Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
Tatizo hili ni kwa wanaume mpaka wanawake, wazee kwa vijana. Kuna watu wanakula mchana utadhani hana uhakika wa kula baadaye. Kula kula kula ndo mavitambi hayo!
Mazoezi jamani kwa mji wa Dar yataka moyo. Wengi watu wa kawaida hawawezi kuweka mashine za mazoezi nyumbani. Una chumba kimoja nyumba imejaa ndi hata pa kuruka kamba hakuna. Uswazi mashimo barabarani!
Tabu nyingine foleni ukitoka kazini saa 11 unafika nyumbani saa mbili usiku na unalala unaondoka saa 11 asubuhi. Mazoezi tunayoyazungumzia jamani ni yepi? Na msiseme ya kufanyia chumbani.
Uduni na umasikini wa ki TZ na mazoezi wengi hawawezi. Jamaa mmoja aliamua ku jog mtaani kwako. Barabara mashimoooo. Si akaingia kwenye shimo alianguka na kitambi chake pwaaaa. Zaidi ya hayo MOI wakampokea na kumpa POP. Hajarudia!
Cha muhimu-watch your diet!
Mkuu. Lakini si kuna mwisho wa juma? Tumia mwisho wa juma kufanya mazoezi hata kwa saa 1 kwa siku. Inasaidia sana.
Pia hata siku za kazi unaweza kubadili mienendo kidogo. Punguza kutumia chombo cha usafiri kwa eneo ambalo unaweza kutembea kwa miguu. Pia tumia ngazi badala ya escalators.
Hayo pia uendana na lishe yenye kuzingatia virutubisho muhimu tu kwa mwili.