Dark Angel
JF-Expert Member
- Sep 12, 2013
- 212
- 220
Raia wanaoingia Angola watapokea chanjo
Mlipuko wa homa ya manjano umewaua watu 21 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani{WHO}, homa hii imetoka katika nchi jirani ya Angola.
Taarifa ya WHO inasema vifo hivyo vilitokea mwezi Machi huku kukiwa na visa vingine 151. Kuna hofu huenda mulipuko huu ukasambaa zaidi. Homa hii ya manjano imewaua watu 225 nchini Angola na kuwaambukiza wengine 1,600.
Homa ya manjano huambukizwa na mbu aina ya (Aedes aegypti)
WHO imeongeza kwamba maafisa wa DRC wameweka vituo vya dharura kushughilikia mulipuko huo.
Aidha raia wanaosafiri nchini Angola watapewa chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Homa hii husababisha kuvuja damu na figo kushindwa kufanya kazi.
Inaambukizwa na aina ya mbu (Aedes aegypti). Maeneo yaliyo kwenye hatari ya Homa ya manjano ni pamoja na Bara Afrika na Amerika Kusini.
Chanzo: BBC