Mpango mzima nikuikataa rasimu ya katiba, bila hivyo watanzania tutazidi kuchezewa kama mazuzu na familia za watawala..1. Unafiki kuhusu aina gani ipi ya muungano tuufuate, nimewasikia watu wenye busara zao, wakishindana kwa jazba mate yakiwatoka, ni aina ipi ya serikali tuufuate? Jibu la watu walio na kweli ndani yao, jibu ni rahisi. Tuwe na serikali moja, ya watu wamoja, wanaopendana, tuwe na taifa lisilo na mipaka, raisi mmoja, zanzibar uwe ni mkoa ktk Taifa la jamuhuri ya Tanzania.Kwa kuli zenu za serikali mbili, tatu au nne. Hakuna muungano, kuna siku mtatengana tu, maana hakuna ukweli ndani yenu. Kuna siku kila mmoja wenu ataamua kwenda njia yake. Kwa maana ukichunguza sana utaona kila nchi inahitaji uhuru wake. Wanashindwa kusema ukweli kwa ajili yakutokuwa wawazi. Jibu sahihi kama kweli tunataka muungano tuwe na serikali moja, tuache unafiki.2. Kuhusu maadili ya uongozi, katiba ni kwa manufaa ya Watanzania. Tuunde katiba itakayowafanya watawala wawe makini na waadilifu katika uongozi wao kwa miongo yote ya utawala Tanzania.Katiba itamke wazi kuwa. Serikali yoyote itakayokuwa madarakani kwa kipindi chochote kile. Ikionyesha madhaifu yoyote yakukiuka katiba ya nchi, ubadhilifu, rushwa au serikali ikionyesha hali inayoleta mashaka kwa kutumia madaraka vibaya ya kukandamiza uhuru wa raia wake. Basi katiba itamke wazi kwamba Watanzania wote wenye umri wa miaka 18 nakuendelea, wafanye maandamano ya Amani kwa idadi ya watu isiyo na kikomo, hadi makao makuu ya nchi kushinikiza serikali kujiuzulu. Hii itasaidia kuzuia viongozi kufanya wanavyotaka, kujinufaisha binafsi na kuisababishia taifa hasara. Kung'ang'ania madarakani na kujifanya miungu watu. Bila mambo haya kukubaliwa watanzania tuikatae katiba hii maana katiba pendekezwa ni kwa ajili yakunufaisha familia za viongozi walioko madarakani pekee.