kiss ov love
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 9,363
- 16,099
Habari za muda mrefu wana jukwaa, ni matumaini yangu mu wazima wa afya kwa wenye changamoto mbali mbali Mungu awafanyie wepesi.
Leo ni sikukuu ya Eid kwa ndugu zetu waislamu, Eid Mubarak. Kama ilivyo ada ndugu jamaa na marafiki kwenye matukio kama haya ya sikukuu huwa tunaalikana.
Basi jana jioni kuna classmate ama rafiki yangu wa enzi hizo huwa nawasiliana naye akanipa mualiko, nilifurahia kwakweli maana tangu sikukuu kukaribia na kuanza sikuwahi kupata mualiko wowote.
Sasa leo nilienda eneo la tukio nikawakuta ndugu zake hapo baba ake mdogo anachoma nyama, wengine wapo ndani wanakula, nami nikajumuika nao, kusema ukweli nyama zilikuwa ni tamu sana, lakini kwa upande wa pilau sijaelewa naweza kuungana na yule jamaa aliyesema wakristo hatujui kupika chakula kitamu maana huyu aliepika ni mama yake mdogo ni mkriso.
All in all namshukuru na nilienjoy hiyo minyama maana ndiyo kitu napenda😁✊️
Wenzangu mliopata mialiko na msiopata leo mmekula nini??