Mnaombeza JPM mkumbuke mlikotoka.

Watu ndio sisi sisi. Tukimpata rais msukuma sawa, tukimpata mmasai sawa. Tukimpata msambaa kama januari hata kiswahili anaongea kama mzungu ndio tutasema sawa?
 
wengine nao waambiwe tu wamepost..
Nyerere ndie aliekua na uzalendo kwa wananchi..
mwengine anajisikia tu uishi maisha magumu ndio raha yake..
ndio maana wengine wake zao wamejaa ngeu na kutabasamu walishasahau..
eti napenda waishi kama shetani..
duh
 
Kuna Mwandishi mmoja wa nje (jina na chombo nimesahahu), miaka ya mwishoni mwa 90 alitusifu watanzania kwa utulivu na amani baada ya kudai kuwa eti nchi ilikaa bila Rais kwa miaka 10 lakini ikabaki salama. Alishukiwa kama mwewe
..........ndo historia yetu?
 
Tatizo liko wapi, yeye anaona hivyo
 
Kuna mtu amediriki kumlinganusha JPM mwenye PhD na Mbowe anayesemekana kupata Division Zero Form six.
 
Juzi JK alisema kuwa ana raha kupumzika. alisema kuwa maisha yake ya sasa ni ya raha tu kwani hasomi tena mafaili.
Alisema huwa anafanya kazi nyingi za kimataifa.
Kusema hivi ni kumaainisha kuwa kazi ya urais ni kubwa.
Mimi naona kuwa kuna mengi allifanya na kupigiwa mfano kuna pia aliyotetereka lakini kusema hatukuwa rais ni joke kwa kweli. Tumwache apumzike
 
nimesema sishangai na wewe ni graduate wa UDOM aliyoijenga huyo unayemtukana. sisi tuliozaliwa zamani kidogo na tuliosoma hapo kabla tunajua ilivyokuwa ngumu karibia kwa kila kitu. mfano, kwenda sekondari ilikuwa ni kitu cha kufikirika na pengine hakiwezekani kwa baadhi ya jamii. kusafiri ilikuwa ni shida ndani ya nchi maana kuna kipindi ilibidi upange siku 2 kufika huko uendako ndani ya jamhuri hii. usifikiri tunamsifia Kikwete bure, tunaona na kufaidi aliyoyafanya. (yeye kama binadamu hakosi mapungufu mfano ni hilo la ukusanyaji wa kodi, lakini huyo jamaa kafanya vizuri sana kuliko watangulizi wake wote 3). miaka michache sana baadaye njoo usome ulichoandika. maana hapo ndo uelewa wako ulipoishia.
 
angalau wewe umeandika kitu kinachoeleweka kidogo. tatizo la Kikwete lilikuwa kwenye kusimamia ukusanyaji wa kodi na kuweka nidhamu kwenye utumishi basi. mengine kafanya vizuri sana. mfano miundombinu ya barabara, mashule, mavyuo, mahosipitali, maji, umeme, utawala bora na mwengine mengi. jamaa kajitahidi sana. nawashangaa wanaojifanya vipofu wakati wao ndo wafaidika wakubwa.
kuhusu Magufuli ni mapema sana kumhukumu kwani ndo kwanza ana miezi michache tu tangia akalie ofisi. tumpe nafasi. akijipanga vizuri naye anaweza fanya vizuri au hata vizuri zaidi ya watangulizi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…