Awe alishiriki au hakushiriki acha aseme na tunamsikiliza na kumwamini pia. Hapa hatuhitaji ushahidi, waliotajwa wapo wamemsikia kama anawazushia wajitokeze wajibu. Kama wako kimya tunamwamini aliyesema hata bila kutoa ushahidi.
Kwani kuwa kwenye Serikali ya Magufuli na hata kama hakusemea yaliyotokea wakati ule, Sheria ipi inayomzuia asizungumze uovu unaendelea kwenye Serikali hii?
Tena bora yeye kajitokeza kusema. Wapo walioshiriki uovu tangu wakati ule mpaka leo wanaendelea. Ndio hao wanaohaha huku na kule kujaribu kufubaza hoja za Polepole.