Mnalichukuliaje hili la mzazi kukopa kwenye VICOBA alafu anashindwa kulipa

Mnalichukuliaje hili la mzazi kukopa kwenye VICOBA alafu anashindwa kulipa

mzazi anaenda kukopa huko kwenye vicoba na taasisi uchwara bila hata ya kuwashirikisha watoto, matokeo yake anashindwa kulipa ,mzigo wote wa deni watoto ndio wanaambiwa walipe. hii mnaichukuliaje wakuu. kwangu mimi naona ni ufara na kutojitambua kwa mzazi husika.
Changamoto zipo hizo mzee,Hujui kakutana na Nini.
Hao unaowasema hajawashirikisha ukute amewaambia Mara kadhaa wamsaidie wakiwemo watoto lakini walikataa ukute.
 
Hilo tunalichukulia kawaida tu. Tena bora mzazi, kuna madeni mengi watu wanayalipa/wamelipa ambayo wamekopa mademu zao na bado wakaachwa na hao mademu. Mzazi mlipie tu ila kaa naye chini ongea naye taratibu kuhusu ubaya wa kukopa bila kuwa na uhakika wa kipato cha kulipa.
 
mzazi anaenda kukopa huko kwenye vicoba na taasisi uchwara bila hata ya kuwashirikisha watoto, matokeo yake anashindwa kulipa ,mzigo wote wa deni watoto ndio wanaambiwa walipe. hii mnaichukuliaje wakuu. kwangu mimi naona ni ufara na kutojitambua kwa mzazi husika.
Ikijirudia rudia acha ujinga,.mwache na madeni yake. Maana wanaomkopesha wanaona hawezi kulipa. Wasikusumbue. Wakati mwingine shetani akitaka fedha zako anafungua matobo mengi mengi Ili azichukue.
 
Back
Top Bottom