Mnataka maridhiano ? Basi fanyeni haya

Mnataka maridhiano ? Basi fanyeni haya

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,036
Reaction score
2,130
Kwanza mseme hayo maridhiano mnataka na kina nani ?

Kwa sababu hadi sasa hamjakiri kosa la kuiba kura kwa kiwango cha 98%, hamja kubali kua mmeua watanzania walioingia barabarani , mmekamata watanzania wakubwa kwa wadogo na kuwapa kesi ya Uhaini nchi nzima, lakini mmekiri kua fujo zilifanywa na wageni na sio watanzania.
Sasa mnataka maridhiano na nani hasa na kwa kosa gani mridhiane ?

1. Mkiri kosa mlilofanya

2. Walio katika nafasi na kuruhusu yatokee yaliyotokea wawajibishwe

3. Wananchi wote nchi nzima waliokamatwa na kupewa kesi waachiwe huru bila masharti

4. Waliotekwa wote warudishwe wakiwa hai au maiti

5. Kue na uhuru wa maoni

6. Familia zilizopoteza wapendwa wao tuambiwe zinafarijiwa namna ganj hata kama kwa kuungana Taifa zima.

7. Tutengeneze na majirani mahali tulipo wajeruhi.

8. Wananchi tusikilizwe tunataka nchi yetu iweje na viongozi wa namna gani tunawataka.
........kuna ambalo nimesahau ? Ongeza hapo chini
 
Back
Top Bottom