema serikali imeshindwa
kutekeleza azimio hilo na
matokeo yake ni kwamba,
kati ya mwaka 2008 mpaka
2012 kumeendelea kuwa na
usiri katika hatua za awali za maandalizi ya mikataba, na
pia mikataba mingi mikubwa
haijafanyiwa mapitio. Aliongeza kuwa, utaratibu wa
sasa kwa mujibu wa Sheria ya
Kinga, Haki na Madaraka ya
Bunge ya mwaka 1988
pamoja na kanuni na taratibu
za Bunge, ambao mbunge anaweza kuomba kwa serikali
kupitia kwa ofisi ya Bunge
nakala ya mikataba baada ya
kusainiwa, hauliwezeshi
Bunge kutimiza kikamilifu
wajibu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 63 ya
kuisimamia serikali katika
hatua zote muhimu. Hata hivyo, Mnyika alimuunga
mkono Waziri Muhongo katika
azma ya kutumia wataalamu
wa ndani kabla ya wataalamu
wa nje, na kumtaka aagize
ukaguzi maalumu ili wataalamu na makandarasi
waliohusika katika ufisadi
dhidi ya TANESCO na mashirika
mengine yaliyo chini ya
Wizara ya Nishati na Madini
waondolewe katika orodha (black listing). Alimtaka Muhongo mbali na
kusimamia ongezeko la
uzalishaji na usambazaji wa
umeme, azingatie kuwa
matatizo ya sasa ni matokeo
ya udhaifu wa kisera na kiutendaji kuanzia wakati wa
Rais wa awamu ya pili, Ali
Hassan Mwinyi na baadaye
kwa Rais Benjamin Mkapa
ambapo TANESCO iliwekwa
kwenye orodha ya mashirika ya kubinafsishwa na hivyo
serikali kuacha kuwekeza
kikamilifu katika uzalishaji wa
umeme pamoja na
matengenezo ya
miundombinu ya usafirishaji na usambazaji. Aidha, alisema ni katika
kipindi hicho hicho kuliibuka
matatizo pia ya ufisadi
kwenye uwekezaji katika
sekta ya nishati kama ya IPTL,
Kiwira, Net Group Solution nk. “Awamu ya nne ya Rais
Kikwete nayo ikaongeza zaidi
mzigo kwa TANESCO kupitia
miradi mingine ya kifisadi
kama ya Richmond na sasa
kuna tuhuma mpya za ufisadi kuhusu utekelezaji wa
mpango wa dharura wa
umeme. “Mpango wa Dharura
uliwasilishwa bungeni tarehe
13 Agosti 2011, ahadi ya
serikali ilikuwa kuongeza MW
572 ifikapo mwezi Desemba
2011 na kuweka orodha ya mitambo ya kununua kabla ya
Oktoba 2012. “Pamoja na kuwa na mpango
wa gharama kubwa wa
dharura ambao unahusisha
kwa sehemu kubwa suluhisho
la muda mfupi la kukodi
mitambo, bado utekelezaji wa mpango wenyewe nao
unasuasua hali inayodhihirisha
kuendelea kwa uzembe na
udhaifu katika serikali. “Hata mitambo iliyofungwa
nayo haina uhakika wa kuwa
na uwezo wa kuendeshwa
wakati wote uliopangwa
kutokana na madeni TANESCO
ambayo inadaiwa, serikali kushindwa kutekeleza
kikamilifu ahadi ilizotoa kwa
TANESCO na pia upungufu wa
gesi kwa ajili ya kuendeshea
mitambo husika na kuwa
tishio kwa nchi kuingia gizani katika siku za usoni. Kati ya
miradi ambayo utekelezaji
wake umesuasua kinyume na
ahadi za serikali bungeni ni
pamoja na kununua mtambo
wa MW 150 wa NSSF na kununua mitambo ya MW 100
wa TANESCO Ubungo,” alisema
Mnyika. Kwa upande mwingine,
Mnyika alisema udhaifu wa
kutokutekeleza mipango ya
uzalishaji wa gesi na makaa
ya mawe kwa wakati
umesababisha utegemezi mkubwa kwenye matumizi ya
mafuta katika mitambo ya
kuzalisha umeme wa dharura. Alidai kuwa zaidi ya nusu ya
umeme unaozalishwa nchini
hivi sasa ambao ni sawa na
takribani MW 660,
unazalishwa kwa kutumia
dizeli, mafuta ya ndege na mafuta mazito hali ambayo
imeongeza mahitaji makubwa
ya uagizaji wa mafuta toka
nje ya nchi. “Hii imesababisha mahitaji
makubwa ya fedha za kigeni
kwa ajili ya kuagiza mafuta,
na hivyo kuchangia katika
kuporomoka kwa thamani ya
shilingi. Aidha, ongezeko kubwa la uagizaji toka nje
limeathiri urari wa biashara na
hivyo kuchangia katika
mfumuko wa bei, ambao
umesababisha Watanzania
kubeba mzigo wa kupanda kwa bei za bidhaa na gharama
za maisha kwa ujumla
kutokana na ufisadi kwenye
mikataba, ubadhirifu katika
matumizi, uzembe katika
uongozi na upungufu katika utekelezaji wa mipango
mbalimbali ya serikali kwenye
sekta ya nishati,” alisema. Hii ni mara ya pili ndani ya
siku mbili kwa Mnyika
kuwashukia mawaziri wapya. Juzi, mbunge huyo alimtaka
Waziri wa Maji, Profesa
Jumanne Maghembe achukue
hatua na kueleza bayana
namna kilivyotumika kiasi cha
dola za Marekani milioni 164 kwa ajili ya usambazaji wa
miundomimbinu ya maji jijini
Dar es Salaam ambayo
imeshindwa kufanya kazi
kikamilifu.
Chanzo:TANZANIA DAIMA
 
Pongezi za dhati kwa Mhe Mnyika kwa ufuatiliaji anaofanya, hasa kwa kazi kubwa anayoifanya.

tuko pamoja kamanda mpaka kieleweke 2015,

ni muda umefika watanzania wajue kuwa haya yanayofanywa na Kikwete na ccm ni mchezo wa kuigiza na kutufanya tuonekane wajinga.

hivi rais kavunja baraza la mawaziri mara 4, alafu mnataka kuniambia kosa ni la mawaziri hapana tatizo ni rais na chama cha ccm. na kila siku wataendelea na mchezo huu mpaka watanzania kwa pamoja tutaweka itikadi za udini, ukabila na ubinafsi ndio tutafanyikiwa, wanataka kutugawa ili watutawale lakini mwisho wa siku itakuwa ni wewe msukuma/mchaga/mpare/mmakonde/mhaya etc ambao tutateseka na kuwa watumwa kwenye nchi yetu. wakati wao wanakula na kuimaliza nchi kwa tamaa na ubinafsi wao.

Tanzania tuwe makini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom