Mme hataki kuishi na mke aliebakwa ,....

Kisoda2

JF-Expert Member
May 30, 2008
2,475
745
Huko mashariki ya Congo (DRC) wanaume hawataki kuwarudia wake zao waliobakwa na waasi.
Sababu ya mwanamke kubakwa ni kwamba alimficha mume wake asiuwawe na waasi,ndo akaipata hiyo kama adhabu.

Je, wadau hii imekaaje??
 
1.mwanamme anafanya kosa kumuacha mkewe,ni ukatili mkubwa sana.
2. Inatakiwa amtibu na kwenda kumpima ili aone kama kaambukizwa au la
3.baada ya hapo wataamua waishi vipi.
4.kumbuka kwenye maisha kuna tabu na raha,utajiri na umaskini,dhiki na faraja.
5.kifo ndicho kitakachowatenganisha.
 
huko mashariki ya congo (drc) wanaume hawataki kuwarudia wake zao waliobakwa na waasi.
Sababu ya mwanamke kubakwa ni kwamba alimficha mume wake asiuwawe na waasi,ndo akaipata hiyo kama adhabu.

Je, wadau hii imekaaje??

je kama maaskari wangeamua kumlawiti/kumla tigo mbele ya mkewe,mkewe angeamua kumpa talaka mmewe?
 
kuna walokwisha pimwa na kukutwa hawajaambukizwa maradhi yawayo yote ya kujamiana,bado jamaa wanagoma kukaa na mzigo.
 
mwanaume anadhambi jamani pamoja na mkewe kuokoa maisha yake bado hamtaki .iko kazi
 
Well hayo ni matatizo ya serikali ya kongo na wadau wote huko; wamewapa counselling ya kutosha wahanga wote?
 
Good lesson wanawake msijidai kuwa heroines... next time waacheni wauliwe:angry:
 
Back
Top Bottom