Mliopita Tabora Boys jamani click hapa tushee

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
1,899
3,683
2005 wakat naenda form one niliambiwa Boys ni shule ya kijeshi..
Kidogo nigome kwenda, nafika naambiwa jeshi lilishaondolewa tangu 1997 (jaman wale mliobahatika kulikuta jeshi, maisha yalikuaje, nackia mchakamchaka kila cku mpaka kipalapala)

2006 niko form two tumeenda kuchek mieleka baa ya jeshin cheyo mara second master (Mwl. Masele) na ticha Kamulali haooo....
Wakataka tuandike majina hapo hapo kubabake wanajeshi wakasema :
"walim tokeni hapa, subirini warud shule mmalizane uko uko, hii ni sehem ya starehe "

Form two hiyo hiyo tuliiba jaba la maandaz kanteen kwa mama Mwita tukaenda kulificha mliman pale karib na" Woso "
Bas mida ya uji kila mtu anaenda kujisevia vitafunio, week nzima.

Gradu ya form six 2008 niko form four kengele ya msosi imebani watu bize na disco DH, KUDADADEK tukigawana nyama dish zima mimi na table leader tu (sitosahau)

sitosahau 2005 tulipigwa 2-0 na mwinyi sec golikipa alikua Joshua Samwel Nassari (MP from Arumeru mashariki)

Viboko vya Mwl. Choya kweny practicals za CHEMISTRY 2007 tukiwa form three sitosahau. Nilikosea namna ya kushika bullet flask.

Ticha Barosha aliponikamata ucku natokea Kiloleni ubalozini.
Alinishika ngozi ya tumbo juu juu nikafikia kibao hicho nikaambiwa
"kimbia bwenini, kesho unione "

MBAYA KULIKO ZOTE :
Mazee mpaka nafika form three mwanzon nilikua na tatizo la kukojoa kitandan, Kwa kwel roomate wangu nilikua nawapa mtihan sana, ckua na raha kabisa. Nilikua nakaa bweni la Milambo pale Chamber Squad, mkabala na korido ya kwenda Sina House.

JE NYIE MNA CHOCHOTE CHA KUSHEA WABOZIA??
(mawoso na walambo pia mnaalikwa)
 
M

Mimi ni wa zamani sana pale miaka ya 1970 ndio tupo huko. Nayakumbuka mambo ya Berlin na Warsaw
 
Duuuh! Boys raha sana. Madam Ng'osha alikuwa makamu mkuu wa shule,Dulla ndo boss. Lupenza nidhamu pale,mzee wa kukamata simu na kipiga paa.Nyarugwe kihelehele na mtoa vizigo,pia mpenda sifa. Maandazi ya mama simon. Mr.Kazi,ORGANIC CHEMISTRY. I miss you Tabora School,The head of Tanzania!
 
Aisee mi nimepita hapo T.boys mwaka 2003,nakumbuka kila jmoc tulikua tunaenda mitaa ya ng'ambo kucheck movie za wakubwa ucku tukirudi kila mtu na njia yake.
Nakumbuka siku1 niko form1(2000) kulikua na disco Warsaw halafu wakawaalika mahasimu wetu Milambo,basi tukawasubiri jamaa wanatoka disco mida ya Saa1 jioni tukawapa kichapo sn basi jamaa walichokifanya wakenda kujioganize na watu wa mtaani wakaja usiku wa saa7,basi sisi hatuna habari yyte wengine tumelala mana kulikua na kijimvua flan hv tukaanza kusikia vilio watu wanapigwa fimbo,mawe,ngumi yn jamaa walitufanyia ambush ya ajabu yn ilikua shika pata.

Basi ilibidi tutumie mbinu za kijeshi kuwakabili,unajua tulifanyaje?kwanza tulizima umeme shule nzima halafu tulikua tunatumia neno moja linaitwa "COI",yn ukikutana na mtu gizani unamuuliza coi inatakiwa nae ajibu coi asipijibu basi ujue ni adui na unaanza kumpa kichapo,basi kwa mbinu hyo jamaa tuliwachapa usiku mzima hadi wakakimbia
Duh T.boys ilikua ni shida enzi hizo
 
Mi nilikuwa naishi chemba moja inaitwa WACHINJA KOBE hatari sana, 2010 kombe la dunia kuna jamaa mmoja alikuwa anaitwa PS mechi ya ghana na Uruguay alikuwa anashabikia peke urugway alivunja rekodi ya kubishana na shule nzima
 
Duuuh! Boys raha sana. Madam Ng'osha alikuwa makamu mkuu wa shule,Dulla ndo boss. Lupenza nidhamu pale,mzee wa kukamata simu na kipiga paa.Nyarugwe kihelehele na mtoa vizigo,pia mpenda sifa. Maandazi ya mama simon. Mr.Kazi,ORGANIC CHEMISTRY. I miss you Tabora School,The head of Tanzania!
Kjana inaonekana ni wa miaka yetu ya karibuni, Nakumbuka mabango ya dula "tulipokojolewa" na waoso form6 2012, Lupenza,kamlali,Nyasebwa wazee wa nidham.Pia ndoto za kua maTO mnapoingia uboyzini, Moment nayokumbuka siku tumeshinda umiseta wadau wakakimbia mpaka warsaw dogo m1 akavua akabaki na boxer, viva "THE HEAD OF TANZANIA"
1461949917974.jpg
1461949953341.jpg
 
Mimi nilikua Old Traford Chamber bweni la Mkwawa pale juu kama unaenda Galapagos

Nakumbuka misuli mirefu ya waboyzia kwenye korido za madarasa

Nakumbuka kudoji usiku kwenda kwa Chief kusoma Kemia na Bios,

Napamiss Warsaw, palinipa mtoto mzuri kipepeo
 
Duuuh! Boys raha sana. Madam Ng'osha alikuwa makamu mkuu wa shule,Dulla ndo boss. Lupenza nidhamu pale,mzee wa kukamata simu na kipiga paa.Nyarugwe kihelehele na mtoa vizigo,pia mpenda sifa. Maandazi ya mama simon. Mr.Kazi,ORGANIC CHEMISTRY. I miss you Tabora School,The head of Tanzania!
dullah walimuhamishia kijijini kwenye shule ya kata inaitwa ibiri sec.
 
Mi nilikuwa naishi chemba moja inaitwa WACHINJA KOBE hatari sana, 2010 kombe la dunia kuna jamaa mmoja alikuwa anaitwa PS mechi ya ghana na Uruguay alikuwa anashabikia peke urugway alivunja rekodi ya kubishana na shule nzima
ps nampata, alikua muha, rafiki yake mramba, dah kwa muha ubishi kawaida...
 
Kuna kijana nimemfundisha pale miaka ya 2011-2013 .siku moja nahudhuria msiba hapa mwanza nikauliza huyu aliyefariki ni nani?nikaambiwa ni kihana alikuwa chuo kikuu anasomea umeme shule alimalizia boys.duuu nilistuka sana.
 
mimi nilipita nikienda girlz nikiwa na patner wangu tukienda kurekebisha umeme baada ya kuagzwa na ofis yetu ya temesa, ila watoto wana adabu wale nouma sana.
 
Boyfriend wangu wa kwanza nilimpataga siku tumeenda kucheza Tabora Boys.
Alikua na maakili anafaulu kweli. Akanitoaga bikra.
Umefanya nicheke vibaya sana. Vip hiyo stail ya disco ilikuaje mchuchumio wake madame, ebu tiririka basi jinsi ulivyopoteza bikra
 
I hate single sex schools,, sijawahi soma tofauti na mixture... Single sex schools ndo zinatuzalishia gays and lesbians bila kusahau huandaa wanachama machachari kabisa wa CHAPUTA.
Raha ya shule usome na opposite sex bwana
 
Mimi nimepita boys kwa mwezi mmoja tuu nkashindwa.
Nilitokea private Olevel.. walimu wote wapo, hatufanyi chochote zaidi ya darasani morning,
shida Ilitokea nakutana na kufagia monn, mara kudeki DH under Mr Nyalugwe, ratiba ya msosi shida kwangu while head master mbabe Mr Marwa anapiga vibao hatari nikaona hapa kuna kufa.. mapemaaaa nkachukua pass kwa academic Mr Tantau nkarudi zangu private.
Bwana Nyasebwa anakuchekea lakini hapo hapo anakupa mvua ya fimbo.
Thanks GOD nilipata One na loan juu
Mbona kama mboyzia wa hivi karibuni umemaliza mwaka gani?.
 
Back
Top Bottom