Mnaomuonea wivu na kumchukia Magufuli, msiwe kama Kaini aliyeamua kumuua nduguye

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,932
2,833
Magufuli, mheshimiwa rais wetu, amewatendea mema watz na kulinda maliasili yetu kwa wivu mkubwa! Pia amewalinda watz kutokana na propaganda za corona na kuokoa maisha wa watz wengi Sana kwa kuibua Mambo kadhaa yaliyopelekea watu kuanza kuhoji uwepo wa corona na kiwango Cha hofu kilichojengeka ktk dunia ambacho ndio hasa kilikuwa kikiua zaidi watu.

Pia aliwaelekeza watz kukimbilia kwa Mungu kunapotokea Jambo ambalo linaonyesha wazi kutokuwa na utatuzi wa kawaida kutoka kwa wanadamu! Matokeo yake corona na covid-19 imetokomea kusiko Julikana, na Tz na watz kuendelea kudunda salama salimini! Kwa bahati mbaya Sana wapo watu wanaochukia Sana kwa jinsi Mh. Rais wetu huyu anavyopata kibali kwa Watanzania na dunia nzima na wamekuwa wakipambana sana ili kupotosha ukweli halisi! Nawaomba msiwe kama Kaini aliamua kumuua nduguye Abili kwa chuki za wivu.

Kumuua habili aliyepata kibali kwa Mungu hakukumfanya Kaini apate kibali ila alilaaniwa

Kupambana na wenye kibali hakukufanyi na wewe upate kibali utaishia kupata laana

Kuwachukia waliofanikiwa hakukufanyi na wewe ufanikiwe

Jifunze kuwakubali wengine, kuwabariki wengine, kuwaombea waliofanikiwa.

Ukitenda mema na wewe utapata kibali.

Roho ya wivu inaua, usiwaonee wivu waliopata kibali

Mwanzo 4:6 BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
 
Mwanzo 4:6 BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Unajua hata shetani alivyokuwa anamjaribu Bwana Yesu kule nyikani naye alitumia maandiko. Hivyo sishangai kuona kitu kama hichi ambacho umekiandika hapa kwa kunukuu Biblia.
 
We
Unajua hata shetani alivyokuwa anamjaribu Bwana Yesu kule nyikani naye alitumia maandiko. Hivyo sishangai kuona kitu kama hichi ambacho umekiandika hapa kwa kunukuu Biblia.
Ww Una roho ya Kain! Tubu shauri yako!
 
Ujio wa Lissu unaweza kusababisha heart attack kwa watu wengine!
Nafikiri kwake mwenyewe TL maana sio kwa maendeleo tuliyopiga Tz ya Magu! Domo kaya kaja! Mwambie asifungue Hilo Domo maana hatuna me da nalo maana hapa ni kazi tu!
 
Kwa nini aonewe wivu na zaidi kwa nini achukiwe?Anza na yeye.Anakosea wapi?Achana na kulaumu watu kabla haujaanza kumkagua umsifiaye tu.Be reasonable, specific and clear to the point,fella!
 
Hero,

Hivi haya ukiwaambia wazazi, ndugu, marafiki na jamaa wa Ben Saa8, Azory, nk... na wale weeeengi wa kwenye viroba, watakuonaje?? Siyo Kama shetwani binti Rajim?!
 
Hero,

Kuna mtu alitaka kumuua Magufuli ili mfano wako uwe relevant? Kaini alikuwa mtoto mkubwa, (Magufuli Rais), sasa hapo yeye si ndo Kaini anayetafuna wenzake (Lissu + Mangula)?
 
Hero,
Sijawahi kumchukia huyu Mzee, na alikua rafiki yangu tangu akiishi pale Kinondoni! Hii sample yako sijui umeitoa wapi! Mnajihisi, mnajishuku, mnajipendekeza kwa huyu Mzee. Ndio maana juzi kawaumbua Dodoma kuwa acheni kujipendekeza.
 
Kuna mtu alitaka kumuua Magufuli ili mfano wako uwe relevant? Kaini alikuwa mtoto mkubwa, (Magufuli Rais), sasa hapo yeye si ndo Kaini anayetafuna wenzake (Lissu + Mangula)?
Achana nae mwendawazimu Fulani huyu. Kaota huko kakimbilia kuja kuposti ujinga
 
Kuna aliyekutuma uandike haya?
Umefikiri kabla ya kuandika?
Unajua matendo ya mtu ndio yanafanya kupendwa au kuchukiwa?
 
Hero,
Kamwe hawezi kuwa na kibali kwa kusimamia yaliyompata Lissu, Tundu Lissu ndiye mwenye kibali cha Mungu cha kuwa kiongozi wa nchi hii.
 
Hero,
Kamwe hawezi kuwa na kibali kwa kusimamia yaliyompata Lissu, Tundu Lissu ndiye mwenye kibali cha Mungu cha kuwa kiongozi wa nchi hii. Kulingana na haya yafuatayo, TL alijitakia mwenyewe kwa kuwa ni mjinga sana,
Acha ujinga, ulimuona akisimamia upuuzi huo! Hata hivyo yaliyomkuta TL alijitakia mwenyewe!
TL alijitakia mwenyewe kwa kuwa ni mjinga sana, tena ni Mpumbafu mwenye kiburi na majivuno, ndio maana yalimkuta hayo!
Wewe nchi inapambana kujikwamua afu unajitia unajua saana na kuanza kuihujumu nchi na mbaya zaidi unajiweka mwenyewe kwenye 'cross-fire' kwa kujitia ni adui wa serikali ili hali kuna mijamaa inataka kuipaka matope serikali hiyohiyo! Ni mpumbafu tu ndio anaweza sema upumbufu aliokuwa akisema huyo TL...ambao wasioitakia mema serikali walitumia nafasi ili kuonyesha serikali ndio muhusika! Kwa bahati mbaya hawakuwa smart, maana kama ingekuwa ni serikali asingepigwa na blankoo, ni risasi moja tu inatosha kabisa kumuondoa mtu. Na serikali inao wataaramu wa shabaha wabobezi, wala isingekuwa shida! Uhuni mmefanyiana huko huko kwenu nyie mjitathmini tu!
Mithali 10:14 (NEN)
Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.

Mithali 16:18 (NEN)
Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko.

Mithali 21:24 (NEN)
Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake; hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.

Mithali 22:3 (NEN)
Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom