MNAOJUA NISAIDIENI MAANA YA HILI NENO KWENYE DAWA!!!

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
724
551
Mimi nimesumbuliwa sana na Taifodi kwa mwaka sasa.Sasa nimeelekezwa kutumia dawa fulani na rafiki yangu kuwa naye ilimsaidia.Dawa inaitwa RIJAAL.Dawa hii imeandikwa kuwa ni ya kisuna,naomba mwenye kujua tafsiri ya maneno ni ''ya kisuna anisaidie'' ili nielewe tafadhali!!!
 
Hiyo ni dawa ya kienyeji(local) aliekupa ndie pekee mwenye uelewa na dawa hiyo.Kila mganga wa kienyeji anaijua dawa yake.
 
Aliyenipa hafahamu maana yake naye ni mtumiaji tu!!!
 
Sunna na rijaal kwenye dawa ya typhoid??? Mmh ok ngoja waje tutapata majibu
 
Hakikisha unakwenda hospitali usitumie dawa bila maelekezo ya daktari baada ya kukupima maradhi yanayokusmbua
 
Mimi nimesumbuliwa sana na Taifodi kwa mwaka sasa.Sasa nimeelekezwa kutumia dawa fulani na rafiki yangu kuwa naye ilimsaidia.Dawa inaitwa RIJAAL.Dawa hii imeandikwa kuwa ni ya kisuna,naomba mwenye kujua tafsiri ya maneno ni ''ya kisuna anisaidie'' ili nielewe tafadhali!!!

Kunywa kwanza Mkuu kama ikitokea umezidiwa nayo ndiyo tutajitahidi kukijua hicho ' Kisuna ' chako unachokisema.
 
Mimi ntakupa maana lakini kila nikitizama hayo majina na tatizo lako naona haviendani! Hivo nakushauri kuwaona madaktari bingwa maana typhod mwaka mzima si kawaida hiyo.
Kwanza nikianza na jina LA dawa RIJAAL..moja kwa moja linaakisi matatizo ya wanaume na ndio maana ya neno rijaal (wanaume), hivo tulitarajia dawa hii ideal na maswala ya nguvu za kiume na mfano wake sasa ukisema typhoid napata ukakasi any way tuchukulie ni jina tu...ni nini maana ya kisuna? Kwa kukurahisisha uelewa dawa ya kisuna ni dawa ambayo ina mchanganyiko wa dawa za asili kutoka uarabuni..mfano habbat soda, habbat sufa,kamun aswad n.k
 
Mimi nimesumbuliwa sana na Taifodi kwa mwaka sasa.Sasa nimeelekezwa kutumia dawa fulani na rafiki yangu kuwa naye ilimsaidia.Dawa inaitwa RIJAAL.Dawa hii imeandikwa kuwa ni ya kisuna,naomba mwenye kujua tafsiri ya maneno ni ''ya kisuna anisaidie'' ili nielewe tafadhali!!!

Tiba za kisunna maana yake ni ujuzi na utambuzi wa aina mbalimbali za miti vyakura matunda nk
ambavyo vina uwezo wa kutibu maradhi mbarimbari katika mwili wa binadamu pamoja na ujuzi wa kutambua maradhi yanayowasumbua mwanadanu na namna ya kutibu kwa kutumia madawa yaliotajwa ndani ya Qurani na hadithi za mtume MUHAMMAD (swallahu alayhi wa sallamu)
na swahaba zake(Radhiya Allaahu 'anhum).
Mfano asali imetajwa ndani ya Qurani kama chakura bora kuliko chochote na maziwa yametajwa ni kinywaji bora kuliko wakati habbat saudaa yenyewe imetajwa ndani ya hadithi.
Elimu na ujuzi wa tabibu kuhusu tiba za kisunnah ni jambo la kitaaruma kwa maana haiwezekani mtu akawa tabibu bila ya elimu au fani ya tiba ya kutabibu binadamu
Hapa inamaana sio kila muislamu ni mtaalamu wa tiba za kisunna vivo hivyo si kila imamu au ustadhi wa madrasa ni mtabibu na mjuzi wa tiba za kisunnah lah ! Ni kwa wale wachache walojaliwa karama ya utabibu au walofundishwa au kurithishwa ujuzi huo
Na kwakuwa waislamu sisi ni ndugu na tunaaminiana hasa kwa neno lililotoka katika QURAN na Sunnah(hadithi) hivyo ikiwa imetokea moja akapatwa maradhi fulani na akatibiwa na dawa fulani akapona na akatokea mmoja mwingne akapatwa na maradhi ya kufanana na hayo basi hubashiriana kuwa tumia dawa fulani ya kisunna 7bu mimi pia nilisumbuliwa kama hivyo nikapona basi hicho ndicho kilichotokea kwako
MWENYEZI MUNGU anasema katika SURAT AL ISRAA aya ya 81 "Na tunateremsha katika Qur-aan yaliyo ni matibabu na Rehma kwa Waumini"

Muhimu ni kuwa na IMANI na Uzingatiaji wa maelekezo ya tabibu ama uliponunua hiyo dawa au aliyekupa hiyo dawa ni muhimu kwa kufanikisha kupona kwako
Na la mwisho kila unapokunywa hiyo dawa tia nia ikupatie ahueni na umuombe MWENYEZIMUNGU akufanyie wepesi ikutibu maradhi yako
Namimi nina imani na ninakuombea kwa ALLAH (muweza wa yote) utakapotumia hiyo dawa atakufanyia wepesi maradhi yako na utapata SHUFAA
 
Hiyo Typhoid fever unapima wapi??
 
ASANTE NIMEKUELEWA!!!!!
 
Back
Top Bottom