Mnatupa shida kuwaamini ingawa mioyo i-radhi

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
..TUNAPATA TABU KWAAMINI.




Kamusi ya kiswahili imetoa tafsiri ya neno "unafiki" kuwa ni hali ya kujifanya kua rafiki au kutokua mkweli.Kwenye biblia unafiki umezungumzwa kwenye aya na sura nyingi ikiwepo Matayo 23:28 " Vivyo hivyo nanyi kwa nje mwaonekana watu wema na wenye haki bali ndani mmejaa unafiki na maasi",zaidi "wanafiki wanachokisema siwa nachokiamini(Al-Baragash 2/8).

Hivyo tukichanganya mtazamo wa lugha tukajumlisha na mtazamo wa kiimani katika neno "unafiki" tutapata maana pana zaidi iliyorefuka na kunenepa, ambayo ni utovu wa ukweli katika muendelezo wa binadamu hasa kwa lengo la kujipatia sifa.Nia ya ndani ya mnafiki ni tofauti na anachotenda nje.Lengo la mnafiki ni kupendelea watu wengine ili kupata faida kwao.

Mtu mnafiki anategemea mapato yake katika kuongea na kutenda katika mfumo wa kuridhisha kila kitu ,kumfurahisha kila mtu aliyepo upande unaotaka kunufaika nao.Moja ya kundi kubwa sana duniani lenye tabia za unafiki na usaliti ni wanasiasa hasa wa nchi za Kiafrika.Kwa Tanzania unafiki imekua kawaida.

Ikumbukwe hivi karibun vyama 6 vya upinzani nchini vilikutana mjini humo na kuzaa kitu walichokiita "Azimio la Zanzibar" na kuazimia mwaka 2019 kuwa mwaka wa kudai Demokrasia.Katika moja ya maazimio ni kufanya maandamano ya kudai Demokrasia Zanzibar Januari 12, mwaka huu.

Vyama hivyo sita viliwakilishwa na Maalim Seif Sharifu Hemedi(CUF),Oscar Makaidi(NLD), Hashimu Rungwe Spunda(CHAUMA),Zito Zuberi Kabwe(ACT Wazalendo),James Mbatia (NCCR MAGEUZI),Salumu Mwalimu(CHADEMA).Wakishuhudiwa na baadhi ya watu walioawaalika akiwemo rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika(TLS),Bi Fatma Karume,Jenerali Ulimwengu na aliyekua mgombea wa kiti cha urais kupitia UKAWA 2015 Edward Lowassa.

Hoja ya Tanzania ina demokrasia au haina haina kupitia Azimio hilo la Zanziba halitonoga kabla ya kuwakujadli hawa wanye Azimio
ni watu wa aina gani?waumini wa Demokrasia wanayoidai?wanafanana kwenye nini na wanatofautina wapi?vyama wanavyoongoza vinaendeshwa katika misingi ya Demokrasia?upatinaji wa uongozi wao ulitokana na Demonkrasia kutamalaki?

Ni vizuri sana kabla watanzania hawajaamua kati ya kuwaamini ama kutokuwaamini tukatathimini usahihi na uhalali wa taasisi wanazotoka,maisha yao ya kisiasa na historia zao ili tuone kama wanatosha na kuenea kwenye tafsiri ya neno"unafiki"

CHAMA CHA DMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA)

Hiki ni chama chenye mwenyekiti aliyedumu katika nafasi miaka 15 mpaka sasa .Mtoto aiyezaliwa wakati Freeman Elikaeli Mbowe anapokea uenyekit wa chama hiko mwaka 2004,sasa atakua anasoma kidato cha kwanza.Chadema ya Mbowe haijawahi kuamini kwenye Demokrasi.

Katika uongozi wake wengi waliotajwa tajwa kukitaka kiti cha uenyekiti wa chama hiko hawakutoka salama.Ilianza kwa marehemu Chacha Wange hadi Kina Zitto Kabwe,Samsoni Mwigamba na hivi karibuni Mwita Mwaikabe Marwa.Je huyu angekua kiongozi mwenye dola iliyokamilika(Polisi,Magaereza,mamlaka) nini wangefanyiwa kina Zitto na wengine walioitaka nafasi yake?

Ndani ya chama hiki yupo Edward Ngoyai Lowassa aliyehamia CHADEMA jumanne ya Julai 28,2015 na kukabidhiwa kadi katika Hotel ya bahari jijini Dar es-Salaam siku 27 baada ya jina lake kukatwa na kamati kuu ya ccm julai 11,2015.

Lowassa aliyezaliwa Agust 26, 1953 si muumini kabisa wa Demokrasia wa kiwango cha kufikiri mtu anayefaa kua rais kwa Tanzania ni yeye tu ndio maana hakuridhika na kukatwa kwa jina lake na hakuridhika hata baada ya matokeo kutangazwa kwa kudai ameibiwa kura.Je anadai demokrasia au muendelezo wa jitihada zake za kuitaka Ikulu?

Aliyekiwakilisha chama hiko huko Zanzibar ni naibu katibu mkuu wake upande wa bara Salumu Mwalimu ambaye uteuzi wa nafasi hiyo unathibitisha pia namna CHADEMA sivyo jali Demokrasia na kuthamini uwezo wa wanachama wake.Miongoni mwa wanachedema wengi waliostahili kua manaibu katibu wa chama hiko huyu si mmoja wapo kulinganisha na uwezo wa walioachwa,kwa sababu hii wanachama wengi wa chama hiko Zanzibar wamekisusa chama hiko tangu mtangazaji huyo wa zamani wa runinga aikwae nafasi hiyo.Kinachompa ahueni ni ukaribu wake na mwenyekiti wa chama.

Pamoja na utitiri wote wa matendo yanayokwenda tofauti na misingi ya kidemokrasia ndani ya chama hiko,CHADEMA ni moja ya vyama vilivyo kwenye Azimio la Zanzibar kudai demokrasia.Hivi mhalifu anayedai polisi ni wasumbufu inachukua muda gani kumuamini?

NATIONAL LEAGUE FOR DEMOCRACY-NLD.

Hiki ni chama kingine kilichoshiriki kuandaa azimio hilo la Zanzibar kikidai Demokrasia.Chama hiki kilichoanzishwa Machi 21, 1993 kimewahi kuongozwa na wenyeviti wawili tu katika miaka 26 ya uhai wake ambao ni mtu na mwanae.Mwenyekti wa kwanza wa NLD ni marehemu Emanuel Makaidi.na wa sasa ni Oscar Emanuel Makaidi(mtoto wa mwenyekiti wa kwanza:.

NLD isiyojulikana hata ofisi zake zilipo ilikaa miezi sita bila ya mwenyekiti baada ya kufariki kwa baba mzazi wa mwenyekiti wa sasa marehemu Emanuel Makaidi na April 27,2016 "kumuweka" Osca Makaidi kama mwenyekiti wa chama hiko kuziba pengo la baba yake.

Ukiacha viongozi hawa wawili chama hiki viongozi wake wengine ngazi ya taifa,mikoa hata wilaya hawakulikani.Pamoja na kua na sura ya kifamilia ni moja ya chama kinachodai demokrasia ndani ya Azimio la Zanzibar.Chama kinachoendeshwa kifamilia kinasimama kudai demokrasia ya nchi?Kinaanzaje kuaminika,kwa nini usijiulize kuna kinachotafutwa hapa zaidi ya hiyo demokrasia?Hata kujijenga na kufanya uchaguzi tangu mwaka 1993 walikatazwa?

CIVIC UNITED FRONT_CUF CHAMA CHA WANANCHI.

Hiki ni chama cha kwanza cha upinzani kupata usajili baada mfumo wa vyama vingi n uanze rasm hapa nchini mwaka 1992.Tangu kuanzishwa kwake Februari 12,1992 Cuf haijawahi kua na katibu mkuu na mwenyekiti mwingine nje ya Maalim Seif na Profesa Ibrahim Lipumba.Ni rais Magufuli anaikataza CUF isichague katibu na mwinyekiti mwingine miaka yote 26?

Licha ya ufalme wao katika nafasi hizo mbili,chama hiki hakijawahi kua na mgombea wa nafasi ya urais kwa miaka 20 nje ya Maalimu Seif na Profesa Lipumba.Nani anateua wagombea wa nafasi za urais ndani ya chama hiki? Kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa wanakodai kumechangiaje Lipumba na Maalim Seif kugombea urais miaka 20 mfululizo?

Katika Azimio hilo ,CUF iliwakilishwa na katibu mkuu wake asiyetambulika msajili wa vyama vya siasa na mwenyekiti anayetambulika na msajili wa vyama vya siasa.Chama kisicho na demokrasia,chenye viongozi waliokaa madarakani kwa miaka 26 kinashiriki kudai demokrasia ya nchi.Kwa nini CUF isitengeneze demokrasia ndani ya chama chao?.Chama chenye vyama viwili ndani yake kinasimamaje kudai demokrasia pana katikati ya vidonda wanavyoumizana?

Maalimu Sief aliyezaliwa Oktoba 22,1943 alijiunga siasa za upinzani baada ya kufukuzwa chama cha mapinduzi mwaka 1988.

Kama ilivyo kwa Mbowe wa CHADEMA,maalim anakumbukwa jinsi alivyowashughulikia wote walioonesha kuitaka nafafasi yake akiwemo rafiki yake wa karibu wakati huo Hamadi Rashid aliyemvua uanachama

PART FOR PEOPLE'S REDEMPTION(CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA)-CHAUMA.

Chama hiki kinachoongozwa na Hashimu Rungwe Spunda kwenye azimio hilo kiliwakiliswa na Hashimu Rungwe mwenyewe. Kilianzishwa na kusajiliwa mwaka 2013.Rungwe aliyezaliwa Januari 1,1994 alinzisha chama hiki baada ya kuchoka kutangatanga kwenye vyama mbalimbali.

Mwaka 1966-1977 alikua mwanachama wa TANU,na mwaka 1995-1997alikua chama cha mapinduzi (CCM),kabla ya mwaka 1996 kutimkia NCCR Mageuzi ambapo alikaa mpaka mwaka 2012 alipoondoka na kuanzisha chama chake cha CHAUMA.

Ukiacha Hashimu Rungwe asiyejulikana uenyekiti wake ulipatikana kwenye mchakato upi katika chama hiko ambacho ni mali yake, hakuna kiongozi mwingine wa chama hiko hata ngazi ya kata anayejulikana.Chama chenye kiongozi mmoja tu nchi nzima amabye mchakato wa kumuweka madarakani haujulikani kinasimama kudai demokrasia ya ndani.Kwa nini muda anaoutumia Spunda katika hiko kinachoitwa demokrasia asijaribu kutuonesha namna chama chake kinavyonukia demokrasia kwa kutaja katibu mkuu wa chama hiko,msemaji au katibu mwenezi na wajumbe wa kamati ama almashauri kuu kama ipo wakajulikana?

Chama ambacho mweka hazina huyo huyo,katibu mkuu huyo huyo ikifika wakati wa uchaguzi huyo huyo anagombea kinawezaje kudai demokrasia ya nje kabla ya ndani?

NATIONAL CONVENTION FOR CONSTITUTIONAL AND RECONSTRUCTION-NCCR MAGEUZI.

Kinaongozwa na James Mbatia aliyezaliwa Juni 10,1964 kama mwenyekiti.Mbatia aliyekua mwenyekiti wa kwanza wa vijana wa chaa
Chama hiko kwa kipindi cha miaka 8(1992-200)chama hiko kabla ya kuwa mwenyekiti taifa mwaka 2000 baada ya kuondoka kina Mabere Marando na Dr Lamwai si mwanademokrasia ndani ya chama chake.

Itakumbukwa mwaka 2011 alivyowashughulikia David Kafulila na aliyekua mbunge Muhambwe Felix Mkosamali baada ya kuvuja kwa tetesi kua wanajiandaa kumtoa kwenye nafasi yake ya uenyekiti.

Lakini pia Mbatia alikubali uchaguzi wa mwaka 2015 "kukitoa sadaka"chama chake kwa gharama ya kupoteza wabunge wote ili yeye apate msaada wa ukawa kushinda kiti cha ubunge jimbo la vunjo.Na yeye pia na chama chair wanaleta ukakasi wa kuaminika wanapodai demokrasia aliyoshindwa kuiishi ndani ya chama chake

ALLINCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY-ACT WAZALENDO.

Chama hiki klichopata usajili wake mwaka 2014 kinaongozwa na Zitto Kabwe kama kiongozi mkuu.Kilianzishwa na Kina Lucas Limbu na wenzake kabla ya kufukuzwa na kundi la wakina Zitto.

Kwenye Azimio hilo la Zanzibar kiliwakilishwa na Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe mwenye kadi ya chama hiko namba 007194.

Kwa maneno ya mbunge wa Arusha Godbless Lema,Zitto ni mmoja ya wanasiasa Lema
wanafiki. Maandishi hayaozi,Lema aliyeandika katika moja ya ya kurasa zake za mitandao ya kijamii kula "Zitto sio mzalendo katika suala lolote na hata kwenye maisha yake yote" Akimtuhumu kukataa posho ya shilingi elfu 70,000 kwenye vikao vya bunge na kupokea posho ya shilingi 700,000 kwenye vikao vya machining mbalimbali hususani mashirika ya hifadhi ya jamii alipokua anashiriki kama mwenyekiti wa kamati ya PAC.

HITIMISHO.

Ni vyema vyama vyote vilivyoungana kwenye Azimio la Zanzibar linalodai kulilia demokrasia virudi ndani ya vyumba vyao kuziba viraka vya demokrasia vilivyopo kabla nguo hazijachanika kabisa.

Kwakua sehemu kubwa ya viongozi walioshiriki kwenye Azimio hilo maisha yao ya kisiasa yanatia mashaka sana kutokana na ama kufukuzwa kwenye vyama vyao vya awali au kuhamaha sana,inatia ukakasi wa wa wanachopigania ni vyema wakawapisha wengine wasio mawaa kwenye safari zao za kisiasa.

Mfano,Zitto alifukuzwa Chadema,Hashimu Rungwe alipuyanga kuanzia TANU&CCM,NCCR MAGEUZI mpaka CHAUMA,Maalim Self alifukuzwa CCM,Lowassa alikatwa CCM.Unaweza kutaka kujiaminisha safari yao ilikua ya kuisaka demokrasia lakini mbona wamekua vinara wa kuwaumiz wenzao ndani ya vyama?Maalim mwaka wa 25 sasa ni katibu mkuu,Rungwe kamati kuu ni yeye mwenyewe,almashauri yeye mwenyewe ?

Robert Crooks na Jean Stein kwenyd kitabu maarufu cha "Psychology Science" wanasema mfanano wa binadamu katika malengo inaweza kua sababu kubwa ya binadamu hao kuwa pamoja kabla ya kutimia kwa lengo hilo na kuachana baada ya lengo kutimia.Kwa namna ya wanasiasa wote waliouhusika kulitengeneza azimio hilo na historia yao ya kisiasa ilivyokosa kueleweka ni wazi kinachotafutwa sio demokrasia ni malengo yao wenyewe yanayothibitshwa na sababu za kufukuzwa kwenye vyama walivyotoka.

Tukifikiri sawa sawa kadri ya Thomas Alva mgunduzi huyu wa balbu anavyotaka hitimisho sahihi litakua swali hili,Kwakua wanachodai wapewe wameshindwa kukitoa kwa wengine hata walipokua nacho.


Noel Nguzo.R.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom