Mnaopenda kununua kuku wa kienyeji sokoni bora mkachinje wenyewe, mtanishukuru

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,722
Bahati nzuri kuishi kwenye uhuni ndio nimekulia na kila siku nawapa code ngumu kumeza. Wafanya biashara wa kuku wa kienyeji waliopo sokoni asilimia kubwa ni wajanja sana.

Embu fikiria kuku wametoka vijijini mpaka kufika sehemu ya soko mfano mijini lazima kuna kuku watakufa, wamechoka na wangine hawajanona kama mnavo waona bandani.

Hii tabia ipo sana, yaani mtu anabanda pale sokoni wewe unachagua kuku mnapatana bei na utataka uchinjiwe. Usipokuwa makini akienda huko kuchinjwa bora aje na manyoa utaweza kujua kuliko kuja kanyonyolewa na tayari kashakatwa. Hapa utakuwa umepewa kibudu au tofauti na yule uliyemuona bandani.

Ukitoka anarudishwa tena ili wateja wafike bei. Hii ni sample ya kuku tu, kwenye machinjio huko acha ni nyamaze tuendelee kula nyama.
 
Ila kila mahali ni makanjanja tu
Hata Xmas uk wakati Bata Mzinga wanalishwa miezi 3 ili wanenepe wengi huwa wanakufa ila hawatupwi

Walileta kipindi jamaa walijifanya kuomba kazi kumbe waandishi wa Habari

Walirekodi kila kitu yaani jamaa wakiona Bata mzinga anahangaika roho kutoka wananyonga tu

Duniani watu wanakula vya kunyonga sana
BBC walirekodi hiyo na walipigwa faini wenye farm ila ndio hivyo tena eti Xmas bila Bata mzinga hainogi
 
Bahati nzuri kuishi kwenye uhuni ndio nimekulia na kila siku nawapa code ngumu kumeza. Wafanya biashara wa kuku wa kienyeji waliopo sokoni asilimia kubwa ni wajanja sana.

Embu fikiria kuku wametoka vijijini mpaka kufika sehemu ya soko mfano mijini lazima kuna kuku watakufa, wamechoka na wangine hawajanona kama mnavo waona bandani.

Hii tabia ipo sana, yaani mtu anabanda pale sokoni wewe unachagua kuku mnapatana bei na utataka uchinjiwe. Usipokuwa makini akienda huko kuchinjwa bora aje na manyoa utaweza kujua kuliko kuja kanyonyolewa na tayari kashakatwa. Hapa utakuwa umepewa kibudu au tofauti na yule uliyemuona bandani.

Ukitoka anarudishwa tena ili wateja wafike bei. Hii ni sample ya kuku tu, kwenye machinjio huko acha ni nyamaze tuendelee kula nyama.
Tena ukiwa maeneo ya kuchinjia mteja unawekwa mbali na pale wanapochinja....Ila Mungu nae anatulinda sana waja wake
 
Kuku aliyetoka kuchinjwa lazima awe fresh wa motomoto, mtapigwa nyie ambao hamjui kutofautisha kuku fresh aliyetoka kuchinjwa na mzoga.
Kama wanamnyonyoa na maji ya moto unategea atakua wa baridi?
Mzoga ni mzoga tu hata unyonyoe na maji ya moto, kwa msiojua ndo mtapigwa.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom