Mlipuko wa kipundupindu

Nokiatochi

Member
Joined
Jun 29, 2014
Posts
7
Reaction score
2
Habari wadau,
Kwa kipindi cha miaka ya 2000 tulikuwa tukipewa taarifa mbalimbali juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu. Na mara nyingi ripoti zilikuwa zikitolewa pindi mvua zinapoanza. Kwa Dar taarifa juu ya milipuko zilikuwa sehemu kama Buguruni na maeneo mengine yaliokidhiri uchafu. Mikoani napo pia taarifa zilikuwa zikiripotiwa.
Kwa kipindi hichi cha mvua na uchafu uliokithiri kila kona, je ni kweli hakuna hiyo milipuko ya kipindupindu au kuna chanjo ambazo zimetolewa juu ya ugonjwa huu?
 
huu siyo msimu wa maembe kijana.
 
Kuna uhusiano upi kati ya maembe na kipindupindu jamani?
 
Kuna uhusiano upi kati ya maembe na kipindupindu jamani?

Basi haujafanya utafiti,
Maembe ni matunda yanayooza kwa muda mfupi sana na yanavutia nzi kwa kiwango kikubwa.
Sasa katika msimu wa maembe mvua zinaponyesha ukijumlisha na zile takataka nyingine kama uijuavyo Darslam,
Inakuwa rahisi nzi kuongezeka kutua kwenye matunda na vyakula na mwisho ugonjwa ukianza unasambaa kwa kasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…