Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,744
- 5,769
Kabla ya JPM kuingia madarakani mlikuwa kila siku mnapiga kelele kuwa nchi imeoza, ufisadi umetapakaa kila kona na Ccm inaenda kufa. Ilikuwa kila kikao cha bunge lazima usikie kuna ufisadi wa kuutisha mara Epa ,Escrow n.k.
Rais aliyekuwepo najua kwa asilimia kubwa alikuwa hataki haya mambo ndio maana hata yeye alikuwa anaruhusu bunge liisurubishe serikali yake. Mfano ni kwenye kashifa ya Escrow tuliona namna bunge lilivyoisurubu serikali yake. Mpaka azimio la bunge likaundwa ili waliohusika wachukuliwe hatua.
Kuna jamaa zaidi ya miaka kumi na tano walikuwa wanatuibia rasilimali zetu. Amekuja JPM kasimama kidete ili na sisi tuanze kunufaika na mali ambayo Mungu ametupatia .
Sasa najiuliza je mlitaka watu wachache tu wawe wanajichotea mali za umma kama ilivyokuwa hapo zamani? Maana najua yule mzee wa Msoga upole ulizidi ndio maana watu wakawa wanaiibia nchi wanavyotaka. Kila sekta ilikuwa ni wizi tu. Iwe ni vocha za pembejeo,wafanyakazi hewa n.k
Je nyie Chadema ambao sasa hivi mnaponda JPM mlitaka ufisadi uendelee ili mpate sifa za kisiasa? Mbona mnakuwa wanafiki kama wanawake wa saluni?