Habari zenu wapendwa,
Si ugomvi mkubwa sana ila umesababisha nimenuniwa, ni hivi baba na mama mkwe wamekuja kututembelea sasa tumewaandalia chumba chao wamelala. Jana usiku wao wakatangulia kulala mie na hubby tukabaki sebleni tunaangalia tv huku unasogoa. Tulipoamua kwenda kulala muda ulikuwa umesonga tukapita wote wenye korido kwa kuwa usiku ulikuwa umeenda kulikuwa kimyaa mno tukasikia (wote) sauti kutoka chuma walicholala baba na mama mkwe za mahabat yaani walikuwa wanapeana haki ya ndoa. Sasa tulistuka kidogo tulipoelewa sauti ni za nini tukaingia room kulala. Nusu saa baadae hubby akaanza daah mzee bana sasa ndo nini ugenini anaamua kuaibisha, mie nikacheka kicheko cha kupasuka mbavu hee!!kumbe mwenzangu kachukia. Ndo nimenuniwa tangu jana kisa nimewacheka wazee wake, jamani kwani walichofanya wakwe zangu ni dhambi? halafu pia nikajiuliza hivi kumbe hii kitu, hii kitu hii kitu hii,hii kitu haina mwisho eeehh!!! daahh!! maana wakwe zangu wote washastaafu wako between 65-70 yrs. Na pia hivi mkiwa mtu na mkewe mmeenda nyumbani kwa mtu mwingine say ndugu na mtalala hapo kwa siku zaidi ya mbili, kupeana haki ya ndoa ugenini ni sawa au mnatakiwa mvumilie hadi mnaporudi kwenu?? Au wanandoa hao wanatakiwa watengewe vyumba tofauti?? Najiuliza tuu...............
Sasa mie mambo ya kununiana siyapendi maana napenda sana kucheka, nikamtania hubby japo bado kanuna kuwa ukiendelea kununa mie narudi zangu kwa Obama, kanitizama tuu hajanijibu.
Saa ingine nashindwa kuwaelewa wanaume kabisa sjui ni wivuu au alitaka nilie badala ya kuchekaa.............. puzzled!!:A S confused: