Hizi ni barua ambazo mara nyingi huwa zinaandikwa na West Africans (mostly Nigerians)! Nimekuwa nikizipata kwenye mfumo wa e-mails! Huwa wanatumia matatizo yanayowapata viongozi wakubwa wa nchi mbali mbali (hasa wanapokuwa wametolewa madarakani kwa kupinduliwa au wanapofariki).
Nakumbuka alipokufa baba yetu wa Taifa nilipata e-mail kama hiyo, akijitambulisha kama Kambarage na ni mtoto wa marehemu baba wa Taifa! Nilichokifanya ni nilimjibu kwa kiswahili (kwa sababu nilikuwa nimeshamgundua), matokeo yake sijajibiwa hadi hii leo tunapokaribia kumbukumbu ya miaka 13! Ni dhahiri hakuelewa kile kiswahili, yaani mtoto wa Nyerere Kambarage asijue kiswahili!
Nashangaa kama hadi leo bado wanatumia mbinu hizo hizo za mwaka 47, wasijue hivi sasa Dunia ni kijiji kidogo sana!
Kuhusu ushauri; mwambie rafikiyo awapuuzie na asiwe na tamaa ya hiyo mihela!