the truecaller
JF-Expert Member
- May 8, 2019
- 809
- 940
Hodi JF,
Moderator niache peke yangu tafadhali sana!
Mimi naweza kuwa mgeni humu jukwaani,lakini ni mwenyeji wa Tanzania hii.ni nyumbani kwa baba na mama yangu pia.
Tumezowea misiba yetu Tanzania kuwa na maombolezo yanayoendana na utani na vioja mbalimbali, kutoka kwa makabila mbalimbali nchini mwetu,jambo ambalo ni kawaida kabisa.nimewahi kuona mtani mmoja katika kabila fulani akikatalia ndani ya kaburi,eti mpaka apewe tumbaku nk.
Ila leo nimeona watu hawa wakikataa utani,nimeona ndugu zetu hawa wakikuza na kulitolea tafsiri tamko la mtanzania mwenzao,pale tu alipolitoa katika mfumo uliokaa kiutani.
Lakini kwa ajili ya siasa,kwa ajili ya chuki iliyomo miongoni mwa waombolezaji wale ambayo ni ya kisiasa zaidi.
Basi wamegeuza shughuli nzima ikawa ni ulingo wa kuwananga na kuwakejeli wale walio na mlengo tofauti na wao kisiasa.
Tena ndani ya mimbali mitakatifu ya madhabahu.
Tena bila kujali hawa ndugu,pamoja na nyadhifa zao kisiasa na kiutawala.
Pale walikuwa nyumbani kwao marehemu mpendwa wa wahudhuriaji wote,bila kujali kabila wala itikadi zao za kisiasa duh!
Lakini pia walikuwa sebuleni kwao ndugu wa jamii ya mwendazake.
Hawakupaswa kutumia tukio lile kwa namna walivyolitumia.
Lakini pia Baba huyo mwenye mimbari yake,hakuwa na maneno unganishi na yenye funzo na upendo ili kufikisha ujumbe ule?
Bila kuzalisha kilichochozaliwa pale?
Mimi nimefuatilia kwa kina,hotuba na maoni ya watu mbalimbali waliopata nafasi ya kuhojiwa na vyombo vya habari leo.
Kuna kundi fulani hivi,hotuba na maoni yao vilidhihirisha vijembe na mipasho ya wazi tu.
Lakini nimegundua wengi wa wanasiasa wetu,huyu mzee kaondoka katika kipindi muhimu sana walichokuwa wanajiandaa kunufaika nae au kushirikiana nae kwa namna fulani na kawaacha bila maandalizi yao kimkakati.
Nawakilisha wazo langu kama raia huru.[emoji1241]