Mnada wa TRA wa mtandaoni- Changamoto na maoni yangu

Private-eye

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2013
Posts
1,069
Reaction score
1,211
Wadau wa uchumi wa kati- nawasalimu.

Nianze kwa kutoa pongezi za dhati sana kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuanzisha mnada wa kuuza bidhaa mbalimbali mtandaoni ( Online Auction). Binafsi nimefaidika na huduma hii mara kadhaa. Kwa hakika hii ni moja ya hatua nzuri sana kwa TRA. Pongezi sana kwako Kamishna Mkuu na taasisi yote kwa ujumla.

Hata hvyo siku za karibuni nimeanza kupatwa na mashaka jinsi mnada unavyomalizika.

Kinachonitia mashaka ni muda wa mnada kuisha kabla ya wakati ulioainishwa kwenye mtandao. Mfano tarehe 12/10/2020 mnada ulifungwa dakika moja na sekunde karibu 40 kabla ya muda. Hii si sawa hata kidogo.

Jambo la mnada kuisha dakika moja au sekunde kadhaa kabla ya muda ni suala ambalo nimeliona mara kadhaa sio katika tarehe tajwa pekee.

Kinachotia shaka hapa ni kwamba, kufunga mnada kabla ya muda kunaweza kumaanisha kwamba watu wenye "connection" wanawasiliana na watu wa "IT" ndani ya TRA ambao kwa ujuzi flan flan ama wanazima network au wanasitisha mnada sekunde kadhaa kabla ya muda.....hii inapelekea mtu mwenye "connection" kushinda kabla ya kuisha mnada.....yaani yeye ndio anakuwa mtu wa mwisho wa kuweka dau.

Changamoto hii haikuwapo wakati mnada huu unaanza desemba mwaka jana. Kipindi cha nyuma mnada ulikuwa ukisemwa unaisha saa 3 kamili basi ni saa 3 kamili...sio kasoro wala nini.

Hii binafsi inanipa mashaka na pengine ni kiashiria cha janjajanja ndani ya mfumo wa mnada. Lakini pengine kuna maelezo ya kiufundi....ambayo yanaweza kuondoa mashaka haya.

Binafsi napendekeza Commission General TRA atupie jicho eneo hili. Tuwekane sawa. Fursa iwe sawa kwelikweli.

Changamoto ingine....ni swala la invoice za mtandaoni kukosa control number ya malipo. Yaani ukishinda mnada unaprint invoice unakwenda TRA- wao ndio wakupe control number. Nadhan timu ya ufundi TRA ilitizame hili jambo, invoice itoke ikiwa kamilifu ili mambo yaende kidigital kweli kweli.

Changamoto ingine ni swala la magari haya kuuzwa kabla ya kuwa na kibali cha ubora kutoka TBS. Yaani unanunua gari unalipa kila kitu kisha unaenda TBS walikague kama linafaa kuingia au kutumika nchini.

Hili swala la ukaguzi maanake ni kwamba kuna uwezekano ukanunua gari mnadani kisha TBS/NIT wakasema halifai kutumika TZ ikapelekea mteja kupata hasara.

Napendekeza kwamba, NIT/TBS wakakague mali zote zinazouzwa kisha gharama zao za ukaguzi zijumuishwe kwenye bei ya mnada....ili kuepuasha uwezekano wa mteja kupata hasara ikiwa mali aliyonunua haifai kutumika nchini.

Changamoto ingine....ambayo sijui ni ya TRA au TPA au nani. Ni swala la upigaji picha wa mali zinazouzwa hasa magari.

Kuna nyakati unaona picha hata unashangaa kama mpiga picha alikuwa ana nia ya kupiga picha au lah!!. Yaan picha zote zinaonesha eneo moja tu la gari.....ama matairi tu au pengine mbele tu nk.

Hili la picha linaambatana na taarifa zisizotosha kuhusu gari au kifaa kinachouzwa....mfano unakuta gari inauzwa ila haioneshi ni manual au auto, aina ya mafuta inayotumia, eneo ambalo gari ipo, ukubwa wa injin n.k. Nadhan hizi ni taarifa muhimu sana kwa mnunuzi. Tunaomba improvement eneo hili.

Changamoto nyingine ambayo nimeiona....ni swala la namna ya kumruhusu mtu mwingine (third party) kuchukua mali uliyokwisha kulipia kwa niaba yako.

Mfano nimeshinda na kulipia mali iliyoko Bukoba nami niko Mtwara....natumia utaratibu gan ili mtu mwingine aweze kuchukua hiyo mali kwa niaba yangu?

Nadhan hili haliko wazi sana....napendekeza liwekwe bayana sana ili tuweze kununua na mali popote TZ bila kulazimika kwenda kufanya clearence sisi binafsi.

Changamoto nyingine ya ziada ambayo sio ya TRA kama taasisi ....nadhan ni ya mtu binafsi, ni kuhusu utaratibu wa kukagua magari na bidhaa pale yard ya ubungo.

Pale ubungo...pana mlinzi anaitwa Wambura....huyu bwana ni mnyanyasaji wa wateja sana. Amejaa kiburi na kisirani sana. Yaani ukienda pale kukagua mali zinazouzwa hadi uruhusiwe ni shida sana.

Tunabembeleza sana kupata ruhusa ya kuingia yard ...kiasi kwamba inakuwa ni kama msaada kukagua mali wakati kanuni za mnada zinaruhusu kukagua mali kabla ya kununua.

Napendekeza kwamba huyu bwana ama afundishwe namna bora ya kuhudumia wateja au abadilishwe apelekwe eneo ambalo si lazima kukutana na wateja. Pia pawekwe ratiba maalumu ieleweke ni muda gani wateja wanaruhusiwa kuja kukagua mali badala ya kutegemea hekima ya walinzi.

Namaliza kwa kusema, licha ya changamoto zote tajwa hapo juu, bado mnada huu wa online ni bora mara 1000 zaidi ya kile kilichokuwa kinafanyika zamani.....kwa hili nawapa kongole sana.

Pamoja katika uchumi wa kati.

Asante

UPDATE:

Wanajukwaa ....nawasalamia !

Naomba kuchukua fursa hii kutoa mrejesho wa baadhi ya changamoto nilizozitoa wiki kadhaa kuhusu mnada wa TRA.

Nawapongeza sana TRA kwa kushughulikia maswala haya muhimu:

1. Hongera TRA kwa kuhakikisha kuwa control number zinatoka moja kwa moja kwenye hati ya malipo. Haya ni mafanikio makubwa sana.

Hapa mmeondoa adha ya msingi sana....iliyomtaka mnunuzi afike ofis za TRA kupata control number......hongera sana....!

2. Nimefarijika sana na mabadiliko aliyonayo bwana wambura pale yard ya ubungo. Amejirekebisha sana.....huduma yake kwa sasa ni bora mara 10 zaidi ya hapo zamani. Nina iman kwamba ataendelea kuwa na weledi huo kadri siku zonavyosonga.

Kwa sasa huu ndo uzoefu wangu mpya.....nikaona si vibaya kupongeza pale kero zinapotatuliwa.

Asante.
 
Huyu bwana kwakweli ni shida. Imefika mahala tunafatilia ratiba zake binafsi....tukijua leo ndo yuko zamu wala hatupotezi muda kwenda ubungo kunyanyasika. Tunasubiri siku hayuko zamu.

Ana boa sana huyu mdau..... anazidiwa hata na attendant wa mochuari.
Wambura kuanzia kesho uripoti kwenye kituo cha mwendokasi baruti itakua ndio kituo chako kipya cha kazi
 
Umechambua vizuri sana.
Ungetupia hiyo link ya mnada kabisa tuchungulie
 
Hapo kwenye suala la mnada kuisha kabla ya muda stahiki kuna dalili kubwa ya upigaji uliokusudiwa.

Na suala la Mali kuuzwa kabla ya TBS/ NIT kukagua si ni kiashiria kwamba huu mnada at first place ni janja janja, yaani mwenye kupata apate mwenye kupigwa apigwe sababu sidhani kama watarudisha pesa baada ya mteja kujibiwa na TBS kuwa mali husika haifai.

Kimsingi project au taratibu nyingi za serikali huwa na kusudi jema kabisa awali zinapoanzishwa, Ila muda unaposogea kuna watendaji wanaanza kuingiwa na tamaa kisha huanza kuhujumu mpango mzima.
 
Huyu bwana kwakweli ni shida. Imefika mahala tunafatilia ratiba zake binafsi....tukijua leo ndo yuko zamu wala hatupotezi muda kwenda ubungo kunyanyasika. Tunasubiri siku hayuko zamu.

Ana boa sana huyu mdau..... anazidiwa hata na attendant wa mochuari.
Ila majina ya Wambura hua ni wa dizaini hio,nawajua kama watatu hivi ni wazinguaji wazinguaji tu.
 
Mkuu maoni haya ungefanya namna inayowezekana kuyafikisha kwa Waziri,Kamishna tra,waziri mkuu na hata jpm yangeleta tija, maana yakiishia jF tu yanabaki kuwa 'POVU' tu
 
Wadau wa uchumi wa kati- nawasalimu.

Nianze kwa kutoa pongezi za dhati sana kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuanzisha mnada wa kuuza bidhaa mbalimbali mtandaoni ( Online Auction). Binafsi nimefaidika na huduma hii mara kadhaa. Kwa hakika hii ni moja ya hatua nzuri sana kwa TRA. Pongezi sana kwako Kamishna Mkuu na taasisi yote kwa ujumla.

Hata hvyo siku za karibuni nimeanza kupatwa na mashaka jinsi mnada unavyomalizika.

Kinachonitia mashaka ni muda wa mnada kuisha kabla ya wakati ulioainishwa kwenye mtandao. Mfano tarehe 12/10/2020 mnada ulifungwa dakika moja na sekunde karibu 40 kabla ya muda. Hii si sawa hata kidogo.

Jambo la mnada kuisha dakika moja au sekunde kadhaa kabla ya muda ni suala ambalo nimeliona mara kadhaa sio katika tarehe tajwa pekee.

Kinachotia shaka hapa ni kwamba, kufunga mnada kabla ya muda kunaweza kumaanisha kwamba watu wenye "connection" wanawasiliana na watu wa "IT" ndani ya TRA ambao kwa ujuzi flan flan ama wanazima network au wanasitisha mnada sekunde kadhaa kabla ya muda.....hii inapelekea mtu mwenye "connection" kushinda kabla ya kuisha mnada.....yaani yeye ndio anakuwa mtu wa mwisho wa kuweka dau.

Changamoto hii haikuwapo wakati mnada huu unaanza desemba mwaka jana. Kipindi cha nyuma mnada ulikuwa ukisemwa unaisha saa 3 kamili basi ni saa 3 kamili...sio kasoro wala nini.

Hii binafsi inanipa mashaka na pengine ni kiashiria cha janjajanja ndani ya mfumo wa mnada. Lakini pengine kuna maelezo ya kiufundi....ambayo yanaweza kuondoa mashaka haya.

Binafsi napendekeza Commission General TRA atupie jicho eneo hili. Tuwekane sawa. Fursa iwe sawa kwelikweli.

Changamoto ingine....ni swala la invoice za mtandaoni kukosa control number ya malipo. Yaani ukishinda mnada unaprint invoice unakwenda TRA- wao ndio wakupe control number. Nadhan timu ya ufundi TRA ilitizame hili jambo, invoice itoke ikiwa kamilifu ili mambo yaende kidigital kweli kweli.

Changamoto ingine ni swala la magari haya kuuzwa kabla ya kuwa na kibali cha ubora kutoka TBS. Yaani unanunua gari unalipa kila kitu kisha unaenda TBS walikague kama linafaa kuingia au kutumika nchini.

Hili swala la ukaguzi maanake ni kwamba kuna uwezekano ukanunua gari mnadani kisha TBS/NIT wakasema halifai kutumika TZ ikapelekea mteja kupata hasara.

Napendekeza kwamba, NIT/TBS wakakague mali zote zinazouzwa kisha gharama zao za ukaguzi zijumuishwe kwenye bei ya mnada....ili kuepuasha uwezekano wa mteja kupata hasara ikiwa mali aliyonunua haifai kutumika nchini.

Changamoto ingine....ambayo sijui ni ya TRA au TPA au nani. Ni swala la upigaji picha wa mali zinazouzwa hasa magari.

Kuna nyakati unaona picha hata unashangaa kama mpiga picha alikuwa ana nia ya kupiga picha au lah!!. Yaan picha zote zinaonesha eneo moja tu la gari.....ama matairi tu au pengine mbele tu nk.

Hili la picha linaambatana na taarifa zisizotosha kuhusu gari au kifaa kinachouzwa....mfano unakuta gari inauzwa ila haioneshi ni manual au auto, aina ya mafuta inayotumia, eneo ambalo gari ipo, ukubwa wa injin n.k. Nadhan hizi ni taarifa muhimu sana kwa mnunuzi. Tunaomba improvement eneo hili.

Changamoto nyingine ambayo nimeiona....ni swala la namna ya kumruhusu mtu mwingine (third party) kuchukua mali uliyokwisha kulipia kwa niaba yako.

Mfano nimeshinda na kulipia mali iliyoko Bukoba nami niko Mtwara....natumia utaratibu gan ili mtu mwingine aweze kuchukua hiyo mali kwa niaba yangu?

Nadhan hili haliko wazi sana....napendekeza liwekwe bayana sana ili tuweze kununua na mali popote TZ bila kulazimika kwenda kufanya clearence sisi binafsi.

Changamoto nyingine ya ziada ambayo sio ya TRA kama taasisi ....nadhan ni ya mtu binafsi, ni kuhusu utaratibu wa kukagua magari na bidhaa pale yard ya ubungo.

Pale ubungo...pana mlinzi anaitwa Wambura....huyu bwana ni mnyanyasaji wa wateja sana. Amejaa kiburi na kisirani sana. Yaani ukienda pale kukagua mali zinazouzwa hadi uruhusiwe ni shida sana.

Tunabembeleza sana kupata ruhusa ya kuingia yard ...kiasi kwamba inakuwa ni kama msaada kukagua mali wakati kanuni za mnada zinaruhusu kukagua mali kabla ya kununua.

Napendekeza kwamba huyu bwana ama afundishwe namna bora ya kuhudumia wateja au abadilishwe apelekwe eneo ambalo si lazima kukutana na wateja. Pia pawekwe ratiba maalumu ieleweke ni muda gani wateja wanaruhusiwa kuja kukagua mali badala ya kutegemea hekima ya walinzi.

Namaliza kwa kusema, licha ya changamoto zote tajwa hapo juu, bado mnada huu wa online ni bora mara 1000 zaidi ya kile kilichokuwa kinafanyika zamani.....kwa hili nawapa kongole sana.

Pamoja katika uchumi wa kati.

Asante
Hayo magari takataka wanayouza kweli unategemea yatafika viwango vya NIT?
 
Asante sana.....! Wazo zuri!
Mkuu maoni haya ungefanya namna inayowezekana kuyafikisha kwa Waziri,Kamishna tra,waziri mkuu na hata jpm yangeleta tija, maana yakiishia jF tu yanabaki kuwa 'POVU' tu
 
Kiongozi,

Yapo magari takataka na yapo magari mazuri na mapya kabsa....muhimu ni kwamba TBS/NIT wafanye thathimini kabla hayajaingia mnadani. Yasiyofaa basi yaende kuzimu moja kwa moja.
Sijaona gari zuri/jipya hata moja kwenye auction list, hebu weka picha
 
Yashauzwa mengi tu mapya...sina picha zake kwa sasa kwa sababu sikuzichukua.

Palikuwa na haya mapya kabsa...kwa maana ya used ya nje

1. Subaru foresta
2. Range rover
3. Pajero
4. Hyundai
5. Bmw.

Hizi baadhi ya gari zilizokuwapo quality na bei nzuri sana.

Over...out.!
 
Wadau wa uchumi wa kati- nawasalimu.

Nianze kwa kutoa pongezi za dhati sana kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuanzisha mnada wa kuuza bidhaa mbalimbali mtandaoni ( Online Auction). Binafsi nimefaidika na huduma hii mara kadhaa. Kwa hakika hii ni moja ya hatua nzuri sana kwa TRA. Pongezi sana kwako Kamishna Mkuu na taasisi yote kwa ujumla.

Hata hvyo siku za karibuni nimeanza kupatwa na mashaka jinsi mnada unavyomalizika.

Kinachonitia mashaka ni muda wa mnada kuisha kabla ya wakati ulioainishwa kwenye mtandao. Mfano tarehe 12/10/2020 mnada ulifungwa dakika moja na sekunde karibu 40 kabla ya muda. Hii si sawa hata kidogo.

Jambo la mnada kuisha dakika moja au sekunde kadhaa kabla ya muda ni suala ambalo nimeliona mara kadhaa sio katika tarehe tajwa pekee.

Kinachotia shaka hapa ni kwamba, kufunga mnada kabla ya muda kunaweza kumaanisha kwamba watu wenye "connection" wanawasiliana na watu wa "IT" ndani ya TRA ambao kwa ujuzi flan flan ama wanazima network au wanasitisha mnada sekunde kadhaa kabla ya muda.....hii inapelekea mtu mwenye "connection" kushinda kabla ya kuisha mnada.....yaani yeye ndio anakuwa mtu wa mwisho wa kuweka dau.

Changamoto hii haikuwapo wakati mnada huu unaanza desemba mwaka jana. Kipindi cha nyuma mnada ulikuwa ukisemwa unaisha saa 3 kamili basi ni saa 3 kamili...sio kasoro wala nini.

Hii binafsi inanipa mashaka na pengine ni kiashiria cha janjajanja ndani ya mfumo wa mnada. Lakini pengine kuna maelezo ya kiufundi....ambayo yanaweza kuondoa mashaka haya.

Binafsi napendekeza Commission General TRA atupie jicho eneo hili. Tuwekane sawa. Fursa iwe sawa kwelikweli.

Changamoto ingine....ni swala la invoice za mtandaoni kukosa control number ya malipo. Yaani ukishinda mnada unaprint invoice unakwenda TRA- wao ndio wakupe control number. Nadhan timu ya ufundi TRA ilitizame hili jambo, invoice itoke ikiwa kamilifu ili mambo yaende kidigital kweli kweli.

Changamoto ingine ni swala la magari haya kuuzwa kabla ya kuwa na kibali cha ubora kutoka TBS. Yaani unanunua gari unalipa kila kitu kisha unaenda TBS walikague kama linafaa kuingia au kutumika nchini.

Hili swala la ukaguzi maanake ni kwamba kuna uwezekano ukanunua gari mnadani kisha TBS/NIT wakasema halifai kutumika TZ ikapelekea mteja kupata hasara.

Napendekeza kwamba, NIT/TBS wakakague mali zote zinazouzwa kisha gharama zao za ukaguzi zijumuishwe kwenye bei ya mnada....ili kuepuasha uwezekano wa mteja kupata hasara ikiwa mali aliyonunua haifai kutumika nchini.

Changamoto ingine....ambayo sijui ni ya TRA au TPA au nani. Ni swala la upigaji picha wa mali zinazouzwa hasa magari.

Kuna nyakati unaona picha hata unashangaa kama mpiga picha alikuwa ana nia ya kupiga picha au lah!!. Yaan picha zote zinaonesha eneo moja tu la gari.....ama matairi tu au pengine mbele tu nk.

Hili la picha linaambatana na taarifa zisizotosha kuhusu gari au kifaa kinachouzwa....mfano unakuta gari inauzwa ila haioneshi ni manual au auto, aina ya mafuta inayotumia, eneo ambalo gari ipo, ukubwa wa injin n.k. Nadhan hizi ni taarifa muhimu sana kwa mnunuzi. Tunaomba improvement eneo hili.

Changamoto nyingine ambayo nimeiona....ni swala la namna ya kumruhusu mtu mwingine (third party) kuchukua mali uliyokwisha kulipia kwa niaba yako.

Mfano nimeshinda na kulipia mali iliyoko Bukoba nami niko Mtwara....natumia utaratibu gan ili mtu mwingine aweze kuchukua hiyo mali kwa niaba yangu?

Nadhan hili haliko wazi sana....napendekeza liwekwe bayana sana ili tuweze kununua na mali popote TZ bila kulazimika kwenda kufanya clearence sisi binafsi.

Changamoto nyingine ya ziada ambayo sio ya TRA kama taasisi ....nadhan ni ya mtu binafsi, ni kuhusu utaratibu wa kukagua magari na bidhaa pale yard ya ubungo.

Pale ubungo...pana mlinzi anaitwa Wambura....huyu bwana ni mnyanyasaji wa wateja sana. Amejaa kiburi na kisirani sana. Yaani ukienda pale kukagua mali zinazouzwa hadi uruhusiwe ni shida sana.

Tunabembeleza sana kupata ruhusa ya kuingia yard ...kiasi kwamba inakuwa ni kama msaada kukagua mali wakati kanuni za mnada zinaruhusu kukagua mali kabla ya kununua.

Napendekeza kwamba huyu bwana ama afundishwe namna bora ya kuhudumia wateja au abadilishwe apelekwe eneo ambalo si lazima kukutana na wateja. Pia pawekwe ratiba maalumu ieleweke ni muda gani wateja wanaruhusiwa kuja kukagua mali badala ya kutegemea hekima ya walinzi.

Namaliza kwa kusema, licha ya changamoto zote tajwa hapo juu, bado mnada huu wa online ni bora mara 1000 zaidi ya kile kilichokuwa kinafanyika zamani.....kwa hili nawapa kongole sana.

Pamoja katika uchumi wa kati.
Nina maswali kidogo kwako mkuu
1. Yard ya ubungo iko maeneo gani?
2. Magari yanayouzwa ni used kutoka Japan yaliyoshindwa kulipiwa bandarini au hata used bongo yapo ?
3. Kwa hapa Dar yard nyingine ya TRA iko wapi?
Jibu maswali yangu then issue ya Wambura niachie mimi
 
Back
Top Bottom