MH,,SISI TUMEJIUNGA TOKA JULY HADI LEO HII BADO PROCESS ZINAENDELEA KWAKWELI KWNY PESA SIO KITU RAHISI KUPATA HASA HII MIKOPO YA SERIKALI INA PROCESS SAANA,DI[QUOTE="Matendo Andrew, post: 33579339, member: 218321"
Umewahi kusikia fedha za mkopo za Halmashauri zile zinazokopeshwa bila riba?
Mambo muhimu:
1.Unda kikundi cha vijana, wakina mama au walemavu. Kuanzia watu watano na kuendelea
2. Andaa katiba yenu na muisajili Halmashauri.
3. Procedure nyingine ndogo ndogo kisha mnaomba mkopo. Japo kuna viwango maalumu vya kuanza kukopa mfano mtu mmoja anaanza kupewa 600,000/ kwa mwaka baada ya hapo utaomba zaidi. Ila ukiwa umechangamka unaweza kupata zaidi.
Jambo muhimu zaidi: Uwe na biashara hata kama sio wote angalau Mwenyekiti wa kikundi awe mtu active na mwenye kuweza kusimamia wenzie (Ndio mdhamini mkuu wa kikundi)
Ziada lakini muhimu: Najua wengi mtaona mzunguuko lakini nani anaweza kukupa hela bila masharti yeyote? Naweza kuwaongoza kila hatua ukiwa unahitaji.
(siri)
Unaweza kuunda kikundi ukachukua mkopo utautumia wewe peke yako ila zingatia maelekezo nitakayo kupatia. Marejesho ndio msingi wa kufanikiwa kwako.