Mmh jamani mke wangu ...

Mmh jamani mke wangu ...

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Habari wana bodi.

Natumai hamjambo?

Naomba munisaidie mi nimeowa toka mwaka 2007 mke wangu alikua mwembamba ( kibasmati ) yaaani sio siri nampenda hadi kesho tatizo ni kua baada ya kujifungua mtoto wa kwanza mwaka 2009 alinenepa kiasi sikichukia sana ila nilimuambia sipendi awe mnene mambo yamezidi mara kumi alipojifungua mtoto wa 2 kawa kibonge mbuno huo tumbo limeengezeka balaa yaani hadi sijui nimfanyeje?

Mwanzoni nilikua nampangia malaji na naibana bajeti ya kula wakati tuko na mtoto 1 tena mchanga ila siku hizi siwezi maana nikibana bajeti nitaumiza watoto.

Nimemueleza kua ajipangie utaratibu na mpangilio wa vyakula lakini wapi hanielewi anaishia kuniambia kua hata alipokua mdogo alikua mnene sana alipungua alipokua mwari.

Mi kwa kweli sipendi mwanamke mnene nifanyeje?
 
Ndoa ni hivo kwa shida na raha...kwani hujui miili yetu wanawake inabadilika baada ya uzazi??unless kama mtu yupo strict sana na mazoezi
 
Kaka tatizo ilo dogo sana..wewe unaweza kuwa doctor wa mke wako ninayo namna yakukusaidi nitafute private kama uko serious 0752629999
 
Usiende nae mikumi kuna majangili hawaangaliagi vizuri kabla ya kufanya maamuzi.
 
aisee hiyo changamoto

mnunulie kifaa cha mazoezi weka ndani kama baiskeli alafu unampandisha kwa nguvu
 
Mdau kunenepa si lazima kula japo factor kubwa ni ulaji. Kwa maelezo yaki upendo unaompa mkeo umemfanya akaridhika. Pia kama anatumia vidonge au sindano za majira mwoneni daktari.
 
Kweli tumetofautiana...hupendi vibonge??
 
Sasa kama hutaki mwanamke mnene, si ukaoe mwembamba? Au wanawake wembamba wameisha? Usiumize kichwa while solution unayo
 
Habari wana bodi.

Natumai hamjambo?

Naomba munisaidie mi nimeowa toka mwaka 2007 mke wangu alikua mwembamba ( kibasmati ) yaaani sio siri nampenda hadi kesho tatizo ni kua baada ya kujifungua mtoto wa kwanza mwaka 2009 alinenepa kiasi sikichukia sana ila nilimuambia sipendi awe mnene mambo yamezidi mara kumi alipojifungua mtoto wa 2 kawa kibonge mbuno huo tumbo limeengezeka balaa yaani hadi sijui nimfanyeje?

Mwanzoni nilikua nampangia malaji na naibana bajeti ya kula wakati tuko na mtoto 1 tena mchanga ila siku hizi siwezi maana nikibana bajeti nitaumiza watoto.

Nimemueleza kua ajipangie utaratibu na mpangilio wa vyakula lakini wapi hanielewi anaishia kuniambia kua hata alipokua mdogo alikua mnene sana alipungua alipokua mwari.

Mi kwa kweli sipendi mwanamke mnene nifanyeje?

Acha kumsimanga mkeo kwa kunenepa,kwani hujui kuwa mwanamke akizaa anaongezeka?
 
Ongea nae kwa upole na upendo mkubwa sana ni jinsi gani hiyo hali ya mwili wake huifurahii na kwamba ungependa sana apungue kwani bila hivyo ita athiri ndoa yenu, akishakuelewa mshauri afanye diet na kama uwezo unaruhusu aanze kwenda gym, lakini sio kumwambia kwa ukali na msikhara hutaleta mabadiliko namna hiyo
 
Mimi napenda mke wangu anenepeane imeshindikana kwa namna yoyote!
Nampatia kila kitu nionacho chaweza kumsaidia lakini wapi,
Nakushangaa unavyolalamika.
 
Back
Top Bottom