Mmiliki wa Arsenal anunua shamba la £500m

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Mmiliki wa Arsenal anunua shamba la £500m
160211074822_stan_kroenke_640x360_bbc_nocredit.jpg

Image captionStan Kroenke
Mashabiki wa Arsenal kwa mda mrefu wamelalamika kuhusu kushindwa kwa kilabu hiyo kununua wachezaji wazuri kila dirisha la uhamisho linapokuwa wazi.

Lakini mwana hisa mkuu katika kilabu hiyo Stan Kroenke amenunua shamba kubwa la ng'ombe lililogharimu pauni milioni 500.

Shamba hilo limepitia kaunti sita na Kroenke ambaye ana thamani ya pauni bilioni 5,sasa anamiliki zaidi ya ekari 865,000 za ardhi nchini Marekani,ikiwa ni eneo lililo mara tatu zaidi ya ukubwa wa mji wa Los Angeles,na mara nne na nusu ya ukubwa wa mji wa New York.

160211075154_texas_ranch.jpg

Image captionShamba alilonunua Kroenke mjini Texas
Ni watu wanane pekee wanaomiliki ardhi kubwa zaidi ya Kroenke nchini Marekani.

Chanzo: BBC
 
kuna shida gani kwa mwanahisa kununua kitu? ametumia pesa za club au zake??! arsenal acheni upopompo!
 
Back
Top Bottom