Kweli kila nyakati na mambo yake, nakumbuka michezo ya maigizo kipindi hicho ilivokuwa ina trend. Enzi za kaole kila jumamosi baada ya taarifa ya habari tu, watu macho kwenye TV, mambo hayo, kidedea, jumba LA dhahabu. Basi enzi hizo mastaa waliokuwa wanatamba kwenye uigizaji wakina Kibakuli, Nyamayao, mashaka, mzee pwagu, mzee kipara, Bishanga, waridi, Nina, Davina, Dr cheni, swebe. Nakumbuka enzi hizo jumamosi ni siku ya marudio ya michezo yote basi mna kwenda kuangalia TV kwa watu, na kama hujaoga huruhusiwi, na ukiingia unakaa chini. Kweli kila nyakati ina mambo yake. Hivi kwanini michezo ya kuigiza imepoteza mvuto kama zamani?. Watoto wa kipindi cha kikwete na magufuli hamuwezi elewa Uzi huu.