Mnaomtilia shaka Polepole tusaidieni jambo moja

Mnaomtilia shaka Polepole tusaidieni jambo moja

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,175
Reaction score
48,459
Jee Polepole mambo anayoyasema ni ya kweli au ni uongo? Kama ni uongo ukweli ni upi na una ushahidi upi?

Wakati Polepole alipokuwa kiongozi wa CCM, aliyokuwa anayafanya yalikuwa na baraka za CCM au la. Kama yalikuwa ni mambo yake binafsi CCM waliwahi kumuonya?

Zama za Magufuli mambo maovu yakitendeka na Polepole akiwa kiongozi wa CCM, jee CCM yenyewe iliwahi kukaa kikao na kutoa tamko lolote au maelekezo kwa Serikali kukomesha yaliyokuwa yanatokea?

Leo Polepole anakikosoa chama chake na kwa sehemu usimamizi wa chama chake Kwa Serikali, jee asikilizwe na kuaminiwa au ahojiwe alikuwa wapi zama za Magufuli wakati maovu kama haya yakitokea?

Kama zama za Magufuli kulikuwa kuna uovu, na Sasa Kuna mfanano wa uovu ule ule, jee ni mambo ya Magufuli na Samia ama ndivyo CCM inavyotaka mambo yawe?

Maana kama Magufuli na Samia wote ni CCM na malalamiko dhidi Yao yanafanana, inawezekanaje kuitenga mbali CCM na uovu unaotokea badala yake tuwape watu wawili tu, yaani Magufuli na Samia?

Tatizo la Polepole ni kuusema ukweli ama ni yeye pia kutuhumiwa kuwa ni sehemu ya watenda maovu ila kwa Sasa watendao huo uovu si watu wa upande wake?
 
Mpaka sasa bado hajasema vitu vya maana/vipya na anasema kwa kuvizia huku akiwapa chama chake muda wa jujirudi na anatishia wafanye vitu kadhaa lasivyo utamwaga mchele.

Aanze kumwaga mchele kwanza ndo tutoe tathmini --- tofauti na hapo ni tapeli kama kilivyo chama chake
 
Jee Polepole mambo anayoyasema ni ya kweli au ni uongo? Kama ni uongo ukweli ni upi na una ushahidi upi?

Wakati Polepole alipokuwa kiongozi wa CCM, aliyokuwa anayafanya yalikuwa na baraka za CCM au la. Kama yalikuwa ni mambo yake binafsi CCM waliwahi kumuonya?

Zama za Magufuli mambo maovu yakitendeka na Polepole akiwa kiongozi wa CCM, jee CCM yenyewe iliwahi kukaa kikao na kutoa tamko lolote au maelekezo kwa Serikali kukomesha yaliyokuwa yanatokea?

Leo Polepole anakikosoa chama chake na kwa sehemu usimamizi wa chama chake Kwa Serikali, jee asikilizwe na kuaminiwa au ahojiwe alikuwa wapi zama za Magufuli wakati maovu kama haya yakitokea?

Kama zama za Magufuli kulikuwa kuna uovu, na Sasa Kuna mfanano wa uovu ule ule, jee ni mambo ya Magufuli na Samia ama ndivyo CCM inavyotaka mambo yawe?

Maana kama Magufuli na Samia wote ni CCM na malalamiko dhidi Yao yanafanana, inawezekanaje kuitenga mbali CCM na uovu unaotokea badala yake tuwape watu wawili tu, yaani Magufuli na Samia?

Tatizo la Polepole ni kuusema ukweli ama ni yeye pia kutuhumiwa kuwa ni sehemu ya watenda maovu ila kwa Sasa watendao huo uovu si watu wa upande wake?
Ni heri Polepole anayesema ukweli hadharani hata kama ukweli huo umma unaujua kuliko mijitu mi-pumbavu na mi-binafsi na mi-nafiki ambayo inapiga zumari kwa watawala wa hovyo.

Haijalishi kama anayosema yamesemwa mara nyingi na Chadema au mtu yoyote.

Polepole kajitoa kweli kweli kusema ukweli juu ya watawala kupitia mgongo wa u-CCM lakini ujumbe unafika vizuri sana na umma unamwelewa hata kama amechelewa kusema.

Go on Polepole.
 
Sijui mtandao, sijui polepole, mara nani kapewa mgodi havisadiii kitu...
Polepole mzushi tuu,

twende na NRNE
 
Kabisa... Huyu Lissu alipigwa risasi zama za Magufuli ana kesi ya Uhaini zama za Samia. Sasa hapa tatizo ni watu au mfumo wa CCM ndiyo unaomtesa Lissu?
Polepole anastahili kupongezwa na kutiwa moyo. Amedhubutu kumvalisha paka kengere akiwa ndani ya chama.

Wanachama wangapi ambao wanakerwa na uhuni uliofanyika Januari na kitendo cha Lissu kusingiziwa kesi ya Uhaini??

Wanaompinga Polepole ni wale wananufaika wa utawala huu wa kipuuzi yaani machawa na makunguni
 
Pia Samia alikuwa sehemu ya utawala wa Magufuli kama second in command .

Aliyakalia kimya yote yale maovu bila kujiuzulu na leo hii anaendeleza alipoishia mtangulizi wake .

Mtangulizi wake aliwafyeka kina Saanane, Azori. Lwajabe yeye amewafyeka kina Kibao , Mdude, Chaula n.k

Hivyo Polepole walau ameonyesha kujitoa kwa kujiuzulu na mimi nataka ayaseme yote pia aliyowahi kuyafanya maana nae alikuwa sehemu ya tatizo ila inaonekana kaiona nuru kaamua kuachana na giza.
 
Mambo anayoyaongea ni mepesi ambayo tayari yalishaongelewa na vyama vingine vya upinzani na wanaharakati tena kwa kina zaidi,,kama itakua sio drama ya kuwapotezea watu muelekeo basi atakuwa anaisaidia CCM bila kujua...
 
Ukweli ni kwamba ni mfumo mbovu unaleta hayo matatizo yote, badala ya kupigania CCM , tupambane kubadilisha mfumo

Polepole anapambania CCM,
(NRNE)
Hoja hapa ni mgodi wa makaa ya mawe. Tueleze ukweli wako nani sasa hivi anamiliki????
 
Aongee tu ili Ni Reforms ianzie huko huko kwao, hiyo inaitwa uisyempenda kaja mpka mlangoni
 
Mambo anayoyaongea ni mepesi ambayo tayari yalishaongelewa na vyama vingine vya upinzani na wanaharakati tena kwa kina zaidi,,kama itakua sio drama ya kuwapotezea watu muelekeo basi atakuwa anaisaidia CCM bila kujua...
Sawa, tueleze wewe mazito ili tulinganishe yako na ya Polepole.
 
Back
Top Bottom