Rogart Ngaillo
JF-Expert Member
- Apr 27, 2013
- 908
- 1,911
Mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Magomeni.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya saa 3 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa tayari amefariki.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.
Chanzo : Global Publishers